Thursday, 6 June 2013

Susan Rice mshauri wa usalama wa taifa

Rais Barack Obama, akiwapuuzia wakosoaji kutoka chama cha Republican, amemteua mwanadiplomasia Susan Rice kuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa, na kumpa sauti kubwa katika sera za mambo ya kigeni.
Licha ya shutuma kuwa alitoa taarifa zisizo sahihi kwa taifa baada ya mashambulio mabaya dhidi ya raia wa Marekani mjini Benghazi, nchini Libya Rice anachukua wadhifa huo kutoka kwa mshauri anayeondoka madarakani Tom Donilon.

Uteuzi huo uliofanywa jana Jumatano(05.06.2013) , pamoja na uteuzi wa mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Samantha Power kuchukua nafasi inayoachwa wazi na Rice kama balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa , unaashiria hatua ya Obama kuwapendelea washauri ambao wana mwelekeo wa kupendelea uingiliaji kati zaidi wa Marekani nchi za nje kwa minajili ya kuchukua hatua za kibinadamu.
Susan Rice

Obama hatarajiwi kubadilika

Lakini bado si wazi iwapo nadharia hiyo itabadilisha sera za rais Obama kuhusu Syria , ambako amezuwia mbinyo hadi sasa wa kutumia nguvu za kijeshi kuutatua mzozo wa nchi hiyo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Uteuzi wa Rice unatoa unatoa nafasi ya kupumua kidogo baada ya uchunguzi wenye utata uliofanyika mjini Benghazi kulazimisha kutoweza kufikiriwa kuchukua wadhifa wa waziri wa mambo ya kigeni katika kipindi cha pili cha utawala wa Obama .

Rais , ambaye alimtetea Rice kwa nguvu zote dhidi ya ukosoaji kutoka kwa wabunge wa chama cha Republican , amemsifu rafiki yake huyo wa karibu kwa kusema kuwa ni mzalendo halisi ambaye huweka maslahi ya nchi yake kwanza.
 Samantha Power

Wasifu

"Susan ni mtumishi halisi wa umma, ambaye huweka maslahi ya nchi yake mbele. Simuwoga na ni jasiri. Susan anatambua kuwa hakuna kitu mbadala kwa uongozi wa Marekani. Ni mwenye hamasa , na mtendaji. Na natambua kuwa Susan ni bingwa wa kweli wa kupigania haki na ubinadamu."

Lakini pia ni mtu mwenye kutambua kuwa tunapaswa kutumia nguvu zetu kwa busara na panapostahili.

Rice mwenye umri wa miaka 48 anachukua wadhifa huo wenye ushawishi mkubwa wa usalama wa taifa akiwa mtu wa karibu kabisa na rais kutoka kwa Tom Donilon , ambaye anaacha wadhifa huo mwezi Julai baada ya kutumikia kwa muda wa zaidi ya miaka mitano katika utawala wa rais Obamna.
Rais Barack Obama na rais wa China Xi Jinping

Mabadiliko katika ngazi ya juu ya kikosi cha utawala cha rais Obama yanakuja muda mfupi wakati akianza kupambana na agenda ya sera za mambo ya kigeni. Anatarajiwa kukutana na rais wa China Xi Jinping katika mkutano usio wa kawaida mjini Califonia kuanzia Ijumaa, na kisha atasafiri kwenda katika mataifa ya Ulaya na Afrika baadaye mwezi huu.
Rais Barack Obama na rais wa China Xi Jinping
na
Mwandishi: Sekione Kitojo/ape
Share:

Paris Jackson ajaribu kujiua

Bintiye marehemu Michael Jackson, Paris, mwenye unmri wa miaka 15, amelazwa katika hospitali moja mjini Carlifornia baada ya kujaribu kujiua. Msemaji wa familia ameeleza kuwa anaendelea kupata nafuu na kuwa madaktari wanamshughulikia vilivyo
Wanawe marehemu Jackson, Paris,Prince na Blanket

Inasemekana, Paris Jackson, ambaye babake alifariki mwaka 2009, amekuwa katika hali ya kusononeka kwa muda sasa.

Msemaji wa familia hiyo amesema kuwa usiku wa kuamkia leo binti huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kujaribu kujiua lakini anaendelea kupata nafuu.

Msemaji alifafanua kuwa hali yake si mbaya sana ya kupelekwa kwa wadi ya wagonjwa mahututi.

Paris Jackson ametajwa kama mmoja wa familia ya Michael Jackson anayetaka kulipwa mamilioni ya Dolar kutoka kampuni ya AEG ambayo ilimwajiri daktari aliyempa madawa Michael ambayo yaligunduliwa baadaye kuwa yalimwua.

Kesi inayohusiana na madai hayo imeendelea kwa majuma sita sasa. Mengi ya kusikitisha juu ya Michael Jackson yamekuwa yakitajwa na inadhaniwa kwamba yamechangia pakubwa kupandisha huzuni na simanzi kwa msichana Paris.

Inadhaniwa kuwa Paris amejaribu kadiri ya uwezo wake kumwomboleza baba yake lakini angali anasononeka kutokuwepo kwake. Mlezi wake kisheria ni nyanya yake Catherine lakini hata hivyo siku chache zilizopita amekuwa akiishi na mamake mzazi.
Share:

Wachina wakamatwa Ghana kwa uchimbaji haramu

  1. Maafisa wa uhamiaji nchini Ghana wanasema kuwa polisi wamewakamata zaidi ya raia 150 wa uchina ambao wanashukiwa kuhusika na uchimbaji wa dhahabu kinyume na sheria.
Ghana huzalisha kiwango kikubwa zaidi cha dhahabu barani Afrika

Kulingana na Francis Palmdeti kutoka idara ya uhamiaji nchini Ghana,raia hao wanazuiliwa katika migodi minne tofauti nchini humo.
Taarifa zinazohusiana
afrika magharibi

Mamlaka nchini Ghana ilikuwa imewataka raia wote wa kigeni kutohusika katika uchimbaji madini.

Taarifa zinasema kuwa raia wengi wa uchina wamekuwa wakihusishwa na uchimbaji madini wa kiwango cha chini nchini humo baada ya kuingia kinyume cha sheria kupitia mataifa jirani.

Hata hivyo msemaji wa ubalozi wa uchina nchini Ghana anasema kwamba anataraji kuwa raia hao watarudishwa makwao.

Wakati huohuo, wizara ya mambo ya kigeni ya Uchina imelalamikia serikali ya Ghana baada ya wafanyakazi hao wa China kuzuiliwa kufuatia msako uliofanywa wa wachimbaji haramu wa madini.

Ghana ndiyo nchi yenye kuzalisha kiwango kikubwa cha Dhahabu baada ya Afrika Kusini barani Afrika.

Huku bei ya dhahabu ikiendelea kupanda katika miaka ya hivi karibuni, sekta hiyo imekuwa ikikumbwa na wachimbaji haramu wa madini hayo ikiwemo, idadi kubwa ya wafanyakazi wa kichina inayoendelea kuongezeka.

China imesema kuwa intaka watu hao kutoteswa na kutoibiwa wakati wa msako huo.
Share:

MUME WA KHADIJA KOPA AFARIKI DUNIA

Khadija Omar Kopa akiwa na mumewe Jaffari Ally enzi za uhai wake.
Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya Bagamoyo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.
Share:

AFISA WA BANDARI ANASWA AKIOMBA RUSHWA YA NGONO KWA MWANAFUNZI ILI AMPE AJIRA BANDARINI

 Mtuhumiwa akihojiwa na polisi

MWANAMUME aitwaye Andrew Kabula (34), mkazi wa Kimara Mwisho jijini, hivi karibuni alinaswa gesti akiwa na mwanafunzi ‘denti’ aliyetaka kufanya naye ngono ili ampatie kazi bandarini..
Kabula a.k.a Afisa Feki alijitapa kwa denti huyo kwamba ni Afisa wa Mamlaka ya Bandari jijini Dar na ana uwezo wa kumpatia kazi kama atampa rushwa ya ngono.

Kwa kutambua kwamba kitendo hicho ni kosa kisheria, denti huyo (jina lake kapuni) aliwasiliana na Oparesheni Fichua Maovu ili kumnasa afisa huyo feki.
Waandishi wetu waliwasiliana na polisi wa Kituo cha Mbezi Luis jijini Dar na kumwekea mtego jamaa huyo katika gesti aliyoichagua, iliyopo maeneo ya Kimara jijini Dar.
Afisa huyo kila mara alikuwa akiwasiliana na denti huku akimsisitiza kutoondoka hapo kama kweli alitaka ajira
Waandishi, askari na denti walitangulia katika gesti hiyo na afisa akataarifiwa na denti kwamba ameshafika eneo la tukio.

Yakafuata maelekezo ya kuchukua chumba kutoka kwa afisa huyo aliyedai kwamba yupo mbali kidogo.
Saa moja usiku, afisa feki alifika katika eneo la tukio na kuingia chumbani katika gesti hiyo (jina tunalo), huku askari na waandishi wakifuatilia nyendo zake.

Bila ya kushtuka kama amewekewa mtego, moja kwa moja afisa aliingia chumbani na kumkuta denti huyo ambaye alizidi kumsisitizia lengo lake.

Baada ya kuhakikishiwa kile anachokitaka na denti huyo, afisa alisaula viwalo vyake vyote na kuwa tayari kwa tendo.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive