Wakazi wa nyumba zaidi ya mia moja na hamsini zilizokamilika na zilizo katika ujenzi kwenye eneo la vikongoro -CHANIKA wamejikuta wakipoteza makazi yao baada ya nyumba hizo kuvunjwa na serikali wilaya ya ilala kwa kudaiwa kuwa ni wavamizi.
Ni sehemu ya wakazi wa eneo hilo la vikongoro wakipaza sauti zao mara baada ya ITV kufika eneo la tukio kushuhudia kilichotendeka ambapo wakazi hao wamesema wamevunjiwa nyumba zao pamoja na zile walizokuwa wakiendelea kujenga ilhali wanamiliki maeneo hayo kihalali.
Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo EFESO MSEMO amesema vijana waliohusika na kufanya uvunjaji huo walikuwa wakichukua vitu walivyokuwa wakikuta ndani ya nyumba hizo sambamba na kunywa vinywaji walivyokuwa wakikuta katika maduka wanayoyavunja.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ameiambia ITV kwa njia ya simu kuwa alipewa taarifa na kamanda wa polisi wa wilaya ya kipolisi ya ukonga kuwa uvunjaji huo unatokana na wakazi hao kuvamia katika eneo ambalo linamilikiwa kihalali na mtu mwingine.
COMMENTS










