Wednesday, 12 June 2013

FAMILIA YAMKATAA MTOTO WA NGWEA....!!!

SIKU chache baada ya aliyekuwa mkali wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ kupumzishwa kaburini kufuatia kifo cha usingizini nchini Afrika Kusini kilichotokea Mei 28, mwaka huu, mambo kibao yanazidi kuibuka.

Mtoto wa Ngwea akiwa na baadhi ya wanafamilia wakati wa mazishi ya baba yake.
Habari zinadai kuwa familia ya marehemu Ngwea imemkataa mtoto aliyeletwa na mama yake makaburini akidaiwa kuwa ni mtoto wa Ngwea. Juni 6, mwaka huu wakati wa mazishi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alitimba akiwa na mtoto huyo wa kike aitwaye Neema Albert na kudai kuwa alimzaa na Ngwea mwaka 2001, wakati msanii huyo akisoma Sekondari ya Mazengo. Wakati akijieleza, ndugu wa Ngwea, Anthony Mangweha alikuwa akimsikiliza ambapo aliwataja wanandugu wa marehemu waliokuwa wakijua suala hilo. Waliotajwa kujua kuwa mtoto huyo alikuwa wa Ngwea ni Frank, Jotam na Amani ambao waliwahi kutumwa na marehemu kwenda kumwangalia mkoani Dodoma. Hata hivyo, ndugu huyo aliyekuwa akimsikiliza alimtaka mama Neema kupoa, hadi familia ikae kikao.
Mama Mangwea.
“Kweli wikiendi iliyopita familia ilikaa kikao kwa zaidi ya saa 7, pamoja na mambo mengine lakini wanadaiwa kufikia uamuzi mzito wa kumkataa mtoto huyo hadi mama Neema apeleke vigezo vya uthibitisho,” kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.
Akizungumzia suala hilo kwa sharti la kutotajwa , mmoja wa dada zake Ngwea alisema: “Ni kweli yule mtoto aliondoka na mama yake lakini kama akileta uthibitisho tutampokea.”

Share:

DOGO JANJA AKAMATWA NA BANGI..........


 Jana jioni msanii wa kizazi kipya abdul aziz Chende "Dogo janja" kukamatwa na bangi na Askari polisi na kufikishwa kituo cha polisi Ngarenaro hapa jijini ,katika kujitetea kituoni hapo alidai kuwa alikuja kushow love na rafiki zake wa hapaTown baada ya kunyakua tuzo kili music award weekend iliyopita, nje ya tukio tulikutana na Msanii BAM wa jambo squad wanaotamba na ngoma zao kibao zilizowafanya kunyakuwa tuzo ya kili music award na kusema kuwa,baada ya dogo janja kusafiria nyota yao kwa muda mrefu sasa hayo ni sehem tu ya makofi ya Mwenyezimungu na atarajie kukutana na balaa mtindo mmoja endapo tu atashindwa kuwa na heshima kwa wakubwa zake na waliomjenga kisanii mpaka hapo alipofikia kabla hajaiba idea na mashairi ya jambo squard ambapo dogo alishine na kutoka kimtindo.

tunampa pole dogo janja na kumpa ushauri kuwa ikiwa ana njozi za kuwa msanii mkubwa nchini na kimataifa ajijenge kitabia na kuepuka makundi yanayoweza kumpoteza na kumuingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.


Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive