Wednesday, 14 October 2015

sitaki kuwachanganya mqshabiki:Rose

Gladness Mallya
MWANADADA staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema hataki kujihusisha na harakati za siasa kwa sasa kwa vile anaogopa kuwachanganya mashabiki wake.
Mwanadada staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akipiga stori na gazeti hili, Rose alisema kwa kuwa yeye ni kioo cha jamii anayeelimisha kupitia kazi yake, alisema kujiweka wazi upande ulipo ni kuwagawa watu wake kitu ambacho asingependa kitokee.
“Wasanii wanaozunguka kwenye kampeni hawafanyi vibaya, lakini mimi siwezi na sikutaka kufanya hivyo ila kura nitapiga na kuhusu ni nani nitakayemchagua kuwa rais ni siri yangu,” alisema nyota huyo ambaye anakiri kuwa soko lao limeyumba.
Share:

hatimaye mr chuzi aaga rasmi movie

Mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’.
Gladness Mallya
MKONGWE kwenye gemu la filamu Bongo, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ ameamua kuachana na filamu kwa kile alichodai kwamba hazilipi.
Akichonga na paparazi wetu, Mr. Chuz alisema soko la filamu limeshuka na wasambazaji wanasuasua, jambo linalofanya maisha ya wasanii kuwa magumu, hivyo ameamua kuachana nayo na kujikita katika kutengeneza tamthiliya ambazo zinarushwa na Runinga ya Africa Magic.
“Nimeachana na filamu maana hazinilipi, soko lenyewe halieleweki, nimeamua kutengeneza tamthiliya ambapo naona kiukweli zinanilipa sana, nakuwa bize muda wote,” alisema Mr. Chuz.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive