Tuesday, 1 October 2013

Bayern na mtihani dhidi ya Manchester City

Kocha wa Bayern Pep Guardiola atakabiliwa na mtihani mwingine dhidi ya timu ya premier League, katika Champions League baada ya kupata ushindi wa kombe la Super Cup dhidi ya Chelsea kupitia mikwaju ya penalti 
 
 
Mlinda lango wa Bayern Manuel Neuer anasema huu utakuwa mchuano wa timu mbili zenye nguvu sawa, wakati naye nahodha wa Manchester City Vincent Kompany akiwataka wenzake wakaze buti baada ya kichapo cha mabao matatu kwa mawili dhidi ya Aston Villa.
Katika kundi F, Arsenal ambao maisha yao yanaonekana kuwa ya starehe wakati wakiongoza Ligi Kuu ya England, watakuwa wenyeji wa Napoli. Timu zote mbili zilishinda mechi zao za kwanza za Champions League.
Nao Borussia Dortmund wana mchuano wa nyumbani dhidi ya Olympique Marseille. Baada ya kichapo cha nyumbani cha mabao mawili kwa moja na West Bromwich Albion Jumamosi iliyopita katika Ligi ya nyumbani, mbinyo unazidi kuongezeka dhidi ya kocha wa Manchester United David Moyes kabla ya mpambano wao wa Jumatano ugenini na Shakhtar Donetsk katika kundi A
 
Kevin Prince Boateng ameongeza makali katika ushambuliaji wa Schalke tangu alipojiunga nao msimu huu
kevin Prince Boateng ameongeza makali katika msimu huu ushambuliaji wa Schalke tangu alipojiunga nao
 
 AC Milan inawakaribisha tena kikosini Riccardo Montolivo na Stephan El Shaarawy baada ya kupona majeraha yao pamoja na Mario
 Balotelli ambaye amepumzika vya kutosha, wakati watakapochuana na Ajax mjini Amsterdam katika mechi ya kundi H hapo kesho. Barcelona watasafiri mjini Glasgow kupambana na Celtic hapo kesho katika mechi ya kundi H, bila ya huduma za mashambuliaji wao Lionel Messi. Muargentina huyo alipata jeraha katika mguu wake wa kulia mwishoni mwa wiki lakini Neymar yuko tayari kulijaza pengo hilo.
Atletico Madrid watasafiri hadi Porto katika mchuano wa kundi G. Real Sociedad watajaribu kujikwamua ugenini dhidi ya Bayer Leverkusen katika mechi ya kundi A. Schalke wa Ujerumani wako na kibarua dhidi ya Basel katika mechi ya kundi E, baada ya timu hiyo ya Uswisi kubwaga Chelsea mabao mawili kwa moja katika mchuano wa kwanza nao Schalke wakawapiku Steaua Bucharest mabao matatu bila jawabu. Sasa kocha wa Chelsea Jose Mourinho anasema Juan Mata ataanza katika mchezo wa kesho dhidi ya Steaua ambao ni lazima aishinde. Katika kundi C, Paris St Germain watapambana na Benfica nao Anderlecht wakiwaalika Olympiakos siku ya Jumatano.
Share:

Kenya yawaombea wahanga wa shambulizi la Westgate

Ni siku 9 sasa tangu mkasa wa Shambulizi la magaidi kutokea katika Jumba la kibiashara la Westgate mjini Nairobi, Kenya. Serikali imeandaa maombi ya kitaifa yanayojumuisha dini zote kuombea usalama wa nchi 
  Maombi hayo pia ni ya kuwafariji wale waliopoteza wapendwa wao kwenye shambulizi hilo la magaidi lililosababisha vifo vya watu 67 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.
Viongozi wa dini mbali mbali wamekusanyika katika uwanja wa jumba la KICC kwa maombi ya kitaifa kuombea nchi, manusura na jamaa za waliopoteza wapendwa wao kwenye shambulizi la magaidi Shambulizi hilo lililofanyika tarehe 22 mwezi huu. Maombi hayo yamehudhuriwa na wakuu wa serikali wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Rutto, mawaziri na wabunge.
 Bado kuna maswali mengi yaanyostahili majibu kuhusu namna serikali ilivyolishughulikia shambulizi hilo
 Bado kuna maswali mengi yaanyostahili majibu kuhusu namna serikali ilivyolishughulikia shambulizi hilo

Pia viongozi wa upinzani wa muungano wa CORD wakiongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga akiandamana na viongozi wa vyama tanzu wa muungano huo, aliyekuwa makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na wengineo walijumuika pamoja katika uwanja wa jumba la mikutano ya Kimataifa KICC.
Maombi hayo yanahudhuriwa na viongozi wa didi mbali mbali wakiwemo wakristo, Waislam, 
Wahindu na dindi nyinginezo. Viongozi wa dini ya kiislam wameendelea kukikashifu kitendo 
 hicho cha magaidi na kusihi vyombo vya usalama kutohusisha ugaidi na Uislam.. Huku maombi hayo yakiendelea kundi la wataalam wa uchunguzi kutoka mataifa mbali mbali wanaendelea na uchunguzi wao katika jumba la Westgate Mall kutafuta ushahidi kuhusiana na shambulizi hilo. Maafisa kutoka Uingereza, Ujerumani Marekani, Israel na Canada wakishirikiana na wenzao kutoka Kenya wanaendesha shughuli iliyoanza Jumatano iliyopita. Maswali mengi hadi sasa hayajapata majibu kuhusiana na shambulizi hilo lililodaiwa kuteklelezwa namagaidi wa kundi la Al-Shabaab walio na uhusiano na kundi la magaidi la Al-Qaeda. Washukiwa tisa bado wanahojiwa na polisi kuhusian na shambulizi hilo. Serikali imesema magaidi 5 waliuawa kwenye shambulizi hilo ingawaje hadi sasa hakuna hata maiti moja ya magaidi hao iliyotambuliwa.
Share:

Shughuli za serikali ya Marekani zaanza kufungwa

Sehemu kubwa ya shughuli za Serikali ya Marekani zimefungwa leo baada ya wabunge wa nchi hiyo kushindwa kuutatua mgogoro wa bajeti. Hali hiyo imetokea kwa mara ya kwanza baada ya miaka 17 
Malaki ya watumishi wa serikali wanarudishwa nyumbani bila ya malipo na idara nyingi za serikali zimeambiwa zifunge milango. Sehemu kubwa ya shughuli za serikali ya Marekani zimefungwa kwa sababu serikali hiyo haina bajeti ya matumizi ya kawaida. Mgogoro huo maana yake ni kwamba wafanya kazi wa serikali kuu hadi milioni moja watapewa likizo bila ya malipo.
Baadhi ya huduma za umma kama vile miradi ya utafiti wa tiba zinazoendeshwa na idara za serikali pia zitasimama. Marekani imefikia hatua hiyo baada ya baraza la seneti linalodhibitiiwa na chama cha Rais Obama cha Demokratik kulikataa pendekezo la wajumbe wa chama cha Republican la kuusimamisha mpango wa huduma za afya wa Rais Obama.
Wabunge wa chama cha Republican wanaolidhibiti baraza la wawakilishi walitaka mchakato wa nipe nikupe na chama cha Demokratik. Wabunge wa Republican walikuwa tayari kuipitisha bajeti lakini kwa sharti la kuusimamisha mpango wa afya wa Obama ambao umeanza kutekelezwa leo.
Mpango wa Rais Obama wa huduma za afya kwa Wamarekani unavurugwa na wabunge wa Republican 
 Mpango wa Rais Obama wa huduma za afya kwa Wamarekani unavurugwa na wabunge wa Republican

Juu ya kufungwa kwa shughuli za serikali Rais Barack Obama amesema. "Kwa bahati mbaya bunge halikuutimiza wajibu wake." Hata hivyo baadhi ya wizara zitaendelea kufanya kazi kama vile ya ulinzi. Rais Obama aliwatumia wanajeshi ujumbe wa video kwa kusema. "Kama amirijeshi wenu nimehakikisha kwamba mtaendelea kuwa na uwezo, zana na yote mnayoyahitaji ili kuutekeleza wajibu wenu kwa taifa. Vitisho kwa taifa letu bado havijabadilika na hivyo tunawataka muwe tayari kwa dharura yoyote"

Kila upande unaulaumu mwingine kwa kushindwa kufikiwa kwa makubaliano. Rais obama ametahadhrisha juu ya madhara ya kiuchumi yanayoweza kutokea kufuatia kusimamishwa kwa shughuli za serikali. Amesema kasi ya ustawi wa uchumi inaweza kuvurugika.
Hatua iiyofikiwa leo pia inasababisha wasi wasi iwapo Marekani italifikia lengo lake hadi kati kati ya mwezi wa oktoba la kuongeza deni la serikali hadi dola Trilioni 16.7. Hisa barani barani Ulaya zimepanda juu kidogo mapema leo lakini wawekaji vitega uchumi wameingiwa wasi wasi.
Hata hivyo wachunguzi wanaamini kuwa wabunge wa Marekani watakaa chini pamoja haraka ili kutafuta ufumbuzi. Licha ya kuwa suala muhimu kwa masoko, madhali pana matumaini, masoko hayataathirika sana. Hayo ameyasema mtaalamu wa masuala ya fedha wa Unicredit mjini Munic, Christian Stocker. Wakati huo huo uchunguzi wa maoni umeonyesha kuwa chama cha Republican kitalaumiwa na wananchi wengi wa Marekani kwa kufungwa kwa shughuli za serikali.
Share:

MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI

 
 Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni. Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo. 

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.


Ameongeza kuwa amelazimika  kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.

Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela  

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
 
Share:

GAIDI WA KIKE WA AL SHABAAB SAMANTHA KATIKA MAPOZI MBALI MBALI YA KICHOKOZI


Samantha Louise Lewthwaite, (born 5 December 1983), also known as Sherafiyah Lewthwaite or the White Widow, is the widow of 7/7 suicide bomber Germaine Lindsay and one of the United Kingdom's most wanted terrorism suspects She is currently a fugitive from justice in Kenya, where she is wanted on charges of possession of explosives and conspiracy to commit a felony and is the subject of an Interpol Red Notice requesting her arrest with a view to extradition. Below are some photos of her

 
 
Share:

Mancini kwenda Uturuki


Kocha wa zamani wa Manchester City ,Roberto Mancini anazungumza na mabingwa wa Uturuki Galatasaray kuhusu nafasi iliyo wazi ya kocha wa klabu hiyo. 
kocha wa zamani wa klabu ya manchester city
Roberto mancini
Mancini alifutwa kazi Manchester City

Klabu hiyo ya mjini Istanbul ilithibitisha katika mtandao wa Twitter kwamba Mancini amekutana na wakurugenzi wa klabu hiyo na kupigwa picha na mkurugenzi mkuu , Lutfi Aribogan.
Mtaliana huyo anatarajiwa kushika nafasi ya Fatih Terim, ambae alipigwa kalamu wiki iliyopita baada ya kushindwa kukubaliana mkataba mpya.
Manchester City ilimfuta Mancini mnamo mwezi wa Mei mwaka mmoja baada ya kuongoza hadi kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Galatasaray imeanza vibaya msimu wa soka Uturuki ikishinda mechi moja tu kati ya michuano mitano ya kwanza .
Katika michuano ya klabu bingwa ya Ulaya ilicharazwa na Real Madrid,kwa mabao 6-1.
Terim, mwenye umri wa miaka 60, aliongoza Galatasary kushinda mara 6 ubingwa wa Uturuki pamoja na kombe la UEFA mwaka 2000 baada ya kuichezea kwa kipindi cha miaka 11.
Mancini ameshinda ubingwa wa Italia mara tatu akiwa na Inter Milan ya Utaliana kabla ya kunyakua kombe la FA na ubingwa wa ligi na Manchester City.
Share:

Wabunge, Kenya - wakimbizi waondolewe !





Kamati ya bunge inayohusika na ulinzi na uhusiano na mataifa ya kigeni imependekeza kufungwa kwa kambi za wakimbizi nchini Kenya, ikisema zinatishia usalama wa nchi.Kambi ya wakimbizi ya Dadaab, Kenya.
 Kambi ya wakimbizi ya Dadaab, Kenya

Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndungu Githinji amesema kuwa wana habari kuwa kambi zilizoko kwenye mipaka ya Kenya hutumika kuwapa mafunzo wapiganaji wa kiislamu.
Kenya inahifadhi wakimbizi wa kisomali zaidi ya nusu milioni katika kambi za Dadaab zilizoko kwenye mpaka na Somalia.
Mwenyekiti huyo Ndungu Githinji ameambia BBC kuwa miaka 22 imetosha kwa usaidizi kwa wasomali hao na wanastahili sasa kurudi nyumbani baada ya amani kurejeshwa nchini mwao.
''Hawa wakimbizi wamekaa miaka ishirini na mbili Kenya. Ningependa kuuiomba UN ifunge kambi hizo. Iwarudishe wasomali kwao, maana sasa nao pia wanayo serikali yao. Ili tuweze kukaa kwa amani.''Amesema bwana Githinji.

Lazima usalama uimarishwe

Bwana Githinji pia ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuzidisha usalama na doria katika maeneo yanayotishiwa kushambuliwa na Al shabaab.
''Tunasikia AL shabaab wanasema kwamba bado wanataka kutupiga. Naomba kuwa zile sehemu zote walizotoshia kushambulia zipewe ulinzi wa kutosha kwa saa ishirini na nne.''
Wanamgambo wa Alshabaa wamekuwa wakijihusisha na waislamu katika harakati zao huku wakidai kuwa wanapigania haki ya dini ya kiislamu nchini Somalia na hata mataifa jirani kama vile Kenya.
Pia wamekuwa wakilenga Kenya kwa mashambulio kufuatia hatua ya Kenya kuingia nchini Somalia mwaka wa 2011 kuwaondoa wanamgambo hao kwa madai kuwa wanatishia usalama wa nchi.
Kutokana na hilo wabunge waliozuru eneo la shambulio kule Westgate wamefurahishwa na hatua ya waislamu nchini Kenya kujiepusha na kundi hilo la AL-Shabaab.
Mwenyekiti Githinji asema, '' Ningependa kupongeza viongozi wa waislamu ambao wametoa taarifa yao kuwa hawaungi mkono mashambulio haya.''
Mwandishi wa BBC jijini Nairobi anasema kuwa wito huu wa kufungwa kwa kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma, zimekuwepo kwa muda. Wakenya wengi wanahisi kuwa Kuwepo kwa wakimbizi hao kumeendelea kuiweka nchi hiyo katika hatari ya mashambulio. Lakinim bali na hilo.
Pia baadhi wanahisi wakimbizi hao ndio wa kulaumiwa kwa kupanda gharama ya makaazi hasa katika maeneo ya Nairobi kama vile Eastleigh, wanakoishi kwa wingi zaidi.

Share:

Saturday, 14 September 2013

Upinzani Syria wakana makubaliano




  • Mkuu wa kijeshi wa upinzani nchini Syria, Jenerali Selim Idris, amekataa makubaliano baina ya Marekani na Urusi kuhusu silaha za kemikali za Syria.Mpiganaji wa Syria katika mji wa Deir Ezzor, mashariki mwa nchi 
  • Akizungumza na waandishi wa habari nchini Uturuki, Jenerali Idris alisema makubaliano hayo hayatamaliza msuko-suko wa sasa.





    Amesema upinzani utaendelra na vita.

    Aliwashauri Wamarekani wasidanganywe na pendekezo la Urusi ambalo alisema linakusudia kuvuta wakati.

    Inaarifiwa kuwa mapambano yanaendelea baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa upinzani katika vitongoje vya Damascus vinavyodhibitiwa na wapiganaji.

    Walioshuhudia wanasema ndege za jeshi la Syria zinafanya mashambulio. 
Share:

Monday, 19 August 2013

HUYU NDIYE PRODYUZA ALIYE PIGA PICHA CHAFU NA WANAMITINDO

PRODYUZA mkali Bongo, Manaiki Sanga amekumbwa na skendo ya aibu kufuatia picha zake chafu akiwa na wasichana wanaodaiwa ni wasanii wa filamu kusambaa mitandaoni huku wachangiaji wakisema ni udhalilishaji uliopitiliza,.

Picha hizo mbalimbali zinamuonesha Manaiki na wasanii hao wakiwa katika mapozi tofauti huku wakiashiria kwamba walikuwa wanajua wanarekodiwa.
Baadhi ya picha zinamuonesha prodyuza huyo akiwa na msanii mmoja, tangu ana nguo zake zote kisha kuanza kuzivua moja baada ya nyingine hadi kubaki kama alivyozaliwa

Chanzo; Yaani picha za kwako halafu unasema hujaziona, si ulipiga wewe?”
Manaiki: Kwani zimetapakaa kwenye mtandao gani?”
Alipotajiwa jina la mtandao mmoja tu kati ya mingi yenye picha hizo, prodyuza huyo alisema anamfahamu mmiliki wake hivyo atampigia simu muda si mrefu.




Matukio hayo yote yalifanyika ndani ya chumba kimoja ambacho haijajulikana kama ni hotelini, gesti au nyumbani kwa prodyuza huyo lakini hisia za macho zinasema ni sehemu ngeni na makazi yake.
Kumbukumbu za nyuma zinaibua mahojiano kati ya prodyuza huyo na mtangazaji wa redio moja ya jijini Dar, akiulizwa kuhusu taarifa kwamba amekuwa na tabia ya kupiga picha chafu ambapo majibu yake yalikuwa yakijigongagonga

Ili kuupata ukweli wa picha hizo ambazo nyingi zinazua kichefuchefu kiasi cha kushindwa kutumika gazetini, juzi, chanzo chetu kilimsaka Manaiki kwa njia ya simu ya mkononi ambapo alipopatikana na kusomewa mashitaka alisema:
“Mi sijui lolote bwana, wala sijaziona kwanza.”


Share:

Mwigulu akwama kumzuia Dk. Slaa

 NAIBU Katibu Mkuu (Tanzania Bara) wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Mchemba, ameambulia patupu baada ya mikakati yake ya kutaka kukwamisha mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kushindikana.

Tukio hilo lilitokea juzi jimboni Iramba Magharibi ambalo analiongoza Mwigulu, ambapo Dk. Slaa alifanikiwa kuwahutubia mamia ya wananchi katika mchakato wa chama hicho kukusanya maoni ya wafuasi wao juu ya rasimu ya kwanza ya Katiba mpya.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, Mwigulu alijaribu kufanya kila mbinu ili mkutano wa Dk. Slaa ukose watu wa kumsikiliza lakini ilishindikana.

Tofauti na mikutano mingine ya CHADEMA ambayo ameihutubia Dk. Slaa katika mchakato huo, juzi hali ya ulinzi ilikuwa tofauti kidogo kutokana na polisi wengi kutanda eneo la mkutano la uwanja wa soko la zamani la Kiomboi wilayani Ilamba wakiwa na silaha za moto.

Askari hao ambao walikuwa wamezunguka eneo alilokuwa akihutubia Dk. Slaa, walivalia
kofia ngumu kama vile wanakwenda katika mapambano, jambo ambalo wananchi walidai kuwa ulikuwa ni mkakati wa kuwatisha wasijitokeze kumsikiliza kiongozi huyo.

Pamoja na jitihada hizo, wananchi walijitokeza kwa wingi kumsikiliza Dk. Slaa na kisha kutoa maoni yao kwa njia ya kujaza fomu na wengine kwa kuzungumza mkutanoni.

“Kusema ukweli usione tumejitokeza hapa ni kutokana na ujasiri wetu vinginevyo hali hii kwa wananchi wa kawaida lazima waogope maana askari hawa wanaonekana kama vile wamekuja kupambana,” alisema mmoja wa wakazi wa Kiomboi ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Katika kuhakikisha wananchi hawahudhurii mkutano huo, siku moja kabla yalitolewa matangazo ya kuwaalika watu kwenye mashindano ya mpira wa miguu kati ya timu ya Kiomboi na Simba ya Dar es Salaam ambayo ililetwa na mbunge huyo, wakielezwa kuwa kiingilio ni bure.

Chanzo chetu kiliongeza kuwa baada ya viongozi wa CHADEMA kunasa mbinu hiyo, walijitahidi kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuhudhuria mkutano huo wa juzi, wakisema haukuwa wa siasa walizozizoea bali ni kuwataka watoe maoni yao juu ya rasimu ya Katiba mpya.

Akiwahutumia wananchi hao, Dk. Slaa alisema kuwa kuna vipengele vingi ambavyo wanaviunga mkono katika rasimu hiyo ingawa kuna baadhi vinahitaji marekebisho.

Alifafanua kuwa vipengele vingi ni vizuri japo CCM wanavipinga, huku akidai kwamba kitendo cha chama hicho tawala kupinga kipengele cha uwazi katika tunu za taifa pamoja na rushwa ni hatari katika taifa.

“Tunamuunga mkono Jaji Joseph Warioba katika vipengele vingi hasa katika kipengele cha kulinda rasilimali za taifa, uwazi katika mikataba lakini wenzetu wa CCM wamepinga kwamba uwazi usiwemo katika Katiba mpya sijui malengo yao nini. Kwa hiyo wananchi mnatakiwa kuamua wenyewe maana chama chenu hakitaki mambo mazuri yawekwe katika Katiba yenu,” alisema.

Naye mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mabere Marando, alitoa ufafanuzi kuhusu mapendekezo ya serikali tatu ambazo alieleza kuwa CCM inapinga mapendekezo hayo.

Marando alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wanasiasa wa CCM kuwapotosha wananchi kwamba serikali tatu ni mzigo kwa taifa si cha kweli na kwamba serikali ya sasa ndiyo mzigo kwa taifa.

“Kwa kuzingatia mapendekezo kuhusu Bunge la Jamhuri ya Muungano katika aya ya 105, kwa idadi ya sasa na mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar, Bunge la Jamhuri ya Muungano litakuwa na wabunge 75 tu.

“Kwa mapendekezo ya muundo wa serikali tatu, Bunge la Zanzibar litakuwa na wabunge 50 wa kuchaguliwa wakati Bunge la Tanganyika litakuwa na wabunge 189 wa majimbo ya uchaguzi,” alisema.

Marando aliongeza kuwa muundo wa muungano wa serikali tatu utakuwa na wabunge 314 tu; kwamba upo uwezekano wa idadi hiyo kupungua zaidi wakati wa mchakato wa kuandika Katiba ya Tanganyika na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.

Kuhusu Bunge la sasa ambalo linasemekana kuwa na unafuu, Marando alisema lina wabunge 357 ambapo 189 wanatokana na majimbo ya Tanzania Bara, majimbo 50 ya Zanzibar, Viti maalumu 105, kuteuliwa na rais 10, wanawakilisha watano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa serikali.

Aliongeza kuwa kwa mabunge mawili ya sasa yana idadi ya wabunge 438 na kwamba idadi hiyo ni kubwa kuliko idadi ya wabunge wa mabunge matatu yatakayokuwepo chini ya muundo wa serikali tatu.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kuchangia walionekana kuchukizwa na madaraka makubwa ya Rais huku wakipendekeza kipengele cha kupunguza madaraka ya Rais kiingizwe kwenye Katiba.

Wananchi wengine walipendekeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe huru ili Rais asiweke mkono wake badala yake kiundwe chombo huru cha kuwachagua viongozi wa tume hiyo.

‘CCM imevunja Muungano’

Kutoka mkoani Kagera, mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amesema kuwa CCM tayari imeuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kutokana na muundo wa Katiba mbili za Muungano na ile ya Zanzibar.

Akiwahutubia wanachi waliohudhuria mikutano ya mabaraza ya wazi ya CHADEMA ya kujadili rasimu ya Katiba mpya mjini Bukoba, Lissu alisema kuwa Katiba hizo mbili zinaonyesha mkanganyiko wa wazi unaovunja Muungano.

Alisema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka wazi katika ibara yake ya kwanza kwamba Tanzania ni nchi moja ya Jamhuri ya Muungano, wakati ile ya Zanzibar nayo inatamka kuwa Zanzibar ni nchi, hivyo kuzifanya ziwe nchi mbili zenye madaraka kamili.

“Tanzania si nchi moja kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, kwa sababu Muungano ulioasisiwa na Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume, tayari umekufa na CCM ndiyo imeuua,” alisema.

Lissu alifafanua kuwa Zanzibar tayari ina alama zake ikiwemo wimbo wa taifa, rais wake ambaye ni mkuu wa vikosi vya idara maalumu, mahakama yake na bendera yake.

“Kuna haja sasa kufufuka Tanganyika kama Tume ya Jaji Warioba ilivyopendekeza kuwa na serikali tatu. Leo Jamhuri ya Watu wa Zanzibar imefufuliwa, kwa maana hiyo hakuna budi pia kufufuliwa kwa Jamhuri ya Tanganyika kutoka katika ‘wafu’,” alisema.

Share:

Sunday, 18 August 2013

Maandamano kumng’oa meya Ilemela leo

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza, kimeitisha maandamano makubwa ya amani leo kwa ajili ya kushinikiza kung’olewa kwa meya wa manispaa hiyo, Henry Matata, anayedaiwa kuchaguliwa kinyume cha sheria.

Akitangaza maandamano hayo mbele ya waandishi wa habari jijini hapa jana, Ofisa Operesheni wa CHADEMA Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, alisema yataungwa mkono na maelfu ya wananchi wa Nyamagana.

Alisema maandamano hayo yataanzia Buzuruga saa 4:00 asubuhi kisha kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, katika uwanja wa Furahisha, na kwamba unahitajika kufanyika upya uchaguzi wa meya na naibu wake.

Tungaraza aliyeongozana na ofisa wa chama kanda hiyo, Meshack Mikael, pamoja na katibu wa mbunge wa Ilemela, Laban Agrey, alisema maandamano hayo yanahusisha pia kupinga kufukuzwa kinyemela madiwani watatu wa chama hicho.

Madiwani waliofukuzwa na meya wa manispaa hiyo kinyume cha sheria ni Abubakar Kapera (Nyamanoro), Malietha Chenyenge (Ilemela) na Dany Kahungu wa kata ya Kirumba.

“CHADEMA tumeitisha maandamano makubwa hapo kwa lengo la kumkataa meya wa Ilemela na kushinikiza uchaguzi ufanyike upya.

“Matata amechaguliwa bila kukidhi akidi ya madiwani wa manispaa hiyo ambayo ni theluthi mbili ya madiwani wote 14, hivyo siyo meya.

“Lakini maandamano haya yatalenga pia kupinga Matata kuwafukuza madiwani wetu kinyemela. Sheria zinasema diwani atakosa sifa baada ya kutohudhuria mfululizo vikao vitatu vya Baraza la Madiwani, lakini Matata aliyechaguliwa kinyume cha sheria aliwafukuza ndani ya wiki moja baada ya kuchaguliwa,” alisema.

Alisema CHADEMA pamoja na wananchi wa Ilemela wanahitaji kufanyika upya kwa uchaguzi wa meya na naibu wake na kwamba kama kweli madiwani hao wamefukuzwa kihalali wapewe barua za kufukuzwa kwao na tume ya uchaguzi itangaze kata hizo kuwa wazi.

“Kuna taarifa zinaeleza kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alishaandika barua ya kutengua uamuzi wa kufukuzwa madiwani hao na barua hiyo ‘imekaliwa’ na mkuu wa mkoa,”alisema.

Naye katibu wa Highness Kiwia, Laban Aggrey, kwa niaba ya mbunge huyo alisema kuwa maandamano hayo yataanzia Buzuruga kisha kupita barabara ya Nyerere, Mlango mmoja, Uhuru, Nkrumah, Balewa na kuishia uwanja wa Furahisha.

“Polisi wameshabariki kufanyika maandamano yetu, hivyo ofisi ya mbunge wa Ilemela inawasihi sana wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kudai haki yao iliyoporwa kinyume cha sheria,” alisema.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu, alisema maandamano hayo ya CHADEMA yameruhusiwa na jeshi lake.

“Haya maandamano tumeyaruhusu kabisa yafanyike, maana kama watu wanasema wanadai haki yao kwa nini tuwazuie? Tumewapangia maeneo ya kupita maandamano haya hadi huko Furahisha,” alisema Mangu.

Uchaguzi wa meya wa Ilemela uliofanyika Desemba mwaka jana, ulikiuka kanuni na sheria za halmashauri, ambapo akidi ya wajumbe iliyokuwa ikihitajika kwa ajili ya meya kupigiwa kura ni madiwani tisa, lakini ni madiwani sita tu ndiyo waliopiga kura.

Katika uchaguzi huo uliohudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo, Amina Masenza (DC), pamoja na mwanasheria wa jiji la Mwanza, Savela Manzi, aliyesimamia uchaguzi huo kwa upande wa mambo ya sheria, Matata alitangazwa kuwa meya baada ya kuchaguliwa na madiwani wasiokidhi theluthi mbili.

Madiwani waliopiga kura kumchagua Matata na naibu wake (Dede Swila wa CCM), walikuwa wanne wa CCM, mmoja wa CUF ambaye ni mbunge wa viti maalumu, Mkiwa Kimwanga, na Matata mwenyewe aliyefukuzwa uanachama wa CHADEMA.

Matata alichaguliwa wakati suala lake la kufukuzwa uanachama ndani ya CHADEMA likiwa bado linangojea uamuzi wa mahakama.
Share:

Mwalimu amuweka kinyumba mwanafunzi

Adai shetani alimpitia, polisi wamkingia kifua

MWANAFUNZI wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Sokoine, Manispaa ya Dodoma (jina linahifadhiwa), anadaiwa kuwekwa kinyumba na mwalimu wake David Macha (30).

Mwanafunzi huyo wa miaka 14 ni kati ya watoto wanaofadhiliwa na shirika kisilo la kiserikali la Compassion International Tanzania kituo cha Tz 807 FPCT kilichoko Chamwino.

Hata hivyo, katika hali kushangaza Jeshi la Polisi mkoani hapa, limelalamikiwa na wazazi wa mtoto huyo kwa kitendo cha kumlinda mtuhumiwa licha ya kupewa taarifa za uhalifu huo kwa zaidi ya miezi mitano sasa, limeshindwa kumchukulia hatua.

Uchunguzi wa Tanzania Daima ambao umethibitishwa na wazazi wa mwanafunzi huyo, umebaini kuwa mwalimu Macha amekuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo kwa zaidi ya miezi mitano sasa.

Wazazi wa mwanafunzi huyo wanathibitisha kuwa kwa zaidi ya miezi mitano, mtoto wao alikuwa na tabia ya kutoroka nyumbani nyakati za usiku na kulala nje, jambo ambalo lilianza kuwatia mashaka na kuanza kufuatilia nyendo zake.

Walidai kuwa wakati mwingine alikuwa akirudi nyumbani asubuhi kwa ajili ya kujiandaa kwenda shule na anapoulizwa alikolala, alisema alikuwa katika mkesha.

Akisimulia mkasa huo, mjomba wa mwanafunzi huyo, Silas Mjengi, alisema binti yao anaishi na mama yake pekee katika eneo la Area ‘A’ mjini hapa baada ya mzazi huyo kutengana na mumewe.

Mjengi alisema kuwa baada ya kumbana binti yao, alikiri kufanya mapenzi na mwalimu huyo nyumbani kwake.

“Kwa muda mrefu nilipokea malalamiko toka kwa dada yangu juu ya vitendo vya mjomba wangu kuwa amekuwa akitoroka na kulala nje, ndipo nilipoamua kulifuatilia kwa umakini ikiwemo kumbana ambapo alikiri kuwa alikuwa anaishi na mwalimu kama mke na mume na hata kwenye simu yake alimwandika kwa jina la ‘my husband’,” alisema.

Kwa upande wake, mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Esther Mjengi, alisema kuwa baada ya kuona tabia ya mwanaye imebadilika alianza kumfuatilia ndipo marafiki zake walipomueleza ukweli kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu wake.

Alisema baada ya kufuatilia aliweza kumbamba akiwa nyumbani kwa mwalimu huyo kama mke wake na hata alipomfuata ili kuhojiana naye, aligoma kutoka ndani na ghafla alilazimika kuvua nguo na kumwachia blauzi ambayo alikuwa amevaa na kukimbia akiwa kifua wazi.

“Niliumizwa sana na mwanagu kujikita katika mapenzi na mwalimu, ukizingatia mwanagu bado ni mdogo na mwalimu ana miaka 30; wanangu naangaika nao sana kutokana na baba yao kutokuwa karibu nao, mbaya zaidi ni watoto ambao wanasoma kwa ufadhili wa Compassion Tanzania.

“Lakini baada ya kumbana alikiri kufanya ngono na mwalimu kwa zaidi ya miezi mitano sasa. Nilikwenda kushtaki kituo cha polisi cha kati Dodoma katika kitengo cha dawati la jinsia. Huweziamini! Sikutapa ushirikiano wowote; sijui nini kilifanyika kwani nilianza kubezwa badala ya kushughulikiwa na mtuhumiwa aliachiwa huru bila hata kuhojiwa,” alisema.

Tanzania Daima lilifanikiwa kuzungumza na mwanafunzi huyo, ambaye alikiri kuwa na uhusiano na mwalimu na kwamba alifikia uamuzi huo baada ya mwalimu huyo kumhudumia kwa vitu mbalimbali, ikiwemo kumpatia fedha.

“Aliahidi kunisaidia kwa kila kitu, kwani licha ya kunipa fedha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na shuleni, lakini pia alikuwa akininunulia nguo zangu za ndani, pamoja na simu ya mkononi aina ya Tecno,” alisimulia bila woga.

Ofisa Elimu Manispaa ya Dodoma, Winfrida Bario, alikiri kupokea taarifa za tukio hilo, akisema kuwa alikaa nao wote mzazi na mwalimu, ambapo mwalimu na mwanafunzi walikiri makosa yao ya kuwekana kinyumba.

“Nilichoagiza kwa polisi ni kuhakikisha hatua zinachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo kwani moja kwa moja amevunja kanuni na taratibu za kazi na hata kama ingekuwa vipi mwalimu huyo tayari ameishamharibu kisaikolojia mwanagunzi huyo.

“Mwanafunzi huyo yuko darasa la saba unafikiri anaweza kuwa na akili nzuri tena maana ameishamharibia kila kitu. Mbali na hili, kwa mwalimu wa miaka 30 kutembea na mwanafunzi wa miaka 14 ni kosa la ubakaji,” alisema ofisa elimu huyo.

Aliongeza kuwa kitendo hicho ni cha aibu kwani mtumishi wa umma hapaswi kukiuka maadili ya utumishi wake.

Naye mwalimu ambaye alibambwa kwa kosa hilo la kumweka mwanafunzi kinyumba alijitetea kuwa alifanya hivyo kutokana na tamaa za mwili lakini si tabia yake.

“Ni kweli nilikuwa naishi na mwanafunzi huyo lakini mimi si tabia yangu bali shetani alinipitia, nimewaomba radhi wazazi wa mtoto wanisamehe sitarudia tena na nasubiri kama watanisamehe ila sikutarajia kabisa,” alijitetea.

Upande wa jeshi la polisi umeonekana kuwa na kigugumizi kwani hakuna ufafanuzi wowote wa kina uliotolewa licha ya mzazi wa mtoto kuonyesha vielelezo vyote vya polisi na daktari kuhusiana na mtoto wake kutendewa vitendo vya ngono na mwalimu huyo.

Kamanda wa polisi mkoa Dodoma, David Misime, hakupatikana kulizungumzia tukio hilo lakini ofisa habari wa jeshi hilo, Kung’alo Lupy, alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa uchunguzi.
Share:

Sunday, 11 August 2013

Ronaldo : Kwake ni mwendo wa pesa, starehe na kubadili warembo

KWA sasa anaonekana zaidi kwenye fukwe na kumbi za starehe akiponda raha na mabinti warembo. Hana sababu inayomkwamisha kufanya hivyo, pesa anayo.

Alikitumia vizuri kipindi chake alichokuwa mchezaji, sasa acha atumie pesa yake. Huyu ni Ronaldo de Lima, straika wa zamani wa Brazil aliyetundika daruga Februari 14, 2011.

Soka limempa vitu vingi ikiwa pamoja na utajiri, staa huyo wa zamani wa Barcelona, anatajwa kuwa na pato linalofikia Dola 150 milioni.

Ronaldo aliyezaliwa Septemba 22, 1976 jina lake halisi ni Ronaldo Luis Nazario de Lima. Pesa anayoimiliki kwa sasa ameipata kupitia kazi yake ya kucheza soka. Alipokuwa akitumika uwanjani, aliifanya kazi hiyo kwa ubora mkubwa na kumpatia mikataba minono katika klabu alizopita na mikataba ya matangazo ya biashara.

Kwenye soka, kama kuna watu unaoweza kusema walizaliwa kwa ajili ya kazi hiyo, basi hutakosa kulitaja jina la Ronaldo. Mpira ulizoea miguu yake na ulifanya kile alichokitaka, alipokuwa akiuelekeza kwenda kwenye nyavu.

Kutengeneza pesa

Maisha ya Ronaldo kwenye soka yamedumu kwa miaka 18, akianzia kwenye klabu ya Cruzeiro mwaka 1993 na kuhitimisha soka lake Corinthians mwaka 2011.

Hapo katikati amepita katika klabu za PSV Eindhoven, FC Barcelona, Inter Milan, Real Madrid na AC Milan. Kucheza kwenye klabu hizo kumemfanya atengeneze pesa nyingi kutokana na mishahara yake minono huku akinasa mkataba mbalimbali ya udhamini, ikiwamo kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike. Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, Ronaldo katika enzi zake akiwa bado mchezaji, aliingiza pato kati ya Dola 200 milioni na Dola 250 milioni.

Kwa kuwa mara zote Ronaldo alipohama kutoka timu moja kwenda nyingine, ada yake ya uhamisho ilikuwa kubwa, jambo hilo lina maana hata mishahara yake haikuwa ya kima cha chini.

Alilipwa vizuri. Alipotoka Cruizero, inadaiwa uhamisho wake haukuwa chini ya Dola 5 milioni, kabla ya kuweka rekodi alipotoka PSV kwenda Barcelona ambapo miamba hiyo ya Catalan ililipa Pauni 17 milioni, ilikuwa mwaka 1996.

Mwaka mmoja baadaye, Inter Milan ikapanda dau na kumng’oa Nou Camp kwa Dola 19 milioni.

Baada ya kucheza mechi 99 na kufunga mabao 59 akiwa na jezi ya Nerazzurri, Real Madrid ikaja na Euro 46 milioni mwaka 2002 na kuinasa huduma ya mshambuliaji huyo kabla ya kumuuza AC Milan kwa Euro 8.5 milioni miaka mitano baadaye.


Share:

Neville ataka United isimuuze Rooney


MANCHESTER, ENGLAND

JAMANI acheni! Acheni kabisa. Ndivyo ambavyo beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, ameisihi klabu yake hiyo kuachana na mpango wa kumuuza Wayne Rooney hasa kwenda Chelsea.

Tayari Man United imezitupa chini ofa mbili za Chelsea za kutaka kumchukua Rooney, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 anataka kuandika maombi ya kuuzwa muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kutimiza azma yake ya kuhama Old Trafford.

Hata hivyo, Neville anaamini kwamba kocha David Moyes analazimika kumbakiza Rooney kwa sababu ndiye mchezaji muhimu zaidi katika harakati za kuipatia Man United taji la 21 la ubingwa wa Ligi Kuu England.

Neville anaamini kwamba kama Moyes atamuuza Rooney, basi atalazimika kumnunua mchezaji mwenye kiwango cha juu sana kwa ajili ya kupata mbadala.

“Rooney ni mchezaji muhimu sana. Ni bingwa na ni mtu ambaye anaweza kukupatia ubingwa.

Manchester United haipaswi kumuuza kwenda Chelsea, labda kama wakimnunua mchezaji kama Gareth Bale au Cristiano Ronaldo,” alisema Neville.

“Ukiwa na Rooney ujue una dhahabu, mtu ambaye amethibitisha uwezo wake kwa miaka sita, saba, hadi minane iliyopita. Mtu ambaye kila msimu anaonyesha mambo makubwa.

Ana mabao mengi na pasi nyingi za mabao kwa kila msimu. Hata katika msimu uliopita alikuwa hivyo hivyo ingawa hakuwa katika msimu mzuri.

“Atakupa kila unachotaka na hawezi kushusha kiwango chake katika mazoezi. Umuhimu wa Rooney ni mkubwa.

Ni mtu ambaye katikati ya Oktoba wakati uko pointi nne nyuma na inabidi uende kucheza na Chelsea kisha Arsenal, atakaa mbele ya viungo wake wawili na kufanya kila anachoweza, akipigwa viatu lakini huku akiandaa mabao na kufunga.

“Msiidharau thamani ya Rooney kwa mafanikio ya Manchester United katika kipindi cha miaka minane iliyopita na jinsi ambavyo anapendwa na wachezaji wenzake.


Share:

King Kapita aachia Kasema Poa




MSANII wa muziki wa kizazi kipya, King Kapita, ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kasema Poa’.

Kwa mujibu wa King Kapita, kazi hiyo imeandaliwa katika studio mbili kubwa nchini Nigeria na Tanzania, hivyo anaamini itawashika vilivyo mashabiki kutokana na ubora wake.

King Kapita alisema katika ngoma hiyo amewashirikisha pia Wanigeria, DJ maarufu aitwaye Kalito na DJ Ryder.

King Kapita katika moja ya mashairi ya ngona hiyo anasema: “Sasa tunaimba na kucheza wote, kamwambieni yule mtoto mzuri kasema poa, yanii she say yeahhhh...”

Ngoma nyingine zinazobamba za msanii huyo mmoja wa waasisi wa kundi la Wakacha, ingawa sasa anajitegemea ‘Solo artist’ ni pamoja na ‘Shikamoo Pesa’, ‘Kuna tatizo Kwani’ na sasa kaachia ‘Kasema Poa’.

Msanii huyo aliongeza kuwa, hivi sasa ngoma hiyo inapatikana mtandaoni na kuomba sapoti kutoka kwa wadau mbalimbali wa sanaa.

Share:

Serikali yamgeuka Ulimboka


SIKU chache baada ya Mahakama ya Kisutu kumwachia mtu aliyedaiwa kumteka na kumtesa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, serikali imemshukia daktari huyo na kudai ndiye chanzo cha kukwama kwa dola kukamata watu waliomteka.

Jana Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP), Eliazer Feleshi, alidai kuwa vyombo vya dola vimeshindwa hadi sasa kuwakamata waliohusika katika shambulio hilo kutokana na Dk. Ulimboka kukwepa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Feleshi ambaye jana aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alidai lawama zinazosukumwa kwa Jeshi la Polisi kwa madai ya kushindwa kuwakamata waliomtendea unyama daktari huyo hazina msingi, kwa kuwa mhusika mwenyewe hajafika polisi, licha ya kuitwa mara nyingi kutoa maelezo.

Alisema kama Dk. Ulimboka angetoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kungekuwa na mafanikio makubwa katika kuwasaka na hata kuwatia mbaroni waliohusika katika unyama huo.

“Kila mara mmekuwa mkilaumu polisi wanashindwa kukamata wahalifu lakini tutakamataje kama wenye ushahidi hawataki kutoa ushirikiano?

Kwa mfano mdogo tu ni ‘ishu’ (suala) ya Dk. Ulimboka, hadi leo hajatoa taarifa lakini polisi wanaendelea kusakamwa na kutukanwa tu,” alisema.

Hata hivyo, wakati Feleshi akitoa kauli hiyo, Dk. Ulimboka katika andiko lake alilolitoa mara tu baada ya kurejea nchini kutoka Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili ya matibabu, alimtaja mtu anayeaminika kuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ramadhani Ighondu, kuwa ndiye aliyemteka na kumtesa.

Ulimboka akimtumia Wakili Nyaronyo Kicheere alisema Ighondu na wenzake ni mhusika mkuu katika unyama aliofanyiwa, kauli ambayo imekanushwa mara kadhaa na serikali.

Mapema wiki hii, raia wa Kenya, Joshua Mulundi, aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka aliachiwa na Mahakama ya Kisutu baada ya DPP Feleshi kumfutia shitaka. Hata hivyo Mulundi alikamatwa tena na sasa amefunguliwa mashitaka ya kutoa maelezo ya uongo kwa polisi.

Wakati DPP akisema hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, jana aligoma kuzungumzia shinikizo la kumtaka ajiuzulu kutokana na kukithiri kwa matukio ya raia kumwagiwa tindikali, badala yake amewataka Watanzania kuwa na ushirikiano wa pamoja kukabiliana na uhalifu huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, (IGP) Mwema alishindwa kukubali kujiuzulu wadhifa huo na badala yake alitoa majibu ya jumla huku akiwataka Watanzania kubadilika na kuona suala la kulinda raia na mali zao ni jukumu la kila mmoja na si kazi ya polisi pekee.

Mkuu huyo alisema kuwa Watanzania lazima waelewe kuwa suala la ustawi wa jamii linatokana na uwepo wa amani na utulivu. “Nchi hii si ya mtu mmoja bali ni ya kila Mtanzania, inashangaza kuona asilimia 89 ya Watanzania wanaona suala la kulinda raia ni la polisi, si kweli ni lazima tubadilike,” alisema.

Alisema kuwa jukumu la utu lipo pale pale, hivyo kama taifa wana dhamana ya kuhakikisha suala la matumizi mabaya ya tindikali na dawa za kulevya linakomeshwa.

Mwema alisema kuwa wanalaani vitendo vibaya na vya kikatili vinavyofanywa na mtu mmoja mmoja ambavyo vinaleta hofu kwa jamii.

Alisema kuwa juhudi mbalimbali zinafanywa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa na hata kumalizwa kabisa. “Tumeamua kuja na mkakati wa pamoja kwa kuwa sasa matukio ya umwagiaji tindikali umeshamiri na hatuwezi kusubiri adhurike mtu mwingine, bali tusaidiane wote kwa pamoja kukomesha haya,” alisema.

Alisema kuwa lengo la kutengenezwa kemikali hiyo haikuwa kutumika vibaya au kumdhuru binadamu, bali ni muhimu kwa ajili ya vyombo vya usafiri na maabara.

“Hata kisu ukiangalia kimetengenezwa kwa ajili ya mambo ya msingi, lakini kikitumika vibaya kinaweza kudhuru watu,” alisema.

Huku akionyesha hatua zilizochukuliwa na jeshi hilo bila kutaja jina, alisema kuwa ofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege mmoja amesimamishwa kazi baada ya kudaiwa kuruhusu kupita kwa mabegi tisa ya dawa za kulevya yaliyokamatwa Afrika Kusini mwezi uliopita.

Mwema alisema kuwa ni muhimu wananchi wakatoa taarifa mapema pindi waonapo mwenendo mbaya wa matumizi ya tindikali hiyo, kwa kuwa ni uhalifu mpya.

“Wananchi ndio waathirika wa kwanza, ni vema wakatoa taarifa mapema ili hatua ziweze kuchukuliwa, maana vyombo vya dola pekee haviwezi kuhimili jambo hilo,” alisema.

Matukio ya kumwagiwa tindikali kwa sasa yameshamiri nchini kufuatia baadhi ya raia kupata ulemavu na wengine vifo, huku Julai 19, mwaka huu mmiliki na mfanyabiashara maarufu wa maduka ya Home Shopping Centre, Said Mohammed Saad, akivamiwa na kumwagiwa maji usoni yanayodhaniwa kuwa ni tindikali.

Ikiwa ni takriban wiki mbili tangu kutokea kwa tukio hilo, juzi wasichana wawili raia wa Uingereza waliofika visiwani Zanzibar kujitolea kufundisha somo la Kiingereza walimwagiwa tindikali majira ya saa 1:15 usiku, Mtaa wa Shangani eneo la mji Mkongwe.

Hata hivyo wasichana hao walisafirishwa jana kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mwaka 2007 Mkurugenzi wa Halihalisi Publishers, Said Kubenea, alimwagiwa tindikali, hatua inayomlazimu kwenda nchini India mara kwa mara kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Mwaka 2011 wakati wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Igunga, Musa Tesha, alimwagiwa tindikali, huku mkoani Arusha, wilayani Arumeru, Sheikh wa wilaya hiyo, Said Juma Makamba, alijeruhiwa kwa kumwagiwa usoni kimiminika kinachoaminika kuwa tindikali.

Wakati Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga, Novemba mwaka jana alimwagiwa tindikali.

Mkemia Mkuu wa Serikali

Katika kikao cha jana, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyere, alipiga marufuku usafirishaji wa tindikali bila kibali na kuagiza wahusika kutunza kumbukumbu kuonyesha ukali wa tindikali na kutoa mrejesho wa kiasi walichouza kuanzia mwezi huu.

Alisema kuwa wasafirishaji wanapaswa kuwa na vibali kisheria ambavyo vimetolewa na ofisi yake.

Profesa Manyere alisema kuwa wauzaji wa rejareja ni lazima wawe wamesajiliwa na wanapaswa kutoa taarifa za mauzo wanayofanya kila baada ya miezi mitatu kuanzia sasa.

Alisema kuwa kuanzia sasa wamiliki wa vyombo vya usafiri hawaruhusiwi kuchukua kemikali hiyo na kwenda nayo nyumbani badala yake wapeleke magari yao. “Wale wa lita moja moja hawaruhusiwi kuuziwa bali itapaswa kuuzwa kuanzia lita tano na kuendelea,” alisema.
Share:

Saturday, 10 August 2013

Download NEW TRACK | MABESTE ft PETER MSECHU - NISHAURI


Share:

Thursday, 8 August 2013

Jambazi sugu la ATM lanaswa Dar es Salaam


 Raia wa Bulgaria akiwa chini ya Ulinzi baada ya kupata kichapo kwa kudaiwa kuiba fedha kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) ya BOA tawi la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam jana.

Kama Benki tuliweka mtambo maalumu na mtuhumiwa huyo alionekana kwenye mtambo wetu, hivyo tuliwaagiza walinzi wetu watakapomwona mtu huyo wamkamate haraka sana,”alisema.

Dar es Salaam. Msako wa wezi wa kwenye Mashine za Kutolea Fedha (ATM), umeanza kuzaa matunda baada ya raia wa Bulgaria kukamatwa akiiba kwenye ATM ya Bank of Africa (BOA), Tawi la Afrikana, Kinondoni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za benki, mtuhumiwa huyo ambaye hakutajwa jina lake alikamatwa baada ya kamera maalumu zilizowekwa kwenye ATM za BOA, kumtambua kuwa ni mwizi sugu wa benki hiyo anayetafutwa.

Mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 12 asubuhi baada ya mtuhumiwa huyo kuwekewa mitambo maalumu ya kumnasa.
Alisema benki hiyo ilipelekewa malalamiko na baadhi ya wateja kwamba wakienda kutoa fedha kwenye ATM wanakuta akaunti zao hazina salio wakati wanaamini zilikuwa na fedha.

Chanzo hicho cha habari kilidai kuwa baada ya kupelekewa malalamiko hayo, waliweka mitambo maalumu ya kuwawezesha walinzi wa maeneo ya ATM za BOA kumbaini mtu atakayetoa fedha kwa njia ya wizi.

“Kama Benki tuliweka mtambo maalumu na mtuhumiwa huyo alionekana kwenye mtambo wetu, hivyo tuliwaagiza walinzi wetu watakapomwona mtu huyo wamkamate haraka sana,”alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo alianza mchezo huo kwa muda mrefu ambapo kwa kutumia kadi za ATM zisizojulikana idadi yake, alikuwa anakwenda kwenye ATM mbalimbali za benki hiyo na kutoa fedha hadi Sh10 milioni.

Kuhusu tukio la jana, mmoja wa walinzi wa BOA aliyejitambulisha kwa jina moja la Frenky alisema mtuhumiwa huyo alipofika kwenye ATM hiyo aliingia na kuchukua fedha ambazo alizipeleka kwenye gari lake. Frenky alisema baada ya kupeleka fedha hizo, alirudi kwa mara ya pili ili achukue fedha nyingine ndipo walinzi hao walimkamata na kumfunga pingu.

“Huyu mtuhumiwa mwenye asili ya Kiarabu alifika na gari lake saa 12 asubuhi, aliingia kwenye ATM na kutoa fedha ambazo hazikujulikana ni shilingi ngapi na kuzipeleka kwenye gari lake, baadaye alirejea tena kwa ajili ya kutoa fedha zingine, wakati anaingia ndipo alipokamatwa na mlinzi aliyekuwa analinda hapo,” alisema Frenky.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Camilius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea.

“Ni kweli taarifa nimezipata, mtuhumiwa amekamatwa, bado hatujajua ni kiasi gani ambacho ameiba kwa kutumia mtandao, tunaendelea na uchunguzi,” alisema Wambura.

Tukio kama hili lilishawahi kutokea mkoani Mwanza Februari 19 mwaka huu na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na maofisa ya Benki ya NMB liliwatia mbaroni watu watatu ambao walidaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti.

Share:

FEZA : Ana bendera tatu mkononi

feza kessy

MCHEZO wa kutoana na nani ataibuka mshindi umekuwa wa kikanda zaidi au ukaribu wa mipaka ya nchi, kuanzia jinsi washiriki wanavyopendekezana na hata Afrika inavyopiga kura katika shindano la Big Brother Africa (BBA).

Kwa wiki tatu mfululizo tumeshuhudia mshiriki wa Kenya akipata kura tatu kila wiki nazo ni za Tanzania, Uganda na Kenya yenyewe.

Washiriki wanaowakilisha nchi za Afrika Magharibi wamekuwa wakiwapendekeza washiriki wa Mashariki au Kusini mwa Afrika.

Mshiriki anayeiwakilisha Tanzania na pengine sasa Afrika Mashariki, Feza Kessy, kesho Jumapili ana mtihani mgumu wa kuiinua Afrika Mashariki kwani ili abaki anahitaji kura kutoka nchi zisizopungua tano.

Katika kikaango yupo na mshiriki kutoka Botswana, Oneal na Bimp kutoka Ethiopia. Kutokana na upigaji kura unaoangalia kanda, Feza angejihakikishia kura ya Ethiopia na ya nchi nyingine zisizo na washiriki.

Kura za uhakika ambazo anazo mkononi mpaka sasa ni ya Kenya, Uganda na Tanzania. Kura ya Ethiopia ameikosa kwa kuwa wanaye mshiriki wao katika kitanzi, Bimp.

Nchi kama Ghana ziliwahi kumpigia kura Feza, lakini mchezo umebadilika na kuna malumbano kati ya Elikem ambaye ni mwakilishi kutoka nchi hiyo.

Kura ya Botswana pia ataikosa kwa kuwa ‘shemeji’, Oneal kutoka nchi hiyo naye yupo kwenye kikaango akitegemea huruma za Afrika ili aweze kubakia katika mashindano hayo.


Washiriki wa Afrika Mashariki

Washiriki kutoka Kenya ni Huddah na Uganda ni Denzel, hao walikuwa wa kwanza kuyaaga mashindano hayo katika wiki ya kwanza.

LK4 kutoka Uganda naye alifuatia wiki moja baadaye na kuwaacha Annabel kutoka Kenya, Nando na Feza kutoka Tanzania wakiwakilisha.

Annabel kwa kutumia kura za nchi tatu yaani Kenya, Uganda na Tanzania, alipona katika kikaango mara nne mfululizo kabla ya kutolewa wiki iliyopita.

Share:

Zanzibar mwezi haukuonekana

Imetangazwa rasmi kwamba zanzibar mwezi haukuonekana hivyo kuwataka wananchi kuendelea na kukamilisha hesabu ya siku 30

Taarifa hiyo imetolewa na kamati ya mwezi kupitia zbc imesema sikukuu ya eid al fitri itakuwa siku ya ijumaa.

Kullu aam waantum bikhair

Share:

Young Killer kuipua ‘Mrs Super Star’




MSANII wa muziki wa hip hop nchini, Young Killer, anatarajia kuachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Mrs Super Star’ hivi karibuni.

Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Dear Gambe’, ambacho ameimba na Belle 9.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Young Killer alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, ambacho anaamini kitafanya vizuri kutokana na ubora wa mashairi yaliyomo ndani yake.

“Naamini kazi hii itafanya vizuri kutokana na mashairi ya wimbo huo, naomba wapenzi wa kazi zangu wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuipokea,” alisema.

Young Killer alisema kwa upande wa video ya ngoma hiyo, wataonekana baadhi ya wasanii ‘Mastaa’ wa kike ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya filamu.

Aliwataja wasanii watakaoonekana katika video ya kazi hiyo kuwa ni Elizabeth Michael ‘Lulu’, Irene Uwoya ‘Oprah’, Jacqueline Wolper, Wema Sepetu na mwanamitindo, Jokate Mwogelo.

Share:

Damu ya Ulimboka yaitesa Serikali

dr ulimboka


SIKU moja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kumfutia kesi raia wa Kenya, Joshua Mulundi, ya kuteka na kujaribu kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, Jeshi la Polisi limeanza sarakasi mpya za kutupiana mpira.

Wakati polisi wakikwepa kuwataja wahusika wa tukio hilo, wadau wamedai kuwa vyombo vya dola vinamkumbatia mmoja wa maofisa wa usalama aliyetajwa na Ulimboka kuhusika na utekaji huo.

Itakumbukwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliunda jopo la maaofisa kutoka kanda hiyo na makao makuu kuchunguza tukio hilo na kutamba kuwa halitatokea tena.

Licha ya tambo hizo, hadi sasa jopo hilo halijawahi kutoa hadharani ripoti ya kile walichokibaini hadi tukio jingine kama hilo likajirudia Machi 6, mwaka huu, alipotekwa na kuteswa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini, Absalom Kibanda.

Watuhumiwa wa tukio la Kibanda pia hawajakamatwa pamoja na Kova kuunda jopo la uchunguzi.

Alipotafutwa jana kuzungumzia uamuzi wa DPP kumwachia huru Mulundi kutokana na kutopatikana ushahidi wa kumtia hatiani kutenda kosa hilo, Kova aligoma katakata kutaja kile kilichobainiwa na jopo la kamati yake ya uchunguzi.

Badala yake Kamanda Kova alisema suala hilo lilikwisha kuondoka kwao na kwamba yeyote anayetaka kujua undani wake ni vema akajaribu kuwasiliana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba.

Kova alisema masuala yote hayo ikiwamo watuhumiwa kudaiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi hayako kwake.

“Kwanza uliwahi kunisikia hata siku moja nikimuita mtuhumiwa gaidi, sijawahi, mimi kazi yangu ni kukamata wahalifu mbalimbali wakiwamo wa magari kama haya niliyowaonyesha baada ya kuibwa na majambazi wanaotumia silaha,” alisema Kova.

Tanzania Daima lilimtafuta Kamishna Manumba ili kupata undani wa hatua inayofuata baada ya mtuhumiwa pekee kuachiwa, lakini ofisa huyo naye alikuwa na majibu ya kukwepa.

“Hivi baada ya kuachiwa kilitokea nini? Si umeona alikamatwa tena?” alihoji Manumba ingawa alipobanwa kuwa hakukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka, alisema sheria inasema kuwa mtu yeyote anaposema uongo, moja kwa moja atakuwa ametenda kosa.

Aidha, alipotakiwa kutolea maelezo mtindo uliozuka wa watu kubambikiziwa kesi za ugaidi, kamishna huyo hakutaka kusikiliza, zaidi ya kusema: “Kwa heri,” kisha kukata simu yake.

Wadau wahoji

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wadau hao walionyesha hofu kwamba kwa sasa kuna hatari ya wananchi kubambikizwa kesi za baadhi ya watu serikalini wanaofanya vitendo hivyo bila kuchukuliwa hatua zozote.

Mkurugenzi wa zamani wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Ananilea Nkya, alieleza kusikitishwa na kitendo cha polisi kutomtia hatiani ofisa wa Ikulu aliyetajwa kwa jina la Ramadhani Ighondu, kuwa ndiye aliyeratibu tukio hilo la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.

“Kesi ya Dk. Ulimboka mbona ipo wazi, mtuhumiwa yupo wazi, alitajwa na aliyeteswa, serikali ndiyo imemlinda. Kwa hali hii tunakuwa na hofu kuwa vyombo vyetu vya usalama vinatesa watu na kuwalinda watesaji,” alisema.

Aliongeza kuwa kwa sasa ni kama vile kuna vyombo vya ulinzi vya watu wachache. Kwamba, Tanzania sasa si salama, hakuna utawala bora, haki za binadamu hazizingatiwi wala hakuna demokrasia na uhuru wa mawazo.

Hili si jambo la kuchekea, ni suala la kulaaniwa na kuhuzunisha kwa kila Mtanzania. Ni aibu sana tunapokuwa na serikali inayotesa watu wake,” alisema.

Nkya aliongeza kuwa kwa hali hii Rais Jakaya Kikwete afafanue hadharani kwa Watanzania kuhusu tukio hilo, vinginevyo haeleweki vizuri.

Naye Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema uamuzi wa DPP kuwasilisha mahakamani hati ya kutoendelea na mashtaka hayo ni ishara ya wazi kuwa aliona hayana msingi.

Alisema kuwa mashtaka hayo yalifunguliwa kutumia kisingizio cha kesi kuwa mahakamani ili kudhibiti vyombo vya habari visiandike habari za uchunguzi kuhusu kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.

Mnyika pia alifafanua kuwa ilikuwa ni njia ya kuzuia Bunge lisijadili na kuihoji serikali. “Uamuzi huu wa DPP sasa umefungua mlango kwa vyombo vya habari kuandika na wabunge kujadili, kwani mmoja wa watuhumiwa ni ofisa wa Usalama wa Ikulu,” alisema.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa kwa uamuzi huo, Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda Kova wajitokeze waseme kuwa walilidanganya taifa kwa mwaka mzima, na kwamba sasa wawaeleze Watanzania nani hasa alimteka na kumtesa Dk. Ulimboka.

Share:

Mwakyembe acharuka

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameionya Kamati ya Nne ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri wa Anga nchini (NCASC) kujiondoa kabla hajaifikia iwapo mzigo wowote wa dawa za kulevya kutoka Tanzania utakamatwa nje ya nchi ukitoka nchini kwa njia ya anga.

Dk Mwakyembe alitoa onyo hilo jana Dar es Salaam wakati akizindua rasmi Kamati hiyo yenye wajumbe 11 na kusisitiza kuwa ina wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama katika viwanja vya ndege unaimarishwa, ili kudhibiti biashara ya dawa za kulevya nchini.

“Mimi sidhani suala la kukamatwa kwa dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ni dogo,” alisema Dk Mwakyembe na kusisitiza kuwa kashfa ya dawa za kulevya kupitishwa katika uwanja huo, inadhalilisha jina la Baba wa Taifa kitaifa na kimataifa.

Alisema kutowajibika kwa mamlaka zinazohusika na ulinzi na usalama katika viwanja vya ndege, kumesababisha kuendelea kwa ugaidi wa kimataifa na kusikitishwa na udhaifu unaofanywa na mamlaka hizo hali inayoliletea Taifa fedheha kubwa.

“Sidhani kama mamlaka hizo zinahitaji sheria ili ziwe na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu,” alisema Waziri na kusisitiza kuwa umefika wakati kwa viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili kuleta tija na maendeleo nchini.

Alisema amekuwa akisikia mijadala kuhusu kukamatwa kwa dawa za kulevya, lakini hakuna anayechukuliwa hatua za kisheria kuhusu kashfa hiyo na kuongeza kuwa viongozi wanakataa kuheshimu sheria, hali ambayo alisema inadhalilisha na kushusha hadhi ya viwanja vya ndege nchini.

Baada ya kuzindua Kamati hiyo, Dk Mwakyembe alizuia zawadi zilizoandaliwa kutolewa kwa Kamati inayomaliza muda wake ikiongozwa na Mwenyekiti, Jafari Mpili na kukataa pia kupiga nayo picha ya pamoja badala yake akaomba akutane na Kamati mpya, jana saa nane mchana kujadili kwa kina majukumu.

Awali, katika hutoba yake kwa mgeni rasmi, Mwenyekiti wa NCASC ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Fadhili Manongi, alitaja changamoto kadhaa za kiusalama katika sekta ya anga nchini.

Changamoto hizo ni pamoja na kuchelewa kuridhiwa na Bunge mikataba ya kimataifa inayohusu na usalama wa usafiri wa anga kama vile mkataba wa Beijing na Itifaki ya Mwaka 2010.

Nyingine ni kutojua taratibu za kiusalama na maneno ya kukatisha tamaa kwa maofisa usalama wa viwanja hasa kutoka kwa viongozi waandamizi wa Serikali kwa kauli zao na kutoelewa kanuni za usalama kwa wadau wengi.

Moja ya malengo ya NCASC ni kushauri TCAA hatua za usalama zinazotakiwa katika viwanja vya ndege ili kudhibiti vitisho na ugaidi dhidi ya usafiri wa anga, viwanja na miundombinu yake.

Doa kwa Taifa Juzi katika taraifa yake, Serikali ilisema biashara ya kusafirisha dawa za kulevya imeanza kutia doa taswira ya Watanzania kimataifa. Ilisema uthibitisho ni kwamba katika baadhi ya nchi, kila Mtanzania anayeingia, hivi sasa anachukuliwa kama mshukiwa wa moja kwa moja wa dawa hizo na hivyo kupekuliwa kwa kina.

Serikali ilisema Watanzania waliokamatwa hivi karibuni wakiwa na dawa hizo wamechangia kwa kiwango kikubwa kutoa doa taswira ya nchi. Wiki iliyopita, Mtanzania Jackline Mollel (35), alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare, Zimbabwe akidaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 72.

Kabla ya tukio hilo, Julai, Watanzania wawili, Agnes Gerald ‘Masogange’ (25) na Melisa Edward (24), walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo, jijini Johannesburg, Afrika Kusini, wakidaiwa kuingiza dawa za kulevya kutoka Tanzania zikiwa na thamani ya mamilioni ya fedha. Walifikishwa mahakamani jijini humo.

Share:

Moto mkubwa wateketeza uwanja wa JKIA

Safari za ndege za ndani ya nchi nchini Kenya zinatarajiwa kurejea kama kawaida baadaye leo baada ya moto mkubwa kuteketeza sehemu ya uwanja rasmi wa kimataifa wa ndege nchini humo JKIA.
Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ukiteketea

Msemaji wa ikulu ya rais, Manoah Esipisu alisema kuwa ndege za mizigo zitaanza kusafiri lakini akaongeza kuwa serikali haiwezi kusema bayana ni lini safari za kimataifa za ndege zitarejea kama kwaida.


"Tunatarajia kuwa safari za ndege ndani ya nchi zitaweza kurejea kama kawaida baadaye leo, '' alisema Esipisu.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta awali leo ulikua umefungwa baada ya moto mkubwa kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi. Moto huo hata hivyo ulidhibitiwa

Hakuna ripoti zozote za majeruhi .

Mwandishi wa BBC katika uwanja huo amesema kuwa kulikuwa na moshi mkubwa uliotoka katika eneo la kuondokea na kuingilia wageni.

Baadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo pia ziliahirishwa wakati zengine zikielekezwa kwenda Mjini Mombasa.

Mwishoni mwa wiki jana baadhi ya wenye maduka ya Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada ya serikali kusema kuwa leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na muda.

Huu ni moto mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika uwanja wa Jomo Kenyatta wenye kutumiwa na wasafiri wengi zaidi katika eneo la Afrika mashariki na kati

Uwanja wa ndege wa JKIA ulivyoteketea

Safari za mamia ya wasafiri zimevurugwa na kuachwa nje ya uwanja huo wenye shughuli nyingi zaidi Afrika mashariki
Taarifa za awali zilionyesha kuwa moto huo ulianzia kwenye eneo la uhamiaji katika kitengo cha kupokea wageni kabla ya kusambaa hadi maeneo ya ushuru na mizigo ya abiria.

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana , lakini maafisa wa ngazi ya juu wa serikali wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta walitembelea uwanja huo na kutoa wito uchunguzi ufanyike mara moja. Hata hivyo hawakutoa ishara yoyote ni lini uwanja huo utafunguliwa tena .

Shirika la ndege la kenya -Kenya Airways, ambalo ni kubwa zaidi katika kanda ya Afrika limefuta safari zake zote na kuelekeza ndege zinazoingia nchini katika mji wa Mombasa . Tayari hisa za ndege zimeshuka kwa kiwango cha asilimia 2 . Ndege za kimataifa ambazo zilitakiwa kuondoka leo asubuhi ziliruhusiwa kuondoka bila wasafiri.

Share:

MFANYABIASHARA BILIONEA MOSHI AUWAWA KWA RISASI ISHIRINI

Moshi. Mfanyabiashara tajiri wa Mirerani na Jijini Arusha, Erasto Msuya, ameuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 kwa kutumia bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), jana mchana.

Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri,

aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

“Eneo la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 ya risasi zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa kweli ameuawa kinyama sana,” alisema polisi mmoja wa Kituo cha Bomang’ombe.

Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea kati ya neo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na mji wa Bomang’ombe, mji huo ulifurika magari ya wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na Mererani.

Habari za uhakika zilieleza kuwa wauaji wake walikuwa katika pikipiki na baada ya kumminia risasi hizo, walimpora kibegi ambacho haikujulikana kama kilikuwa na madini ama mamilioni ya fedha.

Kulingana na vyanzo vya habari, mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na kukubaliana kukutana katikati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya Barabara ya Kia katika Barabara Kuu ya Hai kwenda Arusha.

RPC Kilimanjaro afafanua alivyouawa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa saa 7:00 mchana eneo la Mjohoroni kati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya barabara ya Kia.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Eransto alikuwa akitokea Moshi kuelekea Arusha, na alipofika hilo eneo la Mjohoroni alichepuka na kwenda meta 300 nje ya barabara,” alisema.

Kamanda Boaz alisema alipofika eneo hilo, alikutana na vijana wawili waliokuwa na pikipiki ambao waliingia ndani ya gari kwa lengo la kufanya mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.

Hata hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye gari lake na kuanza kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka kwenye gari la Erasto na kuanza kumminia risasi nyingi.

Kijana wa Kimasai alivyoshuhudia mauaji

Kijana pekee wa kabila la kimasai anayedaiwa kushuhudia mauaji hayo, aliwaeleza polisi kuwa mara baada ya Erasto kufika eneo hilo la mtaa wa Wasomali, alisimamisha gari na kuwapigia wauaji.

Habari hizo zimedai kuwa vijana wale wawili walipokea simu hiyo na kumtaka ashuke kwenye gari lake la kifahari aina ya Range Rover New Model, ili wafanye biashara ambayo haijui.

Inadaiwa kuwa Erasto alipojaribu kupeleka mkono ili achomoe bastola, mmoja wa wale vijana alianza kumshambulia kwa risasi nyingi ambazo zilimfanya afariki dunia papo hapo.

Kijana huyo wa kimasai anayedaiwa kuwa msaada mkubwa kwa polisi, alidai kuwa baada ya Erasto kudondoka chini, vijana hao walichukua begi alilokuwa nalo na kutokomea.

Pikipiki iliyotumika yapatikana



Taarifa zilizopatikana baadaye jana jioni zilisema pikipiki iliyotumika katika tukio hilo imepatikana katika kijiji cha Olkolili, huko Sanyajuu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Kamanda Boaz alithibitisha kupatikana kwa pikipiki hiyo yenye nambari za usajili T316 CLV ikiwa imetelekezwa baada ya gurudumu moja kupata pancha baada ya kufika katika eneo hilo.

“Kwa vile tulikuwa tumesambaza taarifa kila mahali kwamba kuna raia wema walituarifu kuwa kuna watu wametelekeza pikipiki, baada ya kupata pancha na walikuwa wakitembea kwa miguu,” alisema.

Alisema Polisi walikwenda katika eneo hilo na mashuhuda walioshuhudia tukio hilo la mauaji wameitambua pikipiki hiyo kuwa ndiyo iliyokuwa ikitumiwa na wauaji wa mfanyabiashara huyo.

Kamanda Boaz alisema pia kuwa polisi watachunguza kwa kina mawasiliano ya simu ya mfanyabiashara huyo, kwa lengo la kutafuta watu wa mwisho kuwasiliana na marehemu.

Share:

MUME WA PILI WA WASTARA AIBUKA ADAI WASTARA NI MKE WAKE

Na Issa Mnally
MIEZI nane baada ya kufariki dunia mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’, hatimaye mume wa pili wa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Ahmed Kushi ameibuka na kudai kwamba anatambua kwamba staa huyo bado ni mkewe na anataka ampatie mwanaye aliyezaa naye.
Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kuwa Wastara aliachana na mwanaume huyo kwa talaka kabla ya kuolewa na Sajuki lakini kuibuka kwake na madai kuwa bado mwanadada huyo ni mkewe kumezua mshangao mkubwa.



MADAI YA KUSHI
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Kushi alifunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye na Wastara walifunga ndoa ya Kiislamu mwaka 2000 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Fares.
Alisema: “Kisheria bado ni mke wangu kwa kuwa nilikuwa nimempa talaka moja tu wala hazikufika tatu,” alisema Kushi na kudai kwamba ndoa yake na staa huyo ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu na kuvunjika kutokana na kutawaliwa na migororo.
Jamaa huyo alidai kuwa zaidi ya mara tatu amekuwa akimtaka Wastara ampatie mwanaye huyo ambaye kwa sasa ametimiza miaka minane bila ya mafanikio.

KWA NINI WAKATI HUU?
Gazeti hili liliamua kumbana kwa kumuuliza kwa nini ameibuka wakati huu baada ya Sajuki kufa na mbona hakujitokeza kwa zaidi ya kipindi cha miaka kumi iliyopita? Pia akaulizwa kwa nini ameamua kutafuta umaarufu kwa kumdhalilisha? Akaishia kukaa kimya.

WASTARA AFUNGUKA
Baada ya Kushi kuibuka na ishu hiyo yenye utata, gazeti hili lilizungumza na Wastara ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Kuhusu mtoto, kama kweli alikuwa na lengo la kumchukua mwanaye na ananijua, basi atakuwa anawajua wazazi wangu hivyo angefuata utaratibu.
“Hakuna utaratibu kama huo kama kweli anamhitaji mwanaye angeenda kwa wazazi wangu, huko ni kunidhalilisha kwa kuwa ananiona mnyonge baada ya kufiwa na mume wangu Sajuki.
“Kama siyo kunidhalilisha ni nini? Naomba asitumie jina langu kutafuta umaarufu kwa kunichafua. Naomba aache kwa sababu ananiongezea maumivu juu ya maumivu.”
Kuhusu madai kwamba bado ni mkewe, Wastara alilia: “Hivi huyo mtu alikuwa wapi muda wote nikiwa na Sajuki? Mbona hakuibuka wakati mume wangu akiwa hai? Najua anatumia kigezo cha kuondoka Sajuki kunionea lakini Mungu anajua.”

NI KWELI ALIFUNGA NDOA NA KUSHI?
Pamoja na kumbembeleza aeleze kama kweli aliwahi kufunga ndoa na Kushi, Wastara alisema: “Sitaki kumzungumzia mtu, naomba watu wawe na huruma kwangu, wasitumie kigezo cha kumpoteza Sajuki kunidhalilisha.”

SHEHE AMPINGA KUSHI
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimtafuta shehe wa Msikiti wa Nuur wa Magomeni-Mapipa jijini Dar, Juma Simba ili kupata ufafanuzi juu ya talaka moja ambapo alimpinga Kushi kwa kusema kuwa kisheria Wastara si mkewe tena.
“Kumpa talaka moja si sababu ya kuendelea kuwa mke wake mpaka leo hii, sheria inasema kuwa Kushi alitakiwa kumrejea Wastara kabla ya miezi mitatu kupita tangu alipompa talaka moja,” alisema na kusisitiza kuwa ndoa hiyo ilishakufa.

YATOKANAYO
Awali ilidaiwa kuwa Wastara aliwahi kuolewa mara mbili kabla ya kufunga ndoa na staa mwenzake wa filamu, Sajuki.
Ndoa ya kwanza ya Wastara aliifunga mwaka 1998 na Juma Mpemba ambaye alibahatika kupata naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Samir.
Sajuki alikuwa mume wa tatu kwa Wastara ambaye naye alibahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Farheen.

Share:

Tuesday, 30 July 2013

FEZA AONGOZA KUCHUKIWA NA WENZAKE NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER



Habari mbaya kwa Tanzania, Feza Kessy ni miongoni mwa washiriki watatu waliopigiwa kura zaidi kutoka wiki hii...FEZA amepata kura nyingi zaidi hii inaonyesha kuwa ndio mshiriki anayechukiwa zaidi ndani ya jumba hilo...
Feza ameungana na mpenzi wake Oneal na Elikem kwenye kikaango hicho cha eviction. Wa kwanza kumtaja Feza kwa kudai kuwa ni mbeya na jinsi anavyopenda kuwakusanya washiriki wenzake na kuwashawishi mi Msouth, Angelo.

Beverly wa Nigeria pia amemtaja Feza kwa madai kuwa ana upinzani mkali kwenye shindano hilo.

Elikem amewataja Oneal na Feza huku Cleo wa Zambia akimtaja Feza kwa madai kuwa ni tishio kubwa kwake na kusema wazi kuwa hatak

Share:

Saturday, 27 July 2013

STARS WAKIWA MAZOEZI KUPAMBANA NA CRANE LEO

Wachezaji mbalimbali wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Satrs' ambao wanasakata kabumbu ndani ya nchi wakijifua katika Uwanja wa Taifa wa Mandela uliopo Nambole nchini Uganda. Stars ipo nchini Uganda na kesho inataraji kushuka katika dimba la uwanja huo kumenyana vikalina The Crenes ya Uganda kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani
CHAN.

Moja ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya kesho (Julai 27 mwaka huu) dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.

Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive