Saturday, 18 April 2015

Wanafunzi waliopigwa na radi kufuatia mvua iliyonyesha mkoa wa kigoma wazikwa.

Mkuu wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya  amewaongoza mamia ya wakazi wa manispaa ya kigoma ujiji  kuaga miili ya watu wanane wakiwemo wanafunzi  sita wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya kibirizi mjini kigoma walio fariki dunia jana baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua iliyonyesha kwa takriban masaa matatu.
Majonzi yalitawala shughuli hiyo  hasa baada ya miili hiyo kupokelewa katika viwanja  vya  shule ya msingi kibirizi kabla ya ndugu kukabidhiwa tayari kwa maziko huku mwili wa Mwalim Elieza Mbwambo ukisafirishwa kwenda moshi kwa maziko .
 
 Akitoa salam za rambirambi mkuu wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewataka wafiwa na wananchi kuchukulia  tatizo hilo kama ni tukio la ajali ya kawaida na kwamba msiba huo ni mzito.
 
Kwa upande wao viongozi wa dini Shekh Moshi Guoguo kutoka Bakwata na mchungaji Emmanuel Mtoi wa kanisa la KKKT wakitoa mawaidha katika msiba huo, wamewataka waumini wa dini mbalimbali kujiandaa kwa kuwa kila mwanadamu ataonja mauti  kwa wakati wake na kwamba imani za kishirikina zisihusishwe katika msiba huo.
Share:

Chama cha ACT chaitaka serekali kutoa taarifa za uchunguzi wa ajali zinazo tokea mara kwa mara.

li kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na wananchi kupata ulemavu,chama cha ACT wazalendo kimeitaka serekali kutoa taarifa ya tume ya uchunguzi wa ajali za barabarani zilizo fanyiwa utafiti ili kuweza kutafuta namna yakutatua matatizo ya ajali za mara kwa mara.
 akiwahutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Singida na viunga vyake  kwenye mkutano wa kunadi chama cha ACT kiongozi mkuu wa chama hicho Bwana. Zitto Kabwe ,amesema aliyekuwa waziri wa uchukuzi Dk Harsson Mwakyembe aliunda tume ya uchunguzi wa ajali na mpaka sasa majibu hayaja tolewa,jambo ambalo limekuwa likisababisha ajali kuendelea kutokea na kwa kipindi cha mwenzi Mach na April mwaka huu zaidi wa watu mianane wamesha poteza maisha kwa ajili ya ajali.
Katika hatua nyingine Bwana. Zitto Kabwe ameitaka serekali kuhakikisha inawabana wamiliki wa mabasi kote nchini  ,watoe  mikataba ya kazi   kwa madereva wao ili waweze kujulikana, kwa kufanya hivyo kuta punguza ajali ambazo siyo za msingi.
Awali mwenye kiti wa chama cha ACT Bi.Anna Mghwira na kada wa chama hicho Bwana  Selemani Msindi maarufu kwa jina la Afande Sele wamesema huduma nyingi  hasa za afya wakati wa zamani zilikuwa zikipatikana kulingana na uwezo wa serikali wakati ule, na kwasasa nchi imekuwa na utajiri mwingi wa madini ,kilimo na biashara,lakini cha kushangaza fursa hizo zimekuwa zikitumiwa na baadhi ya watu na kuwaacha wananchi wengi wakiwa masikini.
Share:

Zaidi ya watu miamoja wahofiwa kufa baada ya kuangukiwa na kifusi katika kijiji cha Karore wilayani Kahama.

Watu zaidi ya mia moja wanahofiwa kufa baada ya kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya dhahabu ya wachimbaji wadogo wadogo ya kalole yaliyoko katika kata ya msalala wilayani kahama mkoani shinyanga na inasemekana wachimbaji hao walivamia mgodi baada ya muda wa kazi hali iliyosababisha mashimo manane ya mgodi huo kutobozana na hatimaye nguzo kuvunjika na kisha kifusi kuwaangukia.
ITV ilifika katika eneo hilo na kukuta zoezi la kutambua maiti linaendelea na wakaguzi wakiendelea na zoezi la kukagua mashimo yaliyokuwa wazi huku baadhi ya wachimbaji walionusurika katika tukio hilo wakiulalamikia ulinzi wa machimbo hayo kuwa ndio chanzo cha tukio hilo kwakuwa tukio lilitokea mapema saa kumi na mbili baada ya saa za kazi lakini inashangaza taarifa kupatikana saa sita za usiku na wamedai kuwa idadi ya watu waliofukiwa na kifusi ni zaidi ya mia na hamsini lakini serikali imeridhika na idadi ya watu kumi na tisa ambao wameshaopolewa hadi wakati huu.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga Justus Kamugisha amesema watu hao walivamia mgodi baada ya muda wa kazi kuisha na kulingana na wingi wao mgodi ulielemewa na kusababisha nguzo kuvunjika hali iliyosababisha kifusi kuwaangukia lakini kwa jitihada za jeshi la polisi tayari wameshaopolewa watu kumi na tisa na kumi na mbili kati yao wameshatambuliwa na tayari wameshachukuliwa na ndugu zao tayari kwa maziko.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kahama Bw. Benson Mwampesya amesema kwakuwa imeonekana idadi ya vijana walioangukiwa na kifusi ni wengi zaidi ya hao walioopolewa serikali imeamua kuomba wataalam na mitambo ya kuchimba eneo hilo kutoka katika mgodi wa bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya acacia ili kuharakisha zoezi la kuhakiki kuwa hakuna maiti zingine zilizonaswa katika mashimo ya mgodi huo.
Share:

Ghala lenye dawa zilizopigwa marufuku na zilizokwisha muda wake wa matumizi limekamatwa Mwanza

 
 Maofisa zaidi ya 30 kutoka mamlaka ya chakula na dawa na baraza la Famasi Tanzania
wamekamata ghala lenye dawa za serikali,zilizopigwa marufuku na zilizokwisha muda wake wa matumizi zenye thamani ya shilingi milioni 97 zikiwa zinamilikiwa na mfanyabiashara wa jijini mwanza CHARLES MBUSIRO kinyume cha sheria.
Ghala hilo lililopo eneo la ilemela jijini mwanza limekutwa likiwa limesheheni zaidi ya 120 za dawa ambazo ni sawa na tani 42 zikiwemo dawa za serikali za Kenya na Uganda, dawa za misaada, dawa zilizopigwa marufuku nchini kama vile klorokwini ya sindano, amodiaquine na gripe water -dawa nyingine zilizokutwa ndani ya ghala hilo na kwenye duka lake la dawa lililopo Natta barabara ya nyerere ni pamoja na ambazo hazijasajiliwa na TFDA na azisizoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya dawa.
 
Meneja wa usalama wa dawa wa TFDA Kissa Mwamwitwa ndiye aliyeongoza zoezi hilo liliendeshwa chini ya usimamizi mkali wa askari polisi wenye silaha za moto.
Baadhi ya maofisa wanaotekeleza operesheni hiyo, wakiwemo wanasheria kutoka TFDA na baraza la famasi tanzania pamoja na meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Florent Kyombo wakizungumzia tukio hilo wamesema taratibu za kisheria zinafanyika ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa.
 
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kahasa ilemela Richard Peter alikuwa shuhuda wakati maofisa hao wa TFDA, baraza la famasi tanzania na askari polisi walipokuwa wakitekeleza zoezi hilo kwenye ghala la dawa ambalo linasemekana bado halijasajiliwa na TFDA huku mmliki wake charles mbusiro akitoroka kwa kuruka ukuta na kutokomea kusikojulikana.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive