Saturday, 29 June 2013

NAY WA MITEGO NA DIAMOND KUJA NA NGOMA MPYA..."SALAMU ZAO"

Diamond plutnum akiwa na NAY wa Mitego

Baada ya kutamba na Muziki Gani, Diamond na Nay Wa Mitego wako mbioni kuachia ngoma nyingine hivi karibuni baada ya kupembua ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’.

Nay ameiambia mpekuzi kuwa kuna nyimbo tatu ambazo zipo tayari, Salamu Zao, Kwa Masela na Utakula Jeuri Yako, hawajajua ipi itaanza kutoka kwasababu kila mmoja yupo katika tour zinazoendelea.

Wamesema wakikaa wakashauriana na wadau mbalimbali ndipo watakapoamua mzigo upi uingie mtaani kwanza.

“Kuna kazi ambazo zinakuja hivi karibuni ambazo nimefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi sijajua ni ipi ambayo itaanza kutoka lakini tutawaita wadau wachague ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’ ambazo zipo tayari na ‘Utakula Jeuri Yako’ nimefanya mwenyewe...

"Ilibidi tutoe nyimbo ambayo tumefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi hakuna maamuzi ya moja kwa moja tuitoe au kila mtu atoe ya kwake au tutaendelea na project yetu iliyoendelea, kwahiyo wadau wakae mkao wa kula,” amesema Nay.


Share:

MAMIA NCHINI AFRIKA KUSINI WAJITOKEZA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA KUJA KWA RAIS OBAMA WAKATI ALIPOTUA JANA JIONI KATIKA JIJI LA PRETORIA

Waandamaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Rais Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika jana Jioni wakati Raisi Obama alipotua Katika Jiji Hilo jana Jioni Juni 28

 Waandamaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Rais Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya Juni 28

Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Rais Obama Nchini Humo Mapema jana wakati Rais Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ametokea Nchini Senegali na Kutua Nchini Afrika Kusini huku Akihitisha Ziara Yake Nchini Tanzania wiki ijayo.

Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Rais OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo. Mwandamaji huyu amebeba bango jana Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao. Picha Zote na REUTERS/AFP


Share:

MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU "BRIAN DEACON" AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.

Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS.
  Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''

Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.
 Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.
watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.


Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.


Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.

watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.
Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel
.

Share:

Wednesday, 26 June 2013

Ulinzi wa Obama haujawahi kutokea Afrika

 
Tayari baadhi ya wanajeshi wa Marekani wamewasili Dar es Salaam na kuweka mitambo ya mawasiliano maeneo yote ambayo atapita au kukagua. SHARE THIS STORY Tweet 0 in Share Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake ya Afrika mwaka huu. Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam. Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687 wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali, ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23, ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha ulinzi. Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu iwapo lolote litatokea. Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili hiyo. Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.
Share:

TUTAIFUTA CHADEMA ENDAPO ITABAINIKA KUWA WALIRUSHA BOMU LA ARUSHA WENYEWE"....TENDWA

 


Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa, amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 atakifuta. Tendwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp kuhusu hatua zitakazochukuliwa... Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu.
Share:

MZEE MANDELA AFANYIWA MAOMBI MAALUM

ASKOFU mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini. Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia. Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria. Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili. Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu. Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa. Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana. Chanzo: bbcswahili

Share:

Ujio wa Obama: Mashirika ya ndege yatakiwa kubadili ratiba za safari Julai Mosi

Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.

Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini. Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa. “Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali. “Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Share:

RAIS WA MAREKANI BARAK OBAMA KUANZA ZIARA BARANI AFRIKA LEO

Rais Barack Obama anafanya ziara ya pili barani Afrika kuanzia leo Jumatano. Atazuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Rais wa Marekani Barack Obama Jumatano anaanza ziara ya wiki moja nzima katika nchi tatu za Afrika kwa lengo la kuhamasisha demokrasia na uwekezaji wa Marekani barani humo.

Rais Obama atakwenda Senegal leo Jumatano ambako atakutana na rais Macky Sall na kesho Alhamis atatembelea nyumba ya kihistoria ya watumwa wa Afrika walioletwa Marekani katika kisiwa cha Goree.
Ijumaa bwana Obama atakwenda Afrika Kusini ambako atakutana na rais Jacob Zuma na kutembelea kisiwa cha Robben ambacho rais wa zamani Nelson Mandela alifungwa jela.

Maafisa wa Afrika Kusini walisema ziara ya bwana Obama itaendelea licha ya kuwepo na hofu kote nchi humo kuhusu kudhoofika kwa afya ya bwana Mandela. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye miaka 94 yuko katika hali mahtuti na amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.

Share:

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERIA

Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.
“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.
Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.
Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.
Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.
Alieleza kuwa Kifungu cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.
Kauli hiyo ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi, ilitolewa ikiwa ni ufafanuzi wa jibu la swali la nyongeza lililoulizwa bungeni Mei 28,2013 na Rashir Ally Abdalah (Tumbe-CUF), ambapo Silima alisema mauaji yanayofanywa na askari polisi ni mauaji ya kisheria.

Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashi Mohammed aliomba mwongozo wa spika kupata ufafanuzi wa kauli hiyo, na jana Silima kutoa kauli ya Serikali kujibu mwongozo huo.
“Ikumbukwe pia kuwa, kifungu cha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi Sura322, pamoja na Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi Na274, vinampa haki ya kisheria askari polisi kubeba na kutumia silaha za moto ikiwamo bunduki na mabomu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku..,”alisema Silima.
Alifafanua kwamba katika kutafsiri sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ikiwamo alizozitaja, mahakama katika nyakati tofauti imetoa msimamo wa kisheria juu ya suala hilo.
Akitoa mfano alisema: “Mathalan katika kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuri ya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa na Tanzania Law Report ukurasa wa 122, ambapo mshitakiwa (mwomba rufaa) alimjeruhi kwa panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwake na kuanza kumshambulia.”
Alisema katika kesi hiyo,mahakama ya rufaa pamoja na kuridhia uamuzi wa mahakama ya awali wa kumtia hatiani kwa kutumia nguvu kupita kiasi, ilibainisha kuwa mshtakiwa hakustahili adhabu kwani alitenda kosa lile wakati akijihami dhidi ya mashambulizi toka kwa mlalamikaji.
“Kwa msingi huo, tarehe 28 Mei, 2013 wakati nikijibu swali Na 290, nilitumia maneno ‘mauaji yanayofanywa kisheria’ nikimaanisha mauaji yanayotokea katika mazingira niliyoeleza..,”alisema Silima.
Hata hivyo alisema siyo nia ya Serikali kuhalalisha vitendo vya matumizi mabaya ya silaha ambavyo vinaweza kufanywa na askari wasio waadilifu.
Alibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kuheshimu haki za raia na kutumia busara kutatua migogoro.
Hata hivyo, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imelaani kauli ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi iliyoitoa jana na kueleza kuwa haikubaliani nayo kwa kuwa inatoa baraka kwa polisi kuendeleza mauaji ya raia.
Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kikao cha bunge kuahirishwa, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa kambi hiyo rasmi, Vicent Nyerere alisema kauli hiyo ingekuwa na uthabiti kama askari polisi wangekuwa waadilifu.
“Kauli ingekuwa thabiti kama polisi wangekuwa waadilifu. kabla ya kutoa kauli hiyo, Serikali ilitakiwa kuchuja miongoni mwa askari wa jeshi la polisi, wa ngazi zote na kuwaondoa wasio waaadilifu ndipo wakatoa kauli hiyo wananchi wataielewa Serikali,”alisema Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini(Chadema).
Kwa upande wake, Mbunge wa Ole, (CUF) Rajab Mbarouk Mohammed akizungumzia kauli hiyo ya Serikali alisema kuwa majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima ni ya kisiasa.
Alisema kwamba kauli hiyo ni mwendelezo wa kauli iliyotolewa Alhamisi iliyopita na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwataka pilisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote watakaokaidi kutii sheria.
“Hakuna mwenye haki ya kuua, kuua ni kuua tu. Mahakama pekee ndiyo ina haki ya kuhukumu kifo baada ya kumtia hatiani mshtakiwa husika. Lakini kuwa polisi wanafundishwa utii, siyo kuua,”alisema Rajab.
Alifafanua kuwa kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao na kwamba kuruhusiwa kujihami haimaanishi kuua raia.
Nao Wabunge Aeshi Hilaly na Aly Keissy walisema ni vizuri raia wakatii mamlaka iliyopo na kutekeleza utii wa sheria bila shuruti.
Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu alisema: “Maoni yangu haki za watuhumiwa lazima ziheshimiwe.”
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS), Francis Stola alisema hakuna sheria inayompa mamlaka askari polisi kutumia nguvu za ziada ikiwemo kupiga raia pindi anapotekeleza majukumu yake,isipokuwa tu anaweza kutumia nguvu kiasi iwapo raia anayekabiliana naye anaonyesha vitendo vya kukaidi amri ama kuhatarisha usalama
Stola ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kauli bungeni alisema kuwa kwa kufuata sheria polisi haruhusiwi kupiga raia. “ Ukisoma sheria hakuna mahala utakuta kuna neno limeandika piga…. Askari polisi anachoweza kufanya ni arrest(kamata) na siyo vinginevyo, hana mamlaka kabisa ya kupiga raia”
Alisema sheria imetamka wazi kuwa kunapojitokeza hali yoyote inayopaswa kdhibitiwa na vikosi vya ulinzi, nguvu inayopaswa kutumika ni ile ya kawaida na kwamba kitendo cha kutumia risasi za moto ama kupiga raia ni ukiukwaji wa sheria za nchi.
Alisema polisi anapaswa kutoa mwongozo kwa raia kumwelekeza jambo la kufanya iwapo kunajitokeza hali ya sintofahamu,lakini hapaswi kutumia nguvu kupita kiasi ikiwemo kuwapiga raia
“ Sheria inasema wazi kwamba panapojitokeza hali yoyote korofi, polisi wanatakiwa kutumia nguvu ya kawaida tu kukabiliana na hali hiyo na wala siyo kutumia silaha za moto… silaha za moto zinaweza kutumika tu iwapo kunajitokeza tukio ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa maisha ama mali isipotee” alisema
Kuhusu wananchi kufanya maandamano, rais huyo alisema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia,lakini yanafanyika katika utaratibu maalumu. “ maandamano ni haki ya kila raia lakini panapaswa kuwa na utaratibu maalumu…. Kama kunajitokeza maandamano ambayo hayana utaratibu polisi wanapaswa kutumia reasonable force (nguvu ya kawaida) kudhibiti maandamano hayo na wala siyo kutumia nguvu za ziada.

Mwananchi:

Share:

Kauli ya Pinda inahitaji mjadala wa kitaifa

 
Kauli ya Waziri Mkuu Pinda inatia hofu, hasa inapotolewa kwa Jeshi la Polisi lenye muundo uliorithiwa kutoka kwa wakoloni. Tofauti na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambalo mwaka 1964 lilifanyiwa mabadiliko makubwa kutoka jeshi la kikoloni na kuwa jeshi la wananchi, Jeshi la Polisi tulilorithi kutoka kwa wakoloni lilibakia hilohilo kimuundo na kwa kiasi kikubwa kisheria.

Tangu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atoe kauli tete Bungeni wiki iliyopita ya kulichochea Jeshi la Polisi liendeleze vipigo na mateso kwa wananchi aliodai wanakaidi sheria za nchi, wamejitokeza baadhi ya watu, wakiwamo mawaziri wakijaribu kuipaka sukari kauli hiyo ili itafsiriwe na kuonekana kama ni ya kuhimiza utiifu wa sheria.
Hatari ya kauli hiyo kwa amani na usalama wa wananchi inatokana na ukweli kwamba inaonyesha kama vile nchi yetu inatawaliwa kijeshi. Kinyume chake, nchi yetu inaongozwa na Katiba, kwa maana kwamba Serikali iliyopo madarakani ilichaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura. Haikupatikana kwa mtutu wa bunduki na mapinduzi ya kijeshi.
Kwa maana hiyo, Katiba ya Tanzania na sheria zilizotungwa na Bunge ni mwongozo kwa watawala kuhusu namna ya kuendesha Serikali kwa njia za kidemokrasia na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao. Anapotokea kiongozi wa juu wa Serikali akalichochea Jeshi la Polisi kuvunja Katiba na sheria za nchi kwa kufanya vitendo vinavyosababisha hofu na kuhatarisha amani na maisha ya raia lazima wananchi wapaze sauti, wamlaani kwa nguvu zote na wamwambie ‘hapana’.
Kauli ya Waziri Mkuu Pinda inatia hofu, hasa inapotolewa kwa Jeshi la Polisi lenye muundo uliorithiwa kutoka kwa wakoloni. Tofauti na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambalo mwaka 1964 lilifanyiwa mabadiliko makubwa kutoka jeshi la kikoloni na kuwa jeshi la wananchi, Jeshi la Polisi tulilorithi kutoka kwa wakoloni lilibakia hilohilo kimuundo na kwa kiasi kikubwa kisera.
Kimsingi ni Jeshi lililoundwa kupokea amri na kutekeleza matakwa ya watawala ya kuwakandamiza wazalendo, hata kama wazalendo hao wanadai haki zao za kiraia na kikatiba kama Jeshi la Polisi la Makaburu wa Afrika Kusini lilivyokuwa likiwaua na kuwatesa wazalendo waliokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi. Ndiyo maana hapa nchini umekuwapo uhasama mkubwa kati ya jeshi hilo na wananchi. Watawala wanaonekana kufurahia hali hiyo ambayo tayari imesababisha vifo na mateso kwa raia wasiokuwa na hatia.
Waziri Mkuu anasema jeshi hilo lazima liwapige wananchi anaodai wanakaidi amri halali ya Polisi. Tunauliza amri halali ya Polisi ni ipi? Kupiga marufuku mikutano ya vyama vya upinzani na kuisambaratisha kwa mabomu na silaha za kivita bila sababu za msingi ni amri halali ya wapi? Tunasema hiyo siyo amri halali na inakwenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 inayovitaka vyama hivyo kutoa tu taarifa ya mikutano hiyo kwa Polisi ndani ya saa 24 ili vipatiwe ulinzi. Jeshi hilo sasa limejipachika madaraka ya kutoa vibali, kukataa ama kukubali kwa kutoa masharti ya ajabu. Je, hayo ni maagizo ya chama tawala na serikali yake?
Sisi tunasema kauli ya Waziri Mkuu Pinda inahitaji mjadala wa kitaifa. Ni kauli hatari. Tuikatae, kwani inalenga kuhatarisha amani na umoja wetu. Jaji mstaafu Mark Bomani juzi alionyesha njia alipotahadharisha Serikali na jeshi hilo dhidi ya kutumia nguvu kubwa kukabiliana na umma kwa kutumia silaha za moto. Alionyesha wasiwasi kama kweli Polisi wana uelewa mzuri wa sheria kuhusu matumizi ya silaha za moto au wanafanya kazi kwa kuagizwa tu. Tunahitaji sauti nyingi kama hiyo.
Share:

Tuesday, 25 June 2013

"LAZIMA NIFE KABLA YA KUFIKISHA MIAKA 40"...AUNT EZEKIEL

WAKATI vifo vikizidi kuwatafuna wasanii, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka na kudai kuwa hawezi kuishi miaka mingi na atakufa mapema kuliko watu wanavyodhani.

Aunt Ezekiel alifunguka hayo juzikati alipokuwa akipiga stori na mwandishi wetu jijini Dar ambapo alibainisha kuwa akijitazama mustakabali wa maisha yake basi anaona kabisa kuwa hawezi kufikisha hata miaka 40 kabla hajafa.

“Daah! Sijielewi kabisa yaani kwa jinsi ambavyo najiona, nikifikisha miaka 40 ni bahati aisee, dunia sasa imebadilika sana,” alisema Aunt.


Share:

MWANAMKE AOLEWA NA WANAUME WAWILI NA KUISHI NAO...!!!


MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji iitwayo Kayoga.

Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.

“Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sauti pale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anaweza kuongeza mwanamume mwingine,” anasema mmoja wa majirani hao.

Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa na amani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.

Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mume mkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliweka pingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’ wa mtoto huyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sita iliyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye baba mzazi wa mtoto.

“Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandalizi yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huo ilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia pale Padri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.

“Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado bali wake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena na majibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana,” alisema Katekista Abel.

Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wake ni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapo na baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidia mkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogo wake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.

Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.

"Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugia mpangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa hao yanawahusu nini watu hao?” alihoji.

“Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumba nitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?” alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwamba wataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akina mama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaume wawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufunga ndoa na mume mmoja.

Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili na kuwa na mamlaka juu yao.
Share:

POLISI WAMKEMEA JOYCE KIRIA KWA KUANDAMANA, HAYA HAPA NDIO MAJIBU


Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu (Imetolewa na Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania)
Joyce Kiria akizungumza na waandishi wa habari Jana jijini Dar es salaam ambapo alidai hajui mume wake yuko wapi



Share:

VIONGOZI WATANO WA CHADEMA WASHITAKIWA KWA UGAIDI .... MAJINA YA VIONGOZI HAO HAYA HAPA

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na vijana wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu mkazi Tabora mjini.

Mbali ya Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni Evodius Justinian wa Buboka, Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel Kihawa wa Dodoma, leo wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na kumwagia tindikali Musa Tesha katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwaka 2011.

Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.

Kesi hiyo ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, ya Tabora Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara Baada ya kusomewa shitaka hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili Prof Abdalah Safari, ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela ulitoa hoja kuiomba mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa sababu, kwanza mashtaka hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.

Sheria za uendeshaji wa makosa kama hayo hapa nchini zinadai kuwa mashataka kama hayo yanapofunguliwa ni lazima ridhaa ya Mkurugenzi wa mashtaka iwepo. Kwa kuwa ridhaa hiyo haikuwepo, mawakili waliiomba mawakili kuitupilia mbali kesi hiyo.


Sababu ya pili iliyotolewa na upande wa Utetezi ilikuwa kwamba maelezo ya kesi kuwa ni ya ugaidi, yalikuwa hayaonyeshi kuwa ni ya kigaidi tofauti na makosa mengine ya kawaida kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hivyo waliiomba Mahakama kutupilia mbali shitaka hilo au lifunguliwe kama kosa la kawaida.

Na sababu ya tatu ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, sheria inaelekeza kuwa mshitakiwa ashitakiwe katika mahakama yenye mamlaka na hadhi kama ile waliyopelekwa katika maeneo yale walikokamatwa. Hivyo mawakili waliiomba mahakama itupilie mbali shitaka, kwani washitakiwa kama walikuwa na hatia walipaswa kushitakiwa katika maeneo yao walipokamatwa. Baada ya hoja hizo, Mahakama iliahirisha kesi hiyo na itatajwa tena Julai 8 mwaka huu Tabora Mjini.

Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi au wafuasi wa chadema kufunguliwa kesi zinazohusiana na ugaidi, tarehe 18 Machi 2013, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare, la Ludovick Joseph walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya ugaidi.


Kosa jingine lililowakambili Lwakatare na Ludovick ni kula njama; kosa ambalo pia linawakabili washtakiwa wote ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume na kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Katika kosa la tatu, washtakiwa wote wawili wanadaiwa kufanya mkutano wa kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi.

Wakili wa serikali alidi kuwa washitakiwa wote Desemba 28 Mwaka jana walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyara Msaki kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi.

Pamoja na tuhuma hizo, 8 Mei, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimfutia mashitaka matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Katika uamuzi huo Jaji Lawrance Kaduri akitoa uamuzi huo alisema ulitokana kukubaliana na hoja ya mawakili wa Lwakatare; Tundu Lissu, Peter Kibatara na Mabere Marando na kusema kuwa.

“Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama inatoa amri ya kumfutia Lwakatare mashitaka matatu, yaani kosa la pili, tatu na la nne kwa sababu Jamhuri imeshindwa kuonesha maelezo yanayotesheleza kumshitaki Lwakatare kwa kesi ya ugaidi.


“Naamuru jalada la kesi ya msingi lilirudishwe Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya mshitakiwa kuendelea kushitakiwa kwa kosa moja la kula njama ambalo linaangukia katika sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002,” alisema Jaji Kaduri

Share:

USHAIDI WA PICHA MME WA JOYCE KIRIA NA VIJANA WENGINE WACHADEMA WAKIWA NA PINGU,KESI YA UGAIDI IGUNGA


 Bw.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza 
Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.
Kamanda Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na wtuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013.



Share:

MAREKANI YATOA ONYO KALI KWA MSAFARA WA RAIS OBAMA TANZANIA

Dar es Salaam. Licha ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.
Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.
Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi
Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa na gharama kwa walinzi, lakini safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.
Tahadhari
Kwa mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya Marekani, ambayo Mwananchi imepata nakala yake, watu watakaokuwa kwenye msafara wa Obama wametakiwa kutotumia kachumbari. Pia imewataka kutumia maji ya chupa zaidi.
“Kutokana na mfumo wa maji uliopo, tunashauri watu wetu kutumia maji ya chupa zaidi kwa kunywa na hata kwa kupiga mswaki,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa kuelewa fika tatizo la ugonjwa wa malaria nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa kutumia dawa ya mbu ya kupaka na kupuliza inayoitwa Deet.

Deet ni dawa maarufu huko Marekani na ikiwa katika aina tofauti ikiwamo ya kupaka na kupuliza na imekuwa ikitumiwa na jeshi la Marekani kwenye vita mbalimbali tangu miaka ya 1940 kabla ya kuanza kutumiwa na raia mwaka 1957.
ATM nazo noma
Pia watu watakaokuwa kwenye msafara wa Rais Obama wametakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za kutolea fedha (ATM) zilizoko karibu na hoteli watakazofikia.
“Kuna tatizo la uhalifu kwa hiyo siyo vizuri kutumia ATM ambazo ziko katika sehemu zisizo salama. Pia katika kipindi watakachokuwa Tanzania watu wanapaswa kutumia teksi ambazo zimeidhinishwa na hoteli.
“Pia siyo vizuri kuacha kompyuta ya fedha kwenye vyumba mtakavyolala. Pia kina mama wanapaswa kuchukua tahadhari ya mabegi yao watakapokuwa wanapita mitaani,” ilitahadharisha taarifa hiyo.

Share:

TUMUOMBEE MZEE MANDELA AFYA YAKE YAZIDI KUDORORA, IKULU KWA ZUMA HAKUKALILIKI...!!!

Nelson Mandela ‘Madiba’.

Habari hizo ambazo awali zilifanywa siri kabla ya kuvuja wikiendi iliyopita, zinasema kuwa Ikulu ya Afrika Kusini ilikosa umakini, hivyo ikaacha gari bovu limbembe Mzee Mandela na matokeo yake lilizimika kwenye barabara kuu (high way).

Kuzimika kwa gari hilo, kulisababisha hekaheka lakini ufumbuzi wa haraka ulikosekana mpaka dakika 40 baadaye ndipo ‘ambulance’ nyingine ilipofika eneo la tukio, ikambeba Mzee Mandela na kumuwahisha hospitali.

Ikulu ya Afrika Kusini imelazimika kutoa tamko, baada ya wachambuzi kuelezea tukio hilo kwamba zilikuwa dakika 40 za hatari za Mzee Mandela, kwa maana nusura zichukue uhai wa kiongozi huyo aliyeongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, miaka ya 1900 nchini humo.
Tukio lenyewe, lilijiri Juni 8, mwaka huu (zaidi ya wiki mbili zilizopita) lakini ikawa kimya katika vyombo vya habari, japo minong’ono iliendelea kushamiri, kabla ya mambo kuwekwa hadharani wikiendi iliyopita.

KIVIPI DAKIKA 40 ZA HATARI?
Kwa mujibu wa habari pamoja na makala za wachambuzi mbalimbali wa kisiasa nchini Afrika Kusini, muda mfupi baada ya Mzee Mandela kuondolewa barabarani pale gari lilipomzimikia na kuwahishwa katika Hospitali ya Mediclinic Heart, Pretoria, uvumi ulienea kuwa ameshafariki dunia.

Mchambuzi wa siasa za Afrika Kusini, Olwethu Sipuka ambaye makala zake hupatikana zaidi kwenye Tovuti ya Politicweb ya nchini humo, alieleza kuwa zile dakika 40 zilikuwa za hatari mno kwa Mzee Mandela ndiyo maana wananchi waliamini uvumi kuwa alifia pale.
“Afadhali taarifa za gari lililomzimikia zilisambaa baadaye, kama zingewahi, wananchi wangekusanyika eneo la tukio na pengine ingekuwa hatari sana kwa afya ya Madiba,” aliandika Sipuka na kuongeza:
“Kama wananchi wangewahi kufika pale barabarani, pengine wangetaka kumbemba Madiba wampeleke hospitali. Kama wangeamini amekufa, isingekuwa rahisi kwao kukubali ambulance nyingine imbembe. Hiyo ni hatari ambayo ingeweza kumsababishia kifo.”

Kwa upande mwingine, habari zinasema kuwa baada ya gari kuzimika, Mzee Mandela hakupata huduma yoyote kwa muda wote wa dakika 40 ambazo alikwama pale barabarani.
Dk. Mamphela Ramphele ambaye naye ni mchambuzi wa siasa za nchi hiyo, alihoji katika makala yake ni kwa nini baada ya kuzimika ambulance ambayo ni ya kijeshi, haikwenda nyingine ya serikali kumchukua Mzee Mandela, badala yake ikaenda ya kiraia?

Aliandika kuwa afya ya Mzee Mandela haipaswi kufanyiwa mchezo, kwani jeshi la Afrika Kusini halina ambulance moja, ile ya kiraia haiwezi kuwa na ubora unaotoa huduma kwa mgonjwa anayestahili matibabu ya ICU (kiwango cha uangalizi wa hali ya juu).

Zipo taarifa zinazosema kuwa zile dakika 40 alizokwama barabarani, zilisababisha hali ya Mzee Mandela iwe mbaya zaidi, kwani baada ya ambulance ya pili kuwasili, aliwekwa katika mashine ya oksijeni ambayo ilimsaidia kupumua mpaka alipofikishwa hospitali.
Mchambuzi mwingine, Blade Nzimande, aliandika kuwa kutoka Johannesburg, nyumbani kwa Mzee Mandela mpaka Pretoria kwenye Hospitali ya Mediclinic Heart, ni umbali wa zaidi ya maili 31 (kilometa 50) hivyo ilihitajika umakini wa hali ya juu.

“Alitolewa nyumbani akiwa na hali mbaya, inafahamika macho yote ya wananchi wa Afrika Kusini yanafuatilia mwenendo wa afya yake. Gari lililombemba halikutakiwa kuwa na hitilafu ya injini. Kuna uzembe mkubwa umefanyika.”

IKULU YATOA TAMKO
Kutokana na kuenea kwa uvumi huo, Ikulu ya Afrika Kusini, wikiendi iliyopita, ilitoa tamko kuhusiana na tukio hilo la ambulance iliyokuwa imembeba Mzee Mandela kuzimika barabarani.

Msemaji wa Ikulu ya Afrika Kusini, Mac Maharaj, alisema kuwa ni kweli kwamba gari lililokuwa limembeba Mzee Mandela lilizimika barabarani lakini halikumwathiri kwa chochote.

“Alikuwa na madaktari ambao walijiridhisha kwamba hakutakuwa na hatari yoyote katika kusubiri gari lingine la kumpeleka hospitali,” alisema Maharaj kwa niaba ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.

Aliongeza: “Ambulance iliyokuwa imembeba ilikuwa inasindikizwa na magari mengine, kwa hiyo kama hali ingekuwa mbaya zaidi, angehamishwa katika gari lingine na kukimbizwa hospitali. Haikuonekana hatari kubwa.

“Timu ya madaktari kutoka idara ya ulinzi ilijiridhisha kwamba afya ya Mzee Mandela itakuwa salama ndiyo maana waliruhusu subira hiyo ya dakika 40. Ile ambulance ni ya jeshi, tulipewa taarifa baada ya kuzimika, tukafanya juu chini kupata nyingine, ikaonekana itachelewa zaidi ndiyo maana ikatumika ya kiraia.

“Tunapenda wananchi wote wajue kuwa tupo makini na afya ya mzee wetu. Ile ambulance ya kijeshi ina vifaa vyote ya ICU na madaktari waliokuwa wamemzunguka ni madaktari bingwa, kwa hiyo wana uwezo mkubwa. Hakukuwa na uzembe hata kidogo.”

ZUMA IKULU HAPAKALIKI
Kwa mujibu wa taarifa za Ikulu ya Afrika Kusini, afya ya Mzee Mandela, inasababisha Rais Zuma asiwe na utulivu, kwani muda mwingine anafuatilia maendeleo ya kiongozi huyo aliyewahi kufungwa jela miaka 27, kipindi anaongoza harakati za kupinga sera za ubaguzi wa rangi nchini humo.

Imeelezwa kuwa tangu Aprili 29, mwaka huu, pale Zuma alipomtembelea Mzee Mandela na kuona ukweli jinsi afya yake inavyobadilika na kuwa mbaya zaidi, amekuwa hakai akatulia ikulu, badala yake hutumia muda mwingi kufuatilia maendeleo ya rais huyo wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini.

Habari zinafafanua kuwa siku hiyo, Zuma ambaye aliongozana na viongozi wengine wa Chama cha African National Congress (ANC), kwenda kumjulia hali hali, alishtushwa kuona Mzee Mandela akiwa hatikisi kichwa wala kupepesa macho.

Chanzo kimoja kutoka Ikulu ya Afrika Kusini ambacho hakikutajwa jina, kilieleza kwamba hata safari za nje, Zuma amezipunguza kwa hoja kwamba taifa halitamwelewa yeye kuwa mbali katika kipindi hiki ambacho Mzee Mandela anaumwa sana, japo afya yake inaelezwa kuimarika.

MBEKI AWATOA HOFU WANANCHI
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, amewatoa hofu wananchi wa nchi hiyo kuwa Mzee Mandela anaendelea vizuri, ingawa katika siku za hivi karibuni amekuwa akipelekwa hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kutibiwa.
Mbeki aliyemrithi Mandela mwaka 1999, alisema kuwa ni vizuri wananchi wakadumisha sala kwa kumwombea mzee huyo badala ya kukata tamaa na kuamini uvumi kwamba ameshafariki dunia.

ANC YATAKA MANDELA AHESHIMIWE
Chama cha ANC, Jumamosi iliyopita, kilitoa tamko kuwa Mzee Mandela inabidi aheshimiwe na kwamba siyo kila mtu anaweza kuwa msemaji wa maendeleo ya afya yake.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Ikulu ya Afrika Kusini inabidi ifanye kazi vizuri kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kweli na zenye uhakika kuhusu kiongozi huyo aliyeiongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 1994 mpaka 1999.

“Chama chetu cha The African National Congress kwa mara nyingine kinataka pande zinazohusika zifanye kazi yake. Vilevile tunataka vyombo vya habari na familia, kuheshimu taarifa za faragha kuhusu Mandela.”

TATIZO NI MAPAFU
Mzee Mandela ambaye mwezi ujao anatarajiwa kutimiza umri wa miaka 95, kwa muda mrefu sasa anasumbuliwa na tatizo la mapafu kujaa maji.
Habari zinasema kuwa tatizo la mapafu, ni matokeo ya athari alizozipata akiwa gerezani kipindi alipofungwa miaka 27 jela katika miaka ya 1900.
TUMUOMBEE MZEE MANDELA

Mandela amekuwa kielelezo chema siyo tu kwa Afrika Kusini, bali Afrika na duniani kote. Nasi Watanzania kila mtu kwa imani yake ni vema kumuombea salama ili Mungu ampe nafuu na kumponya maradhi yanayomsibu kwa sasa.
Share:

HAWA NDIO AINA YA WANAUME ASIOWAPENDA JACQUELINE WOLPER "GAMBE"

Jacq wolper

Jacqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai hawapendi wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu na si rahisi kuonyesha mapenzi yao ya dhati kwake, pia hawezi kutembea nao hadharani kwa kuhofia ndoa zao.

“Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake halafu mtu mzima hivi unakosa penzi la kweli. Mapenzi yenu yatakuwa ya chumbani tu,” alisema.

“Hamtaweza kutembea pamoja, lakini ukiwa na kijana ambaye ni rafiki hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake.

“Wengi wenye fedha zao kuna wakati wananiona nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke, ninahitaji kuwa na mtu anayenijali na kuwa karibu na mimi.

“Kuna watu wanaamini fedha zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau.”
Anasema wengine huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni malaya, lakini wanasahau kuwa nao ni binadamu.

“Kila binadamu anapenda na kupendwa,” alisema.

Share:

MAMA ALIA BAADA YA KUJIFUNGUA MAPACHA WALIOUNGANA KWENYE MAKALIO MBEYA...!!!


MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Kasumuru, Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Grace Joel Lwesha (19), amelia baada ya kujifungua watoto walioungana.Akizungumza na waandishi wetu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jengo la Watoto, Grace alilia kutokana na kile alichodai kujifungua watoto walioungana wakati yeye ni maskini.
Watoto hao mapacha wa kiume, Eliudi na Elikana wameungana sehemu ya makalio hivyo kulazimika kutumia sehemu moja ya haja kubwa.

Grace aliwaambia waandishi wetu kwamba, watoto hao walizaliwa katika Hospitali ya Kyela, Februari 20, mwaka huu wakiwa na miguu miwili na mikono miwili kila mmoja.
“Baada ya kujifungua Machi mosi nilihamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa uchunguzi zaidi ili waweze kujua ni jinsi gani watakavyotenganishwa,” alisema.

Hata hivyo, hospitali hiyo ya mkoa haikufanikiwa badala yake Machi 16, walimhamishia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kuanzia hapo mpaka sasa anafanyiwa maandalizi kwa ajili ya safari ya kupelekwa nchini India kwa upasuaji.
“Ninawapenda sana watoto wangu hawa pamoja na kwamba wapo katika hali hii, ndugu zangu walipokuja hospitalini kuniona akiwema mama yangu walinifariji na kunisihi nisiwachukie nizidi kuwapenda.

“Kuwatunza ni kazi ngumu sana kwani mara nyingi wamekuwa wakininyima usingizi kwa sababu wamekuwa wakilala kwa nyakati tofauti.
“Nakumbuka siku niliyojifungua mume wangu alikosa raha lakini sasa anawapenda kwani amejua kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.

“Maisha yetu ni magumu kwani tunatoka kwenye familia maskini, kazi yetu ni kilimo cha kutumia jembe la mkono hivyo bado kuna mahitaji mengi nashindwa kumudu. Nichukue nafasi hii kuwaomba msaada Watanzania wote walioguswa na tukio hili,” alisema Grace.
Grace alifunga ndoa na Erick William Mwakyusa Desemba 23, 2010 na katika ndoa yao wamejaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Lide (3) na hao mapacha ni uzao wake wa pili.

Mama huyo anaomba msaada kwa mtu yeyote aliyeguswa na habari hii atume mchango wake kupitia namba 0753308525 ambayo ni ya mumewe au aende kumuona Muhimbili.
Share:

KAJALA AKUNUSHA KUHUSU KUGOMBANA NA WEMA SEPETU

Kajala akiwa kajiachia katika pozi

Baada ya siku chache za magazeti ya udaku nchini kuripoti kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa karibu sana kati ya mwanadada Wema sepetu na Muigizaji mwenzake Kajala masanja, tuliamua kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa suala hili ili tusije kuipotosha jamii kwa habari za zisizo na ushahidi wowote.

Katika habari iliyoripotiwa na blogs na magazeti kadhaa ya udaku kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema kuwa chanzo ni vitendo vya mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala kwenye dili anzopata za kucheza filamu na hasahasa kumkosesha dili ya kwenda china kufanya filamu aliyoalikwa na watanzania waishio nchini humo.

Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta hewani wasanii hawa ili tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada Kajala alikuwa wa kwanza kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo na kuwashangaa wanaoziandika wanazipata wapi.

“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala

Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema
“Wolper nimekutana naye kwenye party ndo tukaamua kupiga picha, au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu mwingine zaidi ya wema? Wolper ni rafiki yangu” Alisisitiza Kajala

Tulipojaribu kumtafuta wema simu yake ilikuwa haipokelewi na baadaye ilipokelewa na alisema yuko location anatengeneza filamu na mwigizaji Rado hivyo tumtafute baadaye.

Share:

Sunday, 23 June 2013

RIHANNA AMPIGA SHABIKI WAKE NA KIPAZA SAUTA BAADA YA SHABAKI HUYO KUMKERA...!!!

Rihana akiwa katika pozi

MWIMBAJI nyota wa muziki wa R&B, Robyn Rihanna Fenty, anayefahamika zaidi kwa jina la Rihanna, amenaswa na kamera akimpiga shabiki ‘mic’ usoni alipokuwa akifanya shoo huko Birmingham, Uingereza Jumatatu iliyopita.

Rihanna alifanya tukio hilo la kushtua alipojichanganya kwenye umati wa mashabiki, huku akiimba kwenye shoo hiyo ambayo ni sehemu ya ziara yake ya dunia inayojulikana kama ‘Diamond World Tour’ akiitangaza albamu yake ya saba ya ‘Unapologetic’ iliyotoka mwaka jana.

Ilidaiwa kuwa Rihanna mwenye umri wa miaka 25 alishindwa kudhibiti hasira zake baada ya shabiki huyo asiyefahamika kumng’ang’ania mkono wake.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliandika kwenye ukurusa wake wa Twitter: "Rihanna amempiga mtu mmoja na mic yake katika ajali haha oops."

Na Rihanna alijibu akisema kuwa alikusudia kumpiga shabiki huyo kwa sababu alikuwa akimzuia.

Share:

ASKOFU AITAKA SERIKALI KUWABANA WASIOTAKA NCHI ITAWALIKE.

RAIS Jakaya Kiwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na dini wakati alipohudhuria sherehe za miaka 25 ya Askofu wa jimbo kuu la Morogoro Telesphol Mkude wa pili kulia kwa rais katika viwanja vya shule ya ST Peter mkoani Morogoro jana.


SIKU chache baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutaka Serikali iachwe ifanye kazi yake katika kudhibiti vurugu zinazoibuka kila kukicha, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude naye ameitaka Serikali kuwadhibiti wote wasiotaka nchi itawalike.Askofu huyo amesema kuonya pekee hakusaidii, bali inawajibu wa kuwachukulia hatua kali ili kukomesha vitendo vinavyotishia amani nchini.Askofu Mkude aliyasema hayo jana wakati wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 ya uaskofu wake kwenye viwanja vya Seminari ya Mtakatifu Petro mjini hapa ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria.

Katika maadhimisho hayo, maaskofu zaidi ya 35 wakiwemo wa Majimbo Makuu wa ndani na nje ya nchi walihudhuria.

Aidha walikuwapo mapadri, watawa, waamini na mamia ya wananchi wa mikoa ya jirani, sambamba na viongozi wa Serikali na vyama vya siasa wakiwemo wa chama tawala, CCM.

Pamoja na ushauri wake, Askofu Mkude pia alimshukuru Rais kuweza kushiriki katika maadhimisho hayo, huku alirudia kumwomba yeye pamoja na Serikali yake kusimamia suala zima la amani ya Tanzania.

Askofu Mkude alisema Serikali inao wajibu kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa wakati wote na kuchukua hatua za haraka za kukutana na viongozi wa dini pale panapotokea kutoelewana katika imani zao ili kufikia mwafaka utakaodumisha amani ya Tanzania.

“Suala hili la kuchinja ...linaweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa viongozi wa dini na Serikali kukutana na kuliweka sawa...mbona hatugombani kwenye kuzika, makaburi ...hili la kuchinja kwanini linakuzwa zaidi wakati huu , ambako huku nyuma halikuweza kuwepo ...” alihoji Askofu Mkude mbele ya Rais.

Naye Rais Kikwete, akizungumza, aliwataka viongozi wa madhehebu ya dini nchini kuendelea kuhubiri amani, upendo, utulivu na mshikamano ili kujenga misingi imara ya maelewano yaliyodumu kwa miaka mingi miongoni mwa Watanzania.

Pamoja na kuomba viongozi wa dini kuhubiri amani, Rais Kikwete alisema Serikali itaendelea kushirikiana na Madhehebu ya dini katika kuleta maendeleo ya wananchi ili kuinua hali zao za kimaisha.

Mbali na hayo Rais Kikwete pia alisema viongozi wa madhehebu ya dini wanayo nafasi kubwa na ya kipekee ya kuwafundisha vijana kuwa Wacha-Mungu na raia wema wa nchi yao.

Katika hotuba yake pia alimpongeza Askofu Mkude kwa kutimiza miaka 25 ya uaskofu na kusema yeye pia ni miongoni mwa wakazi wa Parokia ya Lugoba, Wilaya ya Bagamoyo ambayo ni sehemu ya Jimbo la Kanisa Katoliki la Morogoro.

Rais pia alisema Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro limetoa fursa kwa maelfu ya vijana kupata elimu kwa manufaa yao sambamba na kuanzisha vituo vya afya ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa Serikali za kupunguza vifo vya watoto na akinamama wajawazito.

Kwa upande wake, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, aliwataka viongozi wa Kanisa hilo, wanapobanwa na hali ngumu ya kutukanwa na watu wengine, jukumu lao ni kumkimbilia Yesu Kristo huku wakiendelea kuhubiri upendo na amani.

“Sisi Viongozi wa Kanisa letu akiwemo Askofu Mkude tunapokumbana na hali ya ugumu wa kutukanwa na watu wengine ni vyema kuwa karibu na Yesu ili tuache mahangaiko na badala yake tuhubiri amani na upendo miongoni mwa waamini na jamii nzima,“ alisema Mwadhama Kardinali Pengo.

Hata hivyo alimtaka Askofu Mkude kutumia nafasi ya Jubilei hiyo si tu kumshukuru Mungu kwa kutekeleza mema pia kumwomba radhi Mungu kwa yale ambayo hakuweza kuyatekeleza na kuwataka waamini wa Jimbo hilo kuendelea kumpatia ushirikiano katika majukumu yake.

Naye Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu, Tarcisius Ngalalekumtwa ambaye ni Askofu wa Jimbo la Iringa na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la Songea, alisema upendo ndiyo jambo kuu katika kusukuma gurudumu la kuwatumikia wananchi na waumini wa Kanisa hilo.

Hivyo aliwataka Maaskofu na waamini wengine pamoja na wananchi kuendelea kumwombea Askofu Mkude aweze kutimiza majukumu yale pamoja na Taifa kwa ujumla.

Wakati huo huo Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, limetoa zawadi ya fedha Sh milioni 25 pamoja na kununua matairi matano na kumkabidhi Askofu Mkude kwa kutimiza miaka 25 ya uaskofu.
Makamu wa Askofu wa Jimbo hilo, Padre Patrick Kung’alo, alibainisha hayo wakati akisoma risala ya Jimbo hilo mbele ya wageni waalikwa akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa Makamu huyo wa Askofu pia Umoja wa Mapadri wakati wa maadhimisho hayo ya Jubilee umezindua usajili wa Bima ya Afya ambapo katika hatua ya awali umetoa kiasi cha Sh 7,890,000 kwa ajili ya kuwalipia mapadre 23 kwa kadi ya kijani.

Akizungumzia mafanikio mengine ya kimaendeleo chini ya Askofu Mkude ndani ya kipindi cha miaka 25 kati ya hiyo 20 akitumika Jimbo la Morogoro na mitano Jimbo la Tanga, alisema amewezesha kujengwa kwa sekondari 11 za Kanisa , Shule za Msingi 12, shule sita za ufundi pamoja na shule 25 za awali.

Makamu wa Askofu huyo alitaja mafanikio mengine katika kipindi hicho ni kusomesha mapadri wapya 54, uanzishwaji wa Kituo cha Redio Ukweli, mashirika 27 ya kuhudumia watawa wa Kanisa hilo wa Jimbo la Morogoro.

Padri Kung’alo, alitaja mafanikio mengine ni upandishwaji wa hadhi ya Kituo cha Afya cha Mikumi cha Kanisa hilo kuwa Hospitali kamili, ujenzi wa vituo vitano vya afya, zahanati 10 na kuwezesha kupandishwa hadhi Hospitali ya Bwagala kuwa Hospitali Teule ya Rufaa.

Hata hivyo alisema, Askofu Mkude aliwezesha kuanzishwa kwa kituo cha kuwatunza watoto wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo ili kuwezesha kundi hilo kupata huduma muhimu za kijamii ambazo wanakuwa hawazipati kama elimu na afya.

Share:

Saturday, 22 June 2013

Watu 6 wauawa Kaskazini mwa Kenya

Watu sita wameuawa kufuatia mapigano mapya ya kiukoo katika kuanti za Mandera na Wajir Kaskazini mwa Kenya.
Ramani ya Kenya

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, watu wanne waliuawa, wakati wapiganaji kutoka kwa jamii ya Degodia waliposhambulia lori moja ya mizigo.

Gavana wa Jimbo wa Mandera Ali Roba, watu hao waliuawa hiyo jana na emeongeza kusema kuwa wamepokea ripoti kuwa watu hao waliuawa kinyama.

Mandera County governor Ali Roba said the people were killed during the broad daylight attack on Friday.

Roba amesema watu waliokuwa wakisafiri kwa lori hilo waliviziwa katika eneo la Eldas ambapo wanne waliuawa papo hapo na wengine wanne walifanikiwa kutoroka.

Baada ya kuwauawa watu wao, wavamizi hao waliteketeza lori hilo baada ya kupora mali yote.

Shirika la Msalaba Mwekundi nchini Kenya, waliojeruhiwa wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya wilaya ya Mandera.

Katika tukio lingine watu wengine wawili wameuawa katika Kaunti ya Wajir.

Gavana wa eneo hilo amethibitisha tukio hilo na kutoa wito kwa raia wa eneo hilo kudumisha amani.

Mashambulio katika eneo la Kaskazini mwa Kenya yamekuwa yakiongezeka katika miezi ya hivi karibuni, tangu serikali ya Kenya ilipoamua kutuma wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wapiganaji wa Al Shabaab.

Tarehe kumi na moja mwezi huu, watu sita waliuwa kufuatia mapigano hayo ya kiukoo katika jimbo la Mandera

Share:

Gari lililomsafirisha Mandela liliharibika

Gari la wagongwa lililokuwa likimsafirisha hospitalini rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela wiki mbili zilizopita, liliharibika likiwa njiani kwenda hospitalini.
Mandela akiwa na Mkewe Graca

Msemaji wa rais wa Afrika Kusini Mac Maharaj, amethibitisha kuwa gari hilo lilikumba na matatizo na kuwa ilibidi rais huyo wa zamani kuhamishwa hadi gari lingine.

Hata hivyo Bwana Maharaj, amesema tukio hilo halikuwa na tishio lolote kwa afya ya Bwana Mandela, kwa sababu alikuwa na madaktari wa kutosha.

Shirika la habari la Marekani CBS limenukuu vyanzo kadhaa vikidai kuwa Mandela alisalia katika eneo hilo kwa zaidi ya dakika arubaini kabla ya usaidizi kufika.

Shirika hilo la CBS limesema kuwa wakati Bwana Mandela alipokuwa akihamishwa hadi gari lingine viwango vya joto vilikuwa chini sana.
Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alikuwa akisafirishwa kutoka hospitali moja mjini Johannesburg hadi Pretoria, wakati wa tukio hilo lililotokea tarehe nane Juni mwaka huu.

Mandela alilazwa hospitalini huku hali yake ikiwa mbaya kutokana na maambukizi ya mapafu ya mara kwa mara na tangu wakati huo amekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Hii ni mara ya tatu kwa Bwana Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.

Share:

ANGALIA PICHA ZA BOB JUNIOR AKIPEWA KICHAPO LOCATION...!!!

Bob Junior ameshare picha hizi kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika: Kwa Dizaini hii lazima nirudi kwetu k…Aaaaah Maisha Haya Ya Bongo?,,,,COMING SOON Huu Mzigo…1 Love.


Bob Junior akiwa location kushoot video yake mpya, duuuuuuh...!!! kaaazi kweli kwelii

Share:

HII NI KAULI YA FREEMAN MBOWE ALIPOJISALIMISHA POLISI LEO

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na mandeleo Mh. Freeman Mbowe na mbunge wa jimbo la Arusha Godbless Lema wamejisalimisha kwa jeshi la polisi huku wakiendelea kusisitiza kuwa ushahidi walio nao hawatauwasilisha kwa jeshi la polisi mpaka pale rais Jakaya Kikwete atakapounda tume huru ya majaji ya uchunguzi

Share:

MBUNGE WA MBEYA AMTUKANA WAZIRI MKUU NA KUDAI KUWA "TANZANIA HAIJAWAHI KUWA NA WAZIRI MKUU MPUMBAVU KAMA ....."

Katika hali yakushangaza , mbunge wa mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, mh. SUGU ameporomosha tusi zito kwa waziri mkuu wa tanzania ( mh. PINDA ) akidai kuwa Tanzania haijawahi kuwa na waziri mkuu mpumbavu kama yeye.....

Tusi la Sugu limekuja baada ya waziri mkuu kuwaruhusu rasimi polisi kutumia nguvu ya ziada kuwadhibiti wananchi kwa kuwashushia kichapo ili wazitii sheria.....

Hili ndo tusi la mbuge wa mbeya kwa waziri mkuu...


Share:

MEYA AZIMIA BAADA YA KUPIGWA NA POLISI

Meya wa Mji Mkuu wa Kampala nchini Uganda akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa tuhumza za kusababisha vurugu.

Kampala, Uganda. Watu wawili wameuawa kwa risasi nchini Uganda juzi, wakiwa katika mkusanyiko kwenye eneo la soko la Kisekka.

Meya wa mji mkuu wa Uganda, Kampala, Erias Lukwago, pia alizirai baada ya kupigwa na polisi hao waliofyatua risasi za mipira kuutawanya umati wa wafuasi wake.

Akiwa kitandani, Meya huyo amesema baada ya kupata kipigo hicho alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitalini.

“Bomu ambalo lilinifanya nipoteze fahamu lilirushwa katika gari langu na kuingia ndani,” amesema.

Meya huyo ni mpinzani wa rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, alieleza kwamba maofisa wa polisi walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake wakimtuhumu kwa kuchochea ghasia.

Katika tukio hilo, imedaiwa kwamba mtu mmoja anadaiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kukamatwa wakati wa ghasia hizo.

Hata hivyo, polisi wamekanusha madai ya kumpiga meya huyo, ambaye pia ni mkosoaji mkubwa wa Rais Museveni.

Upinzani umesema kuwa serikali inajaribu kukandamiza kilio cha mageuzi nchini humo.

Katika tukio lingine, kiongozi wa upinzani, Kizza Besigye alikamatwa kwa kuandaa mkutano ambao polisi hawakuuidhinisha.

Lukwago, juzi alikuwa anaelekea kwenye jopo maalumu kwa mara ya kwanza, ambako huenda ikamwondolea wadhifa wake kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi.


Polisi walizingira nyumba yake na kisha kumpeleka ambako jopo lilikuwa linaendesha vikao vyake.

“Walinipiga kifuani na kudai kuwa nachochea ghasia, walinirarulia nguzo zangu na kunitesa, nilijaribu kuwaambia waniache lakini sikufanikiwa,’’ amesema Lukwago.

Share:

ALICHOKIANDIKA ZITTO KABWE KUHUSU KAULI YA PINDA KURUHUSU POLISI KUPIGA WANANCHI

Baada ya mh.waziri mkuu mizengo pinda kutoa ruhurusa kwa polisi kupiga wananchi..Mh mbunge zitto kabwe nae atoa lake juu ya mh.waziri mkuu…Kupiitia tweet yake Zitto alisema “Viongozi wa kisiasa lazima wajue kuwka akiba ya maneno yao .kuropoka hovyo hovyo wakati kama huu wenye taharuki ni hatarii sana”..Aliongezea “Ni lazima viongozi wawajibishwe kwa maneno wanayotamka.Mh. Pinda anahamasisha ukiukwaji wa katiba na sheria Asipowajibishwa.”

 HIZI NDIZO TWEET ZA MH.ZITTO KABWE


Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive