Sunday, 2 June 2013

Maelfu waandamana Addis Ababa

                                           Maelfu ya waandamanaji wameandamana katika barabara za mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakidai waandishi wa habari na wanaharakati walioko kizuizini wafunguliwe.
                              Waandishi wa habari wanasema ni nadra kuonesha upinzani wa namna hiyo kwa chama tawala ambacho kinadhibiti shughuli za jamii sawasawa.

Makundi ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema serikali imetumia sheria za kupambana na ugaidi ili kuwafunga waandishi wa habari.

Waandamanaji- wengi kutoka upinzani - walipiga kelele kudai uhuru na haki.

Haya ni maandamano ya kwanza tangu mwaka wa 2005 ambapo mamia ya waandamanaji waliuliwa katika ghasia zilizofuatia uchaguzi.

















Share:

DAKTARI AKIRI NGWEA KAFA KWA KUNYWESHWA SUMU, ADAI KUWA ALITOKWA NA DAMU NYINGI SANA PUANI WAKATI AKIKATA ROHO.:

                                     KIFO cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika.
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo) alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa kwenye Mochwari ya Hillbrow.
                                      M 2 THE P Akiwa hospitali hoi hajitambui
Mbongo huyo alisema alifanikiwa kuutazama mwili wa marehemu Ngwea ambapo ulionesha kuwa wakati wa kukata roho damu nyingi zilimtoka kupitia puani na mdomoni kiasi cha kuwashangaza wauguzi.

NI SUMU
Alisema muuguzi mmoja aliyekuwa akimtibu mshirika wa marehemu, Mgaza Pembe a.k.a M2 The P aliyenusurika, alimwambia wawili hao walionekana kuingiwa na kitu cha hatari na kibaya sana mwilini jambo lililowashtua hata madaktari wenyewe.


Alisema muuguzi huyo alimweleza kuwa kitu walichokula au kulishwa kiliwadhuru sana ndani ya miili yao na kusababisha mishipa ya damu kwa Mangwea kupasuka hovyo kwa kuwa moyo ulizidiwa na presha ya msukumo wa damu.
Mtanzania huyo alidai kuwa hata kama kweli wawili hao walichanganya vileo kama watu wanavyodai, basi ule mchanganyiko ndiyo uliotengeneza sumu mwilini akisisitiza kuwa hilo halina shaka kwa mujibu wa muuguzi huyo.
“Unajua kuna watu wanapenda kuchanganya pombe kali kwa hiyo kuna wanaodai wawili hao walichanganya ‘unga’, bangi na pombe kali.
Mchanganyiko huo tu wenyewe ni sumu tosha mwilini kwa binadamu yeyote yule.
“Wataalam wanajua, ukichanganya pombe kali unapata upungufu wa oksijeni katika damu hivyo unaupa moyo kazi ya ziada ya ‘kupampu’ damu kwa kuwa presha inakuwa kubwa. Kwa hiyo kinachotokea ni kupasuka kwa mishipa mikubwa ya damu, ndiyo maana damu zilitoka puani na kinywani kwa wingi.
“Kwa kuchanganya vileo hivyo unatengeneza sumu ambayo husababisha shambulio kubwa la damu na mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi.
“Sasa usipowahishwa hospitali ili kuchomwa sindano ya limao, kifo kinakuwa njenje.
“Kwa vyovyote walikula au walilishwa sumu, daktari anasema mwili wa Ngwea umeharibika sana kwa ndani.
“Kile siyo kipigo, hakuna jeraha lolote la kupigwa, ile ni sumu,” kilidai chanzo hicho cha kuaminika.

SAA CHACHE KABLA YA KIFO
Habari za kina kutoka kwa mmoja wa watu waliokuwa nao kabla ya kukutwa na tukio hilo zilieleza kwamba kabla ya kwenda kulala, Ngwea na mwenzake, walikutana na baadhi ya Watanzania waishio Sauzi na kupiga stori kwenye baa moja huku wakitaja majina ya wasanii wa Bongo Fleva waliotangulia mbele ya haki.
Ilidaiwa kuwa kila jina la msanii marehemu lilipotajwa Ngwea alikuwa akitamka ‘OMG’ (Ooh! My God) yaani Ooh! Mungu Wangu, bila kujua kitakachomkuta baadaye.

MADAI MENGINE, MAISHA YA SAUZI


Kuna madai mengine kwamba baadhi ya Wabongo waishio Sauzi huwa wana maisha ya kutegana hasa wakijua Mtanzania mwenzao kaenda kule akiwa na ‘mkwanja’ mrefu.
“Tatizo lingine ni kwamba kama walifanyiziwa na mtu huo uwezekano ni mkubwa sana kwani huku jamaa wakikushtukia tu kuwa una mkwanja, kwanza wanakuwa karibu sana na wewe ‘then’ ukikaa vibaya lazima wakutoe uhai.
“Inawezekana akina Ngwea walifanyiziwa kwa kulishwa sumu kwa sababu walikuwa wameshapiga mkwanja tayari kwa kurejea Bongo,” alisema Mbongo huyo.

MCHUNGAJI ALIKIONA KIFO CHAKE MAPEMA!
Mwezi Machi mwaka huu, kupitia gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa la Machi 22-28, 2013 liliandika ukurasa wa mbele habari yenye kichwa; ‘MASTAA WAWILI KUFA MWAKA HUU’ ambapo mchungaji maarufu jijini Dar alisema mwaka 2013 ameona katika maono yake vifo vya wasanii wawili wa Bongo.
Katika habari hiyo, mchungaji huyo alitahadharisha mapema kuwa wasanii wamrudie Mungu kwani upepo siyo mzuri kwao.
Mchungaji huyo alieleza: “Mwaka huu ulipoanza, Januari 2, Sajuki (Juma Kilowoko) aliaga dunia katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa lakini nimepewa maono na Mungu kwamba wasanii wengine wawili watakufa mwaka huu.
“Katika hayo maono niliona wasanii wenyewe, mmoja wa kike, mwingine wa kiume. Wa kike ni msanii wa filamu, wa kiume anaimba hizi nyimbo za kisasa za Bongo Fleva.
“Huyo wa Bongo Fleva siyo mkongwe sana kama wale waanzilishi wa fani hiyo lakini anajulikana sana na mashabiki wengi. Nyimbo zake zinajulikana pia.
“Huyu wa kike yeye ni mkongwe kidogo, halafu ni mweusi, zamani aliwahi kuwika sana lakini kwa siku za hivi karibuni amepoapoa.”

MANENO YAKE YALIJAA UTABIRI
Watu wa karibu waliokuwa wakichati na Ngwea kupitia mitandao ya kijamii walisema siku za mwisho wa uhai wake, marehemu alipenda kutumia maneno yenye kumtaja Mungu, Yesu au viashiria vingine vinavyofanana na hivyo.

TURUDI KWENYE TUKIO
Habari zilieleza kuwa baada ya majibu ya kilichomuua Ngwea kujulikana, mwili wa staa huyo utaagwa kesho jijini Dar ambapo msiba upo kwa kaka yake Mbezi Beach na baadaye mwili utasafirishwa kwenda mkoani Morogoro eneo la Kihonda, nyumbani kwao.

NGWEA HAPA, BABA’AKE PALE
Habari kutoka msibani Morogoro zimeeleza kwamba marahemu Ngwea atazikwa jirani kabisa na kaburi alilozikwa marehemu baba yake, mzee Kenneth Mangwea. Huo ni ushauri wa familia yake.

HALI YA M2 THE P
Kwa upande wake, M2 The P, hadi gazeti linakwenda mitamboni alikuwa akiendelea na matibabu huko Sauzi huku hali yake ikisemekana inaendelea kuimarika.
Ngwea alizaliwa Novemba 16, 1982 huko mkoani Mbeya (asili yake ni Mkoa wa Ruvuma) akiwa mtoto wa mwisho katika familia yao. Hajaacha mke wala mtoto.
Share:

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA BUSHOKE AKIWA SOUTH AFRIKA KUHUSU KIFO CHA NGWAIR

Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa kuwa Mangwea alikuwa pamoja na mtu aitwaye M TO THE P ambaye naye yupo mahututi kwa sasa.
                     Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini Johannesburg nchini                                              Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi amefariki akiwa usingizini.
                               Akiongea na Clouds FM muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.

“Sijui hata huko alitumia nini,” amesema.

Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.

Hata hivyo amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi leo nchini.
Awali Tulizungumza na Bushoke anayeishi jijini Pretoria ambaye amesema alikuwa akutane naye leo jijini Johannesburg lakini alishangaa kutompata kwenye simu. Amesema baada ya kuwatafuta washkaji ambao ni wenyeji wake ndipo walipomuambia kuwa Ngwair amefariki.

“Unajua Ngwair ni mshkaji wangu sana yaani hata siamini kama amefariki aisee,” amesema Bushoke.

Bushoke amesema kesho amepanga kwenda Johannesburg kujionea mwenyewe.

Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na watu na makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Kilimanjaro Lager ‏

Umeondoka wakati bado tasnia ya muziki inakuhitaji. Pumzika kwa Amani Albert Mangwea “Cowwizy”.

Ndovu Special Malt

                               R.I.P Albert Mangweir! You will be missed by many Tanzanians.

Adam Nditi

                                 Yani siamini Mangwear amefariki dunia nini ilichomkuta #RIP #Mangwair #akaCowbama

Diva ‏

Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t believe this. I can’t tweet The RIP….. Whyyyyy?
Share:

DIAMOND ATOA SIRI YAKE NA MANGWAIR.

                                                                    DIAMOND
WAKATI watu mbalimbali maarufu nchini, hususan wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), wakiendelea kutoa historia ya mahusiano yao na aliyekuwa msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Albert Mangweair.
wea, msanii maarufu wa muziki nchini Nassib Abdul (Diamond Platnumz) amevunja ukimya na kutoa siri yake na marehemu Mangwea.


Akielezea hisia zake pamoja na mipango mingi aliyokuwa nayo kuhusu kufanya kazi ya muziki na marehemu katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Diamond alisema kwamba alijaribu kufanya kazi ya pamoja na msanii huyo lakini kwa bahati mbaya kazi zote zikaharibika.


"Kinacho niumiza ni jinsi tulivyo jaribu kutengeneza HIT bila mafanikio yaani siyo nilizo mshirikisha hata zile alizo nishirikisha na tuka amua kuplan kutengeneza nyingine akirudi kutoka Afrika Kusini, lakini haikuwezekana yani mungu alimpenda zaidi":alisema Platnumz.

Kila binadamu huwa na jambo lake muhimu ama siri ya mafanikio baina yake na mtu mwingine ambayo pengine si rahisi kuizungumzia hadharani ama wakati wowote, lakini inapotokea mmoja kati yao akifariki dunia anayebaki duniani hujikuta akitoa siri hiyo.

Hatua ya Binadamu kuamua kutoa siri yake na mwenzake wakati wa msiba wa mmoja wao inaweza ikawa na tafsiri nyingi lakini ukweli nikwamba huzuni na machungu ya kuondokewa na mtu muhimu kwake aliyekuwa akitarajia kufanya naye jambo flani muhimu ndiyo husababisha mtu huyo kutoa siri.R.I.P Mgwea.
Share:

Flora Mvungi KUFANYIWA KITCHEN PARTY LEO…

 Mwenyewe anasema kwamba role model wao na mchumba wake H Baba ni Kim Kardashian na Kanye West. Kila kitu ambacho Kim na Kanye wanafanya na wao wanafuata..mfano mdogo ni pale Kanye alinvyomvisha pete Kim K..H baba na yeye akamvisha pete Flora Mvungi. Baadaye Kim K akapata mimba na Florah akafuatia..lakini this time Florah na H baba wanajiandaa kufunga ndoa, upande wa pili wa Kim K na Kanye hatujaskia chochote.

Kitu kikubwa leo hii ni kwamba Florah Mvungi atafanyiwa Kitchen Party tayari kwa ajili ya kufunga ndoa na mchumba wake H baba. Bila shaka ndani ya muda mfupi watakuwa Mr and Mrs..

Share:

Vita vya Syria vyazidi kutapakaa Libnan

.Inaarifiwa mapigano hayo yalitokea mashariki mwa bonde la Bekaa katika mji wa Baalbek.

Jumamosi makombora na mizinga kadha ilirushwa dhidi ya eneo hilo na makombora zaidi yamepiga piya mitaa ya kusini mwa Beirut.

Wapiganaji wa Syria wamesema watafanya mashambulio ndani ya Libnan kulipiza wapiganaji wa Hezbollah kumsaidia kivita rais wa Syria, Bashar al Assad.
Share:

Michael Jackson's Advice Helped Judith Hill 'Sizzle' On 'The Voice'
















Even though she was eliminated Tuesday night, Hill tells MTV News she thinks Jackson would be 'very proud' of her.ichael Jackson in 2001
Photo: Kevin Mazur/WireImage


There are a lucky few who can boast having any contact with Michael Jackson, let alone receiving his priceless advice. And "The Voice" alum Judith Hill is one of them. Despite being eliminated on Tuesday night's show, Hill has become known for her connection to the late King of Pop, serving as his background singer and duet partner during his final "This Is It" tour.

The connection proved to be a "double-edged sword" for Hill on the competition series, receiving high praise from coaches and criticism from some viewers who felt she was "exploiting" Jackson's name.



"Yeah, a weird sort of criticism because I didn't know what it was," Hill says of the unexpected backlash.

The pressure of living up to the pedestal she was placed on took a toll on Hill, who broke down on camera a couple weeks ago when assigned to perform a tribute to her mentor. Reluctant at first, the soulful diva eventually found the experience to be cathartic.

"It was like a release, kind of, to be able to celebrate Michael — my time with him and everything," Hill revealed to MTV News.

After Hill's final performance on Monday night to will.i.am's "#thatPOWER," Levine refused to put her in the category of contestant, recognizing her as an "artist."

Her musical prowess was a forced to be reckoned with on the show, due in part to some invaluable advice she received from Jackson himself.

"Yeah, like sometimes he would say, 'Sometimes you have to let the moment sizzle,' " Hill said, fondly remembering the legend.

Although she will be featured in "20 Feet From Stardom," a musical documentary about the lives of backup singers, Hill is ready to move from the background to the foreground.

And Hill believes that if Jackson were alive, he would fully support her. "He was so, so kind and gracious, he would say, you know, 'It's your time to shine,' " she said. "He said that a lot. I think that he would be very proud of everything I've done so far."

"The Voice" continues its live rounds on Monday when the top 6 go head-to-head.




Share:

Kim Kardashian's Baby Shower: A Gift Guide for Baby Kimye


Kanye West and Kim Kardashian
Photo: Getty Images


Kim Kardashian certainly has a lot to look forward to on Sunday. The mother-to-be not only will reveal the sex of her baby with Kanye West on the season premiere of "Keeping Up with the Kardashians," she will also be celebrating her baby shower with all of her close friends and family.

So what could guests possibly be getting baby Kimye? To get an idea, MTV News caught up with Jessica Henry, manager at the high-end baby boutique Bel Bambini, where Kim was spotted shopping with her sisters back in March, and while she couldn't discuss what she checked out, she did offer some insight on what could fill up baby Kimye's nursery, whether it be a boy or girl.
 Now, if there is one thing we know for sure, it's that baby Kimye will be stylish. Kim has certainly pushed the boundaries when it comes to maternity clothes, wearing everything from sky-high Louboutin heels to figure-hugging Versace dresses, so when it comes to her bundle of joy, there is no doubt that the kid will be runway ready.

"If Kim and Kanye's baby is a girl, Junior Gautier dresses would be the perfect gift that are very in keeping with Kim's new Kanye-approved wardrobe, very feminine, but still stylish and sleek," Henry said. "If Kim and Kanye have a little baby boy, they definitely need a pair of black leather high-top Young Versace sneakers, which retail for $300. These are shoes Kanye would envy."


 Rumored to be in attendance at the "garden chic" baby shower is Beyoncé. Kim and Bey have formed a friendship over the past year, with Kim hitting up Beyoncé's Mrs. Carter World Tour in London and bonding at last year's Watch the Throne concert. Babies have most likely been a conversation topic amongst the women, with Beyoncé possibly giving Kim advice on how to always look fierce while caring for a newborn.

"At Bel Bambini we sell a $1,000 Cavalli diaper bag that would be perfect for Kim," Henry said. "And her good pal Beyoncé also uses a Cavalli diaper bag, so they'll both look stylish at their upcoming play dates."And when baby Kimye is not playing with Blue Ivy, she will most likely be jetsetting around the world. From Los Angeles to Paris, this newborn will be traveling in style, whether it's in a deer skin leather car seat or in a stroller that incorporates Kanye's other love: fine art.

"Bugaboo strollers are a celebrity must-have, and their new collaboration with the Andy Warhol estate has produced some very unique styles that Kim and Kanye would love," Henry said.


Share:

Justin Bieber matatani, gari lake sasa lashikiliwa na polisi kisa hiki hapa


Licha ya watu kumchukia Chriss Brown kwa tabia zake sasa kibao hicho kimeamia kwa msanii justine Bieber ambae ameandamwa sana na majirani zake baada ya majirani hao kupiga kelele za kuomba msaada kupitia vyombo vya habari wakimtuhumu mwimbaji huyo kugeuka kero na kuvuruga utulivu ktk maeneo hayo kwa tabia yake ya kuendesha gari kwa kasi, kupiga kelele na kuvuta marijuana mbele ya watoto, kilio chao kimefika mbali baada ya gari la msanii huyo kuingia mikononi mwa polisi.
Ripoti zinasema gari la mwimbaji huyo aina ya Farrari lilisimamishwa na polisi nje kidogo ya geti la Bieber sababu ikiwa ni mwendo kasi uliopitiliza kwa kuzingatia kuwa yuko katika maeneo ya makazi ya watu. Lakini bahati nzuri Bieber mwenyewe hakuwa na gari hilo siku hiyo na lilikuwa linaendeshwa na rafiki yake aliyefahamika kwa jina la ‘Lil Twist’.

Lakini ripoti kutoka chanzo cha kuaminika upande wa polisi ni kwamba baada ya mahojiano ya muda polisi hao walimpa onyo kijana huyo na kumruhusu aendelee na safari yake.

Hivi karibuni majirani zake Justin Bieber walilalamika na kutishia kumfungulia mashtaka kwa kuwa huwapigia kelele nyingi akiwa anarudi kutoka club na rafiki zake, lakini pia huendesha gari lake kwa kasi sana wakati yuko katika eneo la makazi ya watu, na tuhuma mbaya zaidi ni kwamba huvuta marijuana mbele ya watoto wao wenye umri mdogo.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive