Saturday, 6 July 2013

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA JOYCE KIRIA BAADA YA KUSHAULIWA AMWAMBIE MUMEWE AACHANE NA SIASA

My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.

imeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama).


Hubby Henry Kilewo kikazi zaidi.

Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha????

My family, Hubby Henry With Our Boys, Lincon na Linston.

Fans Wangu wote naamini mtakuwa mmenielewa na mtaendelea kuwa nami all the way, Msimamo wangu ni huu, Nitasimama upande wake na kuendelea kumsupport mume wangu Henry, SIASA ni kitu anachokipenda SIWEZI KUMWAMBIA AACHE


Share:

DIAMOND ASABABISHA KIFO CHA MTOTO MWANANYAMALA...!!!

Vilio na simanzi vilitanda Jumatano iliyopita Mwananyamala Kisiwani, jijini Dar kufuatia mtoto wa mwaka mmoja, Rahim Rajab kufariki dunia kwa kuangukiwa na watu watatu, akiwemo baba yake mzazi, Rajab Said..

Tukio la watu hao kumwangukia mtoto huyo lilitokea Jumatatu iliyopita na lilisababishwa na ugomvi mkubwa wa CD yenye nyimbo za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ulioibuka ndani ya chumba cha kulala kati ya mama wa marehemu na mpangaji mwenzake aitwaye Aisha.

Akizungumza kwa machungu kuelezea tukio hilo, mama mzazi wa marehemu Rahim, Habiba Ally alikiri kuwa kisa cha kifo cha mwanaye ni CD tu.Akasema:

" Kwa kweli hakuna kingine zaidi ya CD, naamini hivyo kwa kuwa mimi sikuwa na ugomvi wowote na Aisha. Tulikuwa tunaishi kawaida tu ukiacha mikwaruzo ya hapa na pale.”

Akaongeza: Jumamosi iliyopita, Aisha alikuja ndani kwangu na CD zake tatu, ya Diamond, Kingwendu na ya Coast Modern Taarab. Alipomaliza kuangalia aliziacha, akaondoka zake.

“Jumapili mimi nikaenda nazo kwa mama zote tatu kwa ajili ya kuziangalia, tulipomaliza na mimi niliziacha huko.

“Jumatatu usiku Aisha akaja kunidai, nikamwambia zipo kwa mama. Kwa kuwa anapajua anapoishi mama, si mbali akaenda kuzichukua zote tatu.

Ajabu aliporudi tu, akaja tena kwangu na kusema hajapewa CD ya Diamond kitu ambacho si kweli na ndipo ulipozuka ugomvi wote huo hadi kusababisha kifo cha mwanangu.”

Akizungumza msibani juzi, bibi wa marehemu, Jamima Hassan alisema siku ya tukio alipigiwa simu na mkwe wake (baba wa marehemu) akamwambia kuna ugomvi nyumbani kwake unaohusu CD kati ya mkewe na mpangaji mwenzake ambapo bibi huyo aliamua kwenda kutatua ugomvi huo.

“Niliondoka muda huohuo kwani huyo Aisha alitoka kwangu kuchukua CD zake muda mfupi tu, sasa nilijiuliza ni CD gani wanazogombania?

“Nilipofika nilikuta ugomvi umepamba moto, baba wa mtoto na mume wa Aisha aitwaye Shaban Sangali walikuwa wameungana kumtoa nje ya chumba Aisha bila mafanikio.

“Wakati naingia, Aisha alikuwa akitukana matusi mazito na tulipojitahidi kumtoa nje alitusukuma kwa nguvu. Ndipo yeye, mume wake na baba wa mtoto waliwaangukia watoto waliokuwa wamelala kitandani,” alisema bibi huyo.

Akaendelea: Tulipowaangalia watoto ambao ni mapacha, hali zao zilikuwa mbaya, tukaamua kwenda kwa mjumbe wa mtaa kuripoti, akatupa barua, tukaenda Kituo cha Polisi Mwinyijuma, pale wakatupa PF3 ya kuwapeleka Hospitali ya Mwananyamala ambako walilazwa kwa matibabu.

Bibi huyo alisema siku iliyofuata, Rahim alifariki dunia, ikabidi waende Polisi Oysterbay ambapo walifungua shitaka lenye faili kwa kumbukumbu No. OB/RB/1150/2013 MAUAJI.

Watuhumiwa katika RB hiyo ni Aisha na mumewe, Sangali ambao walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

Majirani waliozungumza na mwandishi wetu walisema wakati ugomvi kati ya Aisha na Habiba unatookea, mume wa Habiba alikuwa anarudi kutoka kazini, akakutana na kimbembe hicho.

Walisema aliingilia kati kuamua bila mafanikio. Wakati huo mume wa Aisha alikuwa chumbani kwake na amefungulia muziki wa redio kwa sauti ya juu hivyo hakujua nini kinaendelea kwenye chumba cha mpangaji mwenzake.

Ikaelezwa kuwa, kuna watu walikwenda kumgongea na kumwambia mkewe anapigwa na mume wa Habiba kwa kushirikiana na mkewe.

Ilibidi mwanaume huyo atoke mbio hadi chumbani kwenye ugomvi ambako alikuta baba wa marehemu akijitahidi kuwaamulia wawili hao bila mafanikio.

Habari zinasema mwanaume huyo aliingilia kati kuongeza nguvu lakini katika hali ya kuwalemea, Aisha aliwasukuma wote na kisha wao kuwaangukia watoto hao mapacha waliokuwa wamelala kwenye kitanda kimoja.

Katika hali ya kusikitisha, marehemu amemuacha pacha mwenzake aitwaye Rahima Rajab ambaye ni kulwa.

Wengi wanaamini kuwa maisha ya Rahima yangekuwa ya furaha zaidi kama Rahimu angekuwepo na kwamba itamsononesha sana akikua na kusikia mwenzake alifariki dunia kwa ugomvi wa mama yake na mpangaji mwenzao kisa ni CD ya nyimbo za mwanamuziki.

Share:

DOWNLOAD BaghdaD ft Ney & Chidi Benz - Waambie Nipo



Share:

Rais wa mpito aapishwa nchini Misri

Jaji mkuu wa mahakama ya juu zaidi ya kikatiba ameapishwa nchini Misri kuwa rais wa muda baada ya jeshi kumng'oa mamlakani rais aliyechaguliwa na raia kwa njia ya kidemokrasia na kushinda kwa wingi wa kura, Mohammed Morsi.
Viongozi duniani wamepokea kwa tahadhari matukio yanayojiri huko Misri. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amewaambia waandishi kwamba anaangalia kwa umakini hatua iliyochukuliwa na jeshi la Misri.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza , William Hague, amesema Uingereza haiungi mkono uvamizi huo wa kijeshi lakini haina budi kuitambua hatua hiyo na kusogea mbele. Hata hivyo alikataa kulishutumu jeshi kwa kumpindua Morsi akisema ni uvamizi ulioungwa mkono na watu wengi.
Mfalme Abdalla wa Saudia ametuma ujumbe wa hongera kwa kaimu rais wa Misri akisema kwamba uteuzi wake unajiri katika wakati muhimu.

Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.

Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.

Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.

Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.

Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.

Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive