Monday, 6 April 2015

mtoto azaliwa bila pua

mtoto aliyezaliwa bila pua
Eli Thompson alizaliwa tarahe nne Machi jioni, lakini alikuwa na kasoro moja, hakuwa na pua.
Siku niliyojifungua, kila kitu kilikuwa sawa.'' Mamake Brandi McGlathery ameambia ABC News Today nchini Marekani.
''Alipozaliwa daktari alimweka kifuani mwangu. Nilipomwangalia kwa karibu, nilisema ' Hana pua'. Walimchukua na kutoka naye.
McGlathery amesema kwamba daktari alikaa kando ya kitanda chake ili kumweleza hali ya mtoto wake. ''Alikuwa amehuzunika..''Amesema.'' Nilijua papo hapo kuwa hakuwa sawa.''
Hata ingawa mtoto wake hakuonyesha kasoro zozote zaidi, McGlathery amesema kuwa alishangazwa na kuhuzunika kutokana na habari hizo.
Lakini licha ya kukosa pua, Brown amesema kuwa mtoto huyu ana afya nzuri na pia ni mtoto mrembo.
Share:

boko haramu yawauwa watu 20 nigeria....


Watu 20 wameuawa mashariki mwa Nigeria kufuatia mashambulizi mapya yanayoendeshwa na kundi la Boko Haram katika eneo hilo.
Eneo la kwaJaffa, katika jimbo la Borno, lilishambuliwa Jumapili jioni na washambulizi hao waliowashambulia wananchi na baadaye kuteketeza nyumba zao.
Majuma machache yaliyopita miji kadhaa na vijiji vilikombolewa na wanajeshi wa Nigeria wakisaidiwa na Chad, Cameroun na Niger.
Mwanamume aliyetoroka mji wa Kwajaffa wakati wa mashambulizi ya kundi hilo la Boko Harram amerudi nyumbani kwake na kupata kumeharibika pakubwa. 

Aliambia BBC kuwa alihesabu maiti za raia waliokuwa wamepigwa risasi na wanamgambo wa Boko Harram na alipata maiti zingine zilizokuwa zimeteketezwa.
Shambulio hilo linadhaniwa kuwa adhabu kwa jamii nzima kwa sababu karibu nyumba zote ziliteketezwa.
Boko Haram lina tabia ya kulenga maeneo ambayo raia wameunda makundi ya ya kiusalama ambayo wakati mwingine hushirikiana na wanajeshi wa Serikali.
Vijiji viwili katika eneo la Kala Balge lililo karibu na mpaka na Cameroon pia vilishambuliwa na watu 14 waliuawa.

Washambulizi hao wamefukuzwa katika miji na vijiji vingi na jeshi la muungano wa mataifa jirani ambayo yangali nchini humo.
Hata hivyo mauaji ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa raia wengi wangali katika hatari ya kushambuliwa wakati wowote.
Zaidi ya watu milioni moja waliotoroka makwao bado hawawezi kurudi nyumbani kwa sababu hakuna usalama.
Share:

kenya yatekeleza shambulizi somalia

Ndege za kijeshi za Kenya zashambulia Somalia
Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi ameiambia BBC.
Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.
Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita.
Amisom
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.
Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive