Monday, 22 July 2013

LOWASSA, DK. SLAA, MEMBE WAWEKWA NJIA PANDA KUWANIA URAIS.....!!!


Dk. Wilbrod Slaa


*Rasimu kutumika kuwaondolea sifa ya kugombea urais
*Yumo pia Membe, Magufuli, Sitta, Zitto na Wassira


Freeman Mbowe
MKAKATI wa kuwaengua vigogo wanaotajwa kung’ang’ania kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 sasa umebainika, MTANZANIA Jumapili linaripoti.

 Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili,    mkakati huo ambao umelenga kuwang’oa viongozi hao,  unadaiwa kutekelezwa na baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Rasimu ya Katiba Mpya, iliyotolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Dk. Emmanuel Nchimbi


Steven Wassira
Imeelezwa kuwa kupitia Rasimu hiyo ya Katiba Mpya, kuna vipengele vilivyopenyezwa kwa nia ya kuwabana watu fulani fulani ndani na nje ya CCM ambao wanatajwa kuusaka ukuu wa dola mwaka 2015 na chama hicho hakitaki kuona wanakuwa kikwazo dhidi yake.

Mtoa habari wetu ndani ya CCM alilidokeza gazeti hili kuwa vipengele hivyo ambavyo vimewekwa kama mtego, ni vile vinavyotaja sifa za mgombea Urais na mgombea Ubunge.


January Makamba


Bernard Membe
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, kutokana na hilo, baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM kwa makusudi wameamua kuufanya mjadala kuhusu serikali tatu kuwa mkali, ili kuzuia mjadala mpana katika masuala mengine.

Kipengele ambacho kama kikiachwa bila kufanyiwa marekebisho kinaweza kuwabana wanasiasa wengi ndani na nje ya CCM wanaotajwa kuwania Urais 2015 ni pamoja na kile cha Sura ya Saba, ambacho kinazungumzia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu Serikali, Rais na Makamu wa Rais, katika sehemu ya kwanza C kwenye kipengele cha 75 (E) kinachozungumzia sifa za Rais kimeeleza kuwa mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa: anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hiyo.




Wakati ikiwa hivyo katika sifa za kuwania nafasi ya Rais, kwenye Rasimu hiyohiyo kipengele cha sifa za kuwania nafasi ya Ubunge kilichopo katika sura ya tisa, sehemu ya pili (A) inayozungumzia kuhusu uchaguzi wa wabunge, katika kipengele cha (2a) kimeeleza kuwa mtu hatakuwa na sifa za kugombea/ kuchaguliwa kuwa Mbunge ikiwa mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka mitano.

Kutokana na hilo, ni wazi kuwa viongozi au vigogo waliowahi kuwa wabunge kwa vipindi zaidi ya vitatu vya miaka mitano hawatakuwa na sifa za kugombea Urais kwa sababu tayari kipengele cha sifa za kuwania Urais kimetaja kuzingatia sifa za mgombea ubunge.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa vigogo karibu wote ndani na nje ya CCM wanaotajwa kutaka kuwania nafasi ya Urais watakuwa wamepoteza sifa za kuwania nafasi hiyo endapo kipengele hicho kitaachwa bila kufanyiwa mabadiliko.Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.

Vigogo hao wanaotajwa kutoka CCM ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, 
...jambotz8.blogspot.com.... Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, wakati kutoka Chadema ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbroad Slaa na Zitto Kabwe.
MTANZANIA JUMAPILI
Share:

RAIS KIKWETE AWAONGOZA WANANCHI KUAGA NA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MIILI YA ASKARI 7 WALIOFARIKI HUKO DARFUR,SUDANI

 Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Rais na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnard Mengi, akiwa na baadhi ya viongozi, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Majeneza yenye miili ya Askari wa kulinda Amani, wa jeshi la Ulinzi la Tanzania, waliokufa huko Darfur Julai 13, 2013, wakati wa zoezi la kuagwa miili hiyo lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi, Upanga jijini Dar.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Bilal, na viongozi wengine wakiwa katika shughuli hiyo ya kuagwa miili ya askari hao leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga Dar es Salaam. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakati wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. Kulia ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Majeneza yenye miili yakiwa eneo la tukio tayari kuagwa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa zoezi hilo.
 Mkuu wa Majeshi,Jenerali Davis Mwamunyange, akizungumza wakati wa zoezi hilo.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.
 Baadhi ya Askari pia wakiwa na nyuso za huzuni.PICHA NA OMR.
Share:

ALIYEIBA MUME WA MTU MBAGALA NAYE AIBIWA MUME HUYO HUYO NA AJUZA


Waswahili wanasema Ukstaajabu ya Musa utaona ya FIlauni!ni kwelii ndugu zangu!yametokea na muda huu ninaoandika ndivyo ilivyo!!
Hali ilikuwa ivi mdada cheupe dawa toka kanda ya juu,alinogewa na penzi la baba mwenye familia yake huko pande za MBAGALA KIASI CHA KUMFANYA Baba huyo kuisahauu kabisa familia yake ya mke na watoto wawili nae kwa kujiona mjanjaa sana akamdhibiti na maisha yakaendelea,huku nyuma mama wa watu akiwa ameachwa na watoto wawili na mimba juu siku ilipofika ya kujifungua hakupata msaada wowote ule na hata alipokuwa anapiga simu kuitaji mssda toka kwa mzazi mwenziwe alijibiwa kwamba hana pesa na ajitahidi tu mwenyewe aende hospitali,majirani mwenye utu na mioyo yahuruma wakajichanga na kumkimbiza hospitalini mama yule!lakini riziki haikuwa upande wake Mungu akampenda zaidi akiwa na mtoto tumboni kwa maana kwamba alicheleweshwa! Baba akapwa taarifa,kwa aibu akaenda nyumbani kwa jili ya mazishi lakini ndugu majirani walimwacha azike mwenyewe!!!
Baada ya mkasa huo akarudi kule alikokuwa amempangisha Cheupe dawa wake ili kuendelea na maisha,maisha yakaenda akamzalia wana wawili na baada ya muda Baba sasa yupo kwa penzi Zito na jimama lenye pesa zake.

kahama kwake na mazimaa yupo kwa huyo jimama na jimama alivyo na jeuri ya pesa anampa kila kitu Baba huyo asiye na soni wala haya na kinachomfanya huyo dada aliye ni ile hali ya jimama hilo kumwita msamba na kwamba kama yeye mwanzo alimwiba basi atulie sasa ni zamu yake na hata inapotokea BABA huyo yupo kwake humpigia simu cheupe dawa na kusema nipo na mumeo sasa we ulie tuuu!....Cheupe dawa hana kazi alikuwa akimtegemea kila kitu BABA maana kwa mujibu wake mama huyo keshampachika jina baba huyo kwamba ni BONGE LA BWANA!
uNAAMBIWA HALI NI tata cheupe dawa aanatelekezwa na wanawe wawili na mmoja aliyekutwa naye jumla watatu na yule Bonge la bwana keshatangaza kumuowowa BONGE LA MAMA ..huku nyuma cheupe dawa anatembea na kisu popte aaatakapowakuta ama zake ama zao!!!jamani chondechonde mwenye no ya Gea HABIBU atoe ili anusuru uhai hii jamani si uongoooooooooooo!! ni true story hata anavyotusimulia mwenyewe ni kama vile kasahau yeye alivyomtenda mwenzake!''
Je wanawake hii mnaionaje?toeni maoni ushauri gani apate ili asije ozea jela mana kinachomuuma zaidi ni huyo BONGE
LA BWANA KUHEHUKA NA PENZI LA HUYO MAMA NA KUMWELEZEA KILA KITU KINACHOFANYIKA PINDI WANAPOKUWA CHUMBANI..SASA KISASI CHA HUYU dada kipo kwa huyoooo BONGE LA MAMA!
Share:

KWANINI KUNA KIGUGUMIZI MAPAMBANO ZIDI YA DAWA ZA KULEVYA TANZANIA?


Biashara ya dawa za kulevya inaonekana kushamiri nchini, huku kukiwa na maswali mengi juu ya akina nani hasa wahusika wa shughuli hii, hata inashindwa kukomeshwa.
Waliopewa mamlaka kuzuia dawa hizo nao wanahusika au hawana ujuzi, wafukuzwe?
Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wa makala hii, wana mashaka kwamba huenda baadhi ya vigogo au wafanyakazi waliopewa mamlaka kupambana na dawa nchini, wanahusika kufanya biashara hii au kuwasaidia wanaoifanya kwa manufaa yao, madai ambayo wamekuwa wakiyakanusha vikali.
Hata hivyo baadhi ya watu ambao wamewahi kuwa majambazi na kujihusisha na biashara haramu, akiwamo mchungaji mmoja kutoka Arusha ambaye amewahi kuwa jambazi kabla ya kuamua kuokoka na kumtumikia Mungu, anasema ni vigumu mno na huenda ni jambo lisilowezekana kufanikiwa kufanya mambo mabaya nchini kama ya ujambazi au dawa za kulevya na ukadumu katika kazi hiyo kama hauna mtandao na wale ambao wanahusika katika kuzuia vitendo hivyo.
“Kama una mawasiliano na wenye mamlaka utafanya biashara yoyote chafu, kama huna ni ngumu kutokamatwa, mimi nimewahi kuwa jambazi, ninaongea haya kwa uzoefu, sio kweli kwamba ulinzi nchini ni mbaya, bali kuna watumishi si waaminifu” anasema Mchungaji huyo.
Kwa uzoefu wake ni kuwa iko haja kwa viongozi walioko Serikalini kama kweli wana lengo la kupambana na dawa za kulevya, kwanza kuwachukulia hatua wote ambao waliwakagua na kuwaruhusu wahusika wa dawa wanaokamatwa kupita.
Ni kama hakuna lengo la kupambana na dawa za kulevya
“Kama mtu amepita uwanja wa ndege, inapaswa kujulikana alikaguliwa na nani? Wote waliohusika wakamatwe mara moja, waunganishwe kwenye kesi ya hizo dawa za kulevya, hii itaonyesha kweli Tanzania tuna lengo la kupambana na dawa za kulevya, lakini kinachofanyika sasa ni usanii wa mchana kweupe,” anasema Mchungaji huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
Hatua kali kwa wauza dawa
Baadhi ya wananchi akiwamo Ameria Haule, mkazi wa Ubungo anashauri kutungwe sheria kali za kupambana na dawa za kulevya.
Aidha, Juma Hamisi wa Mtongaji, na Tuma Msongwa wa Manzese, Dar es Salaam wanasema pale ambapo mtu amekamatwa na aina yoyote ile ya dawa za kulevya, na kukawa na uthibitisho, kusiwe na haja ya kufanya upelelezi juu yake zaidi, badala yake hukumu itolewe mara moja. Hali kadhalika wakashauri dhamana iondolewe, wakisemabiashara hii ni sawa na mauaji.

Kituo cha daladala kwa Manyanya

Mojawapo ya vituo vya daladala ambavyo vinadaiwa kutumiwa kwa dawa za kulevya ni cha daladala cha Kinondoni kwa Manyanya,  kama unaelekea Posta ukitokea Kinondoni.
“Ni kawaida kuwaona vijana wakisinzia hapa kuanzia asubuhi hadi asubuhi, kama kweli wenye mamlaka wana lengo la kupambana na dawa, wangekuja hapa ikawasomba hawa wote wanaosinzia, kisha ikawapime ili kuona walicholewa kimetokana na nini…kuna madai kuwa hao ndio wauzaji wazuri wa rejareja hapa Kinondoni, hali kama hiyo iko pia vituo vingine vingi vya daladala, huenda ndio sababu kwanini inakuwa vigumu kupiga marufuku wapiga debe kuwepo, maana wauza dawa wanajichanganya na wapiga debe,” anasema mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Ubungo darajani
Katika maeneo ya Ubungo kuna watu kadhaa wanahusika na dawa hizi; Kwa mfano yuko jamaa ambaye huzunguka usiku akisambaza dawa za kulevya kwa gari lake dogo. Hali ni mbaya zaidi eneo la Ubungo Maziwa, wapo hadi akina mama kadhaa kwenye vijiwe vya vijana wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Maeneo mengine ya Tanzania
Karibu nchi nzima, kuna kashfa hii ya kuwapo kwa dawa za kulevya, huku maswali makuu yakielekezwa kwa wana usalama nchini kama ni kweli hawaoni yanayoendelea.
Iundwe tume ya siri
Baadhi ya wananchi wanashauri kuundwe kikosi cha siri kuchunguza utendaji wa askari ili kutoa mashaka ambayo yanaonekana kuongezeka miongoni kwa jamii kuwa baadhi yao huenda wanashiriki katika biashara hii ya dawa mbalimbali za kulevya yakiwemo cocaine, mirungi na bangi.
Wanahoji ni kwanini Serikali ni kama inaonekana kushikwa na kigugumizi katika kupambana na tatizo hili la dawa za kulevya, licha ya idadi ya watumiaji ikionekana kuongezeka kadri siku zinavyokwenda mbele.
Wengine wakashauri Rais Kikwete kumaanisha katika kuchukua hatua na kuwachukulia hatua viongozi ambao wanaonekana wazi kutochukua hatua
Ahadi nyingi vitendo haba
Licha ya kuwapo madai mengi miezi ya hivi karibuni ikiwemo kwamba kuna viongozi wa dini wanahusika  na dawa za kulevya, wapo wabunge waliosema wanawajua wenye kufanya biashara hiyo, baadhi ya viongozi wakielezwa kuhusika.

Hali ya dawa za kulevya nchini
Kwa mujibu wa ripoti ya ofisi ya Waziri mkuu, Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, tatizo la dawa za kulevya nchini limeendelea kukua licha ya jitihada mbalimbali zinazofanyika katika kupambana nalo.
Hali hii inadhihirishwa na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kilichokamatwa hususan heroin na cocaine katika mwaka 2011 ikilinganishwa na mwaka 2012.
Takwimu zinaonyesha kuwa kilo 264.3 za heroin zilikamatwa mwaka 2011 ikilinganishwa na kilo 185.8 zilizokamatwa mwaka 2010. Takwimu hizi zinaonyesha.
Ongezeko la asilimia 42 la kiasi cha heroin kilichokamatwa katika kipindi cha mwaka mmoja tu. Aidha, mwaka 2011 kilo 126 za cocaine zilikamatwa ikilinganishwa na kilo 63 zilizokamatwa mwaka 2010 ambalo ni ongezeko la asilimia 100.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive