Monday, 3 June 2013

MAPYA YAIBUKA KUHUSU KIFO CHA MANGWEA....ALIYELALA NAE ASIMULIA ALIYOYAONA WAKATI NGWEA AKIKATA ROHO..!!

HUKU mwili wake ukitarajiwa kuwasili Bongo kesho, kifo chake Albert Mangweha ‘Ngwea’ kilichotokea katika hali ya utata Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini, kimeibua mambo mapya, Ijumaa Wikienda lina mzigo wote.

MAMA MANGWEA NAYE AZIDIWA, AKIMBIZWA HOSPITALI YA MKOA
Habari kutoka msibani Moro jana zilisema mama mzazi wa marehemu Mangwea, Denisia Mangwea naye alizidiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa baadhi ya waombolezaji msibani hapo, mama huyo alipata mshtuko wa moyo kufuatia kifo cha mwanaye ambapo taarifa za kifo hicho zilimshtua tangu Jumanne mpaka alipozidiwa jana.

HABARI KUTOKA SAUZI SASA
Habari kutoka kwenye Jiji la Johannesburg ambako Ngwea alifia, mtiririko wa maelezo ya wenyeji wa Mangwea na Mgaza Pembe ‘M 2 The P’ nayo yanaibua mapya ambayo awali yalikuwa hayajulikani.
MAELEZO YA SAUTI ZA WENYEJI
Wakizungumza hewani kupitia redio moja ya jijini Dar, wenyeji wao wawili waliojitambulisha kwa jina moja moja la Godfrey na Godluck ambao walikuwa na Mangwea na M 2 The P, kila mmoja alisema lake huku maelezo yao yakionesha dalili ya kutofautiana au kuzua maswali masikioni mwa watu.

KUMBE WALITOKA KLABU SALAMA
Godluck siku hiyo aliwaendesha wawili hao kutoka klabu kurudi nyumbani walikofikia kwa wiki mbili nyuma ambako ni kwa Godfrey. Godluck alikuwa akitumia gari lake.
Kwa mujibu wa Godluck, waliondoka klabu alfajiri kurudi nyumbani kwa Godfrey au God wakiwa salama salimini. Waligonga mlango, God akatoka kufungua, wakaigia ndani wote.
Godluck anaishi sehemu tofauti na nyumba hiyo, lakini kwa sababu saa 2:00 asubuhi Ngwea na M 2 The P walitakiwa kurejea Bongo na ni yeye ndiye aliyetakiwa kuwapeleka uwanja wa ndege, hivyo aliamua kulala palepale.
Alisema wakiwa chumbani, watu wanne, yeye, Ngwea, M 2 The P na mwenyeji Godfery, Ngwea alianza kuonesha dalili za kushangaza.
“Kule chumbani Ngwea alikuwa ananilalialalia huku amelegea, nikawa namuuliza we vipi? Hanijibu, mara akanitapikia, nikamwamsha hakuamka, nikamwamsha God (Godfrey) na kuuliza huyu vipi? Nikamwamsha M 2 The P, nikamuuliza huyu vipi, mbona ananitapikia, akasema huyo ndiyo zake akilewa huwa anakuwa hivyo, si unajua mambo yake tena,” alisema Godluck akikariri maneno ya M 2 The P.
Aliendelea kusema kuwa ghafla alimuona M 2 The P naye kama akaanza kuzidiwa. “Nikamuuliza we vipi? Lakini nikajua labda ni haya mambo yao, maana unajua mimi nilikuwa siwaelewielewi,” alisema Godluck.
Alisema ilipofika saa mbili asubuhi, akiwa anajua wasafiri hao wameshachelewa ndege, yeye aliamua kuondoka kurudi kwake ambako si mbali akipanga kwenda kulala hadi mchana.
Akasema: Lakini nikiwa nakwenda nyumbani, NILIMPIGIA SIMU MIDO, dogo mmoja anaishi jirani, nikamwambia wale jamaa (akina Ngwea) kama wamezidiwa, nenda kawacheki.
Alisema akiwa amelala, aliamshwa na simu ya Mido, akaipokea na kuambiwa hali za jamaa hao ni mbaya sana hivyo yeye akalazimika kwenda na kuwapakia kwenye gari lake WOTE WAWILI hadi Hospitali ya St. Hellen Joseph ambako ilithibitishwa na daktari kwamba, Ngwea aliaga dunia ila M 2 The P hali tete.
MAELEZO YA GODFREY SASA
“Siku ya mwisho, walitoka wakarudi asubuhi, wakanigongea mlango, nikawafungulia. Wakaingia, Ngwea akaniambia NICHUKUE ‘KONTAKTI’ (mawasiliano) yake, nikachukua notebook yangu na kuandika. Walikuwa wazima kabisa.
“Basi, tukawa tunaongeaongea pale kama mtu wa kawaida tu. Hakuniambia kama anaumwa popote wala hakula chochote.
“Baadaye ndiyo wote wawili wakazidiwa, tukawachukua kuwapeleka hospitali ambako daktari alisema Ngwea alifariki dunia lakini M 2 The P hali yake ilikuwa mbaya akalazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).”
KUNA MADAI MAITI YA
NGWEA ILITUPWA NJE YA JIJI
Mtangazaji alimuuliza Godfrey kuhusu madai kwamba, kabla ya Ngwea kupelekwa hospitalini, mwili wake ulikutwa nje ya Jiji la Johannesburg ukiwa umetupwa.
Godfrey: Si kweli, alizidiwa palepale nyumbani ndiyo tukamchukua kumpeleka hosptali. NGWEA NILIMPAKIZA KWENYE GARI LANGU, mwenzake alikuwa kwenye gari la nyuma.
MASWALI MAGUMU
Katika maelezo ya wawili hao, Godluck alisema alipokuwa anarudi kwake, alimpigia simu dogo anaitwa Mido na kumwambia kuhusu kuzidiwa kwa akina Ngwea aende akawacheki, kwa nini asimpigie simu Godfrey ambaye ndiye mwenyeji wa wawili hao, ndiye aliyewafungulia mlango na ndiye aliyemwamsha kumwambia kuhusu hali ya Ngwea?
Godluck yeye alisema aliwapakia wawili hao kwenye gari lake hadi hospitali, lakini Godfrey alisema alimpakia Ngwea kwenye gari lake na M 2 The P alipakiwa kwenye gari jingine la nyuma yake (labda la Godluck).
Godfrey, kwa mtangazaji alikiri kuishi na Ngwea kwa wiki mbili, lakini pia akasema usiku wa kuamkia kifo chake marehemu alimpa mawasiliano, ina maana hakuwa na kontakti za Ngwea kwa siku zote kumi na nne alizoishi pale?
MANENO YA MAMA YAKE MZAZI
Jumamosi iliyopita, mwandishi wetu mkoani Morogoro alifika msibani na kufanikiwa kukutana na mama mzazi wa Ngwea, Denisia Mangwea akiwa na majonzi mazito ambapo alisema:
“Mwanangu Albert amekwenda, najua sitamuona tena katika maisha ya duniani, inaniuma sana. Nilimpenda sana na yeye alinipenda sana lakini Mungu kaamua kumchukua.”
MAZIKO
Kumekuwa na utata wa kuwasili kwa mwili wa marehemu Ngwea, awali ilidaiwa ungefika jana na kuzikwa Jumanne, Kihonda Morogoro, lakini baadaye ikadaiwa mwili huo sasa utawasili kesho Jumanne.
Wakati hayo yakiendelea, jana Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya alikwenda nyumbani kwa baba mdogo wa marehemu Ngwea, David Mangwea, Mbezi Beach, Dar na kusaini kitabu cha maombolezo.
MUNGU ailaze pema peponi roho ya marehemu Mangweha. Amina.

Share:

BINTI AANIKA MAKALIO MBELE YA WABUNGE KATIKA SHINDALO LA MISS TABORA

Mmoja wa washabiki wa muziki wa kizazi kipya ambaye alivaa vazi lililoacha matako nje....

Shabiki huyo alipanda jukwaani kumkumbatia msanii maarufu nchini , Ommy Dimpoz wakati alipokuwa akitoa burudani katika mashindano ya Redds Miss Tabora.

Tukio hilo la aibu lilitokea mbele ya wabunge....

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Bw.William Ngereja akiwa na Diwani wa kata ya Kitete manispaa ya Tabora Bw.Daniel Mhina ambaye alikuwa MC katika onesho hilo lililofanyika katika ukumbi wa Frankman Hotel mjini Tabora.
Ommy Dimpoz akitokwa na machozi wakati akitumbuiza jukwaani alipofikia hatua ya kumkumbuka marehemu msanii maarufu Mangwea.
Ommy Dimpoz alionesha kukubalika zaidi katika onesho hilo

Mbunge Ngereja akiwa na mbunge wa vitimaalum mkoani Tabora wakijaribu kucheza kwa pamoja muziki uliokuwa ukiimbwa na Ommy Dimpoz.


Redds Miss Tabora 2013Annastazia Donald(19)ambaye ni mwanafunzi wa Theofil Kisanji University,kushoto ni mshindi wa pili katika kinyang'anyiro hicho Sabrina Juma(18) kutoka chuo cha African Utalii na mshindi wa tatu ni Cornecia Cossei(21)kutoka chuo cha Utumishi wa Umma Tabora.  




Share:

Mapendekezo ya wagombea huru TZ

Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania, imependekeza wawepo wagombea huru katika ngazi za uchaguzi mbalimbali nchini humo. Hayo ni miongoni mwa mapendekezo yaliyotangazwa jijini Dar es salaam na Mwenyeketi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Kwanza ya Katiba Mpya.

Jaji Warioba amesema pia wapo wananchi waliopendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe kugombea nafasi zote isipokuwa nafasi ya urais. Jaji Warioba amesema tume ilipitia maoni hayo na kupendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe kugombea nafasi zote kuanzia ngazi ya Mwenyekiti wa Mtaa hadi nafasi ya Urais.
Taarifa zinazohusiana
Tanzania

Kadhalika Jaji Warioba amesema, Tume pia imependekeza kwamba, mgombea yeyote wa urais ili athibitike kuwa ni mshindi atalazimika kupata zaidi ya asilimia hamsini ya kura, na kwamba endapo mgombea hatafanikiwa kupata asilimia hamsini uchaguzi utarudiwa kwa kuangalia wagombea wawili waliopata kura nyingi.

Mapendekezo mengine yaliyotangazwa na Tume ni pamoja na kuwepo kwa serikali tatu yaani ya Bara,Zanzibar na ile ya Shirikisho.

Pia tume imependekeza kuwa, Bunge la Muungano liwe na jumla ya Wabunge 75, hamsini kutoka Bara, ishirini kutoka visiwani na watano wateuliwe na Rais kutoka makundi maalum ya walemavu.

Mapendekezo mengine ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni pamoja na Rais kubakia na madaraka yake ya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu, lakini uteuzi wa ngazi za chini uachiwe Tume ya Utumishi.

Imeeleza kwamba, Rais mara baada ya kufanya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu wakiwemo, mawaziri, manaibu waziri, jaji mkuu na naibu jaji mkuu, viongozi hao watalazimika kuthibitishwa na Bunge.
Share:

Wanavyoandamwa na Ukeketaji Uingereza

                                                                  Ukeketaji au kukatwa kwa sehemu za siri za mwanamke ,                                                                              inadhaniwa kuwaathiri angalau wanawake 66,000                                                                                    nchini Uingereza.
Mara nyingine kitendo hiki hufanyika kwa wasichana ambao hurejeshwa nyumbani kwa jamaa zao Afrika Mashariki, lakini pia inaaminika kuwa wanawake wanakeketwa nchini Uingereza pia.
Taarifa zinazohusiana
afya

Hata hivyo hakuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa dhidi ya wanaotenda unyama huo lakini serikali inasisitiza kuwa iko tayari kuhakikisha kuwa ukeketaji unakwisha.

Hospitali kadhaa na kiliniki za kijamii mjini London, huwasaidia wanawake ambao wamekeketewa. Pia kuna kliniki moja Birmingham na nyingine inatarajiwa kufunguliwa Bristol.

Moja ya kliniki za serikali katika hospitali yaChelsea, huwatibu zaidi ya wanawake 100 kila mwaka ambao wamekeketwa na kuwashona kwa sababu ya imani za kitamaduni, akiwemo Filsan, mwenye umri wa miaka 35.

Filsan ni mama mwenye watoto watatu na anaishi nchini Uingereza . Alikabidhiwa nguo mpya akiwa tu na umri wa miaka saba , ikiwa ni dalili ya muda kuwadia wa yeye kukeketwa.

"wasichama wamekuwa wakikeketwa kisiri nchini humu, lakini huu ni unyanyasaji wa wanawake na watoto.''


miguu kufungwa pamoja'

''Nilihisi uchungu mwingi, licha ya kudungwa sindano ya kumaliza uchungu. Wakati uchungu ulipokwisha, singeweza hata kwenda haja ndogo.'
tulilazimika kulala sakafuni , kwa sababu hata hatungeweza kutembea. Miguu yetu ilikuwa imefungwa kwa kamba, kwa hivyo hatungeweza kuitenganisha , yaani uchungu ulikuwa mwingi sana.
"na sasa ikafika muda wangu kujifungua mwanangu wa kwanza. Nilichokuwa nakitafakari tu, je mtoto anaweza kupitia vipi katika sehemu ambayo imeharibiwa hivyo?

''Ilikuwa hali ngumu sana kwangu.Kutafakari yote niliyoyapitia, lakini kwa sasa nina afueni kwa sababu nilikuwa na daktari mzuri ambaye aliweza kuelewa kila kitu nilichokuwa napitia.''
Inasemekana kuwa zaidi ya wasichana 20,000, walio chini ya umri wa miaka 15 , huwa katika hatari ya kukeketwa kila mwaka nchini Uingereza.
Wanawake 66,000 nchini Uingereza wanaishi na athari na makovu ya ukeketeji nchini Uingereza.

Kumbu kumbu za Filsan humletea majonzi tele. Lakini jazi yake anayoifanya na shirika moja la kisomali, inampa matumaini kwa sababu anahisi kuwa watu wa jamii yake wameanza kupinga ukeketeaji.

Anasema kuwa watu wanafahamu na kuelewa kuwa sio kitendo kizuri na kuwa kinahitaji kukomeshwa.

Inasemekana kuwa zaidi ya wasichana 20,000, walio chini ya umri wa miaka 15 , huwa katika hatari ya kukeketwa kila mwaka nchini Uingereza.

Wanawake 66,000 nchini Uingereza wanaishi na athari na makovu ya ukeketeji.


Hakuna manufaa yoyote ya kiafya yanatokana na ukeketaji, bali wanawake huharibiwa sehemu zao za siri bure.
''Kazi nyingi inafanywa barani Afrika, lakini lazima tuwahamasishe watu ikiwemo jamii kila sehemu ambazo zinakumbatia utamaduni wa kuwakeketa wanawake,'' anasema Filsan

Tangazo maalum la kibiashara limepeperushwa kwenye stesheni moja ya kisomali na hivyo kuchochea idadi kubwa ya watu wanaopiga simu katika kniliki ya Queen Charlotte's.

Mkunga Juliet Albert, alielezea kwa nini baadhi ya familia hulazimu wasichana wao kukeketwa.

Anasema ''wanawake wengi, husema kuwa hawatakubali kufanyiwa kitendo hiki , lakini kwa sababu ya shinikizo za kimila na kitamaduni kuhusiana na ukeketeji, hawezi kukwepa.

Baadhi ya wanawake huwa na wasiwasi kuwa ikiwa wasichana wao hawatafanyiwa kitendo hicho, jamii itawatenga na kuwa hawawezi kuoleka tena.

Wao hupata matayizo mengi ya kiafya kutokana na kufanyiwa ukeketaji, kama magonjwa , uchungu wakati wa kujifungua au hata wakati wanapokuwa wanajamiiana na waume zao.

Na tunachokifanya ili kurekebisha tatizo hilo ni kushona na kuacha shimo ndogo wanayotumia kujifungulia mtoto na kujamiiana.''

Kliniki hii huwaelekeza wasichana na wanawake kwa wahudumu wa kijamii ikiwa wanahisi kuwa yeyote anakabiliwa na tisho la kukeketwa
.
Waziri wa afya Anna Soubry anasifu hatua hii sana



Bi Soubry anasema kuwa wanawalinda watoto wote nchini humo licha ya wanavyotaka wazazi wao.

"licha ya kuwa hatujachukua hatua zozote za kisheria dhidi ya wale wanaohusika na vitendo hivyo, haimaanishi kuwa ni sawa kwa vitendo hivyo kuendelea,'' alisema waziri Soubry

Share:

Familia ya Pistorius yashtushwa na picha


Familia ya mwanariadha mlemavu nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius, wameshstushwa na picha zilizofichuliwa za bafu alimomuulia mpenzi wake mnamo mwezi Februari.


                            Pistorius atafikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa                                                                                                  dhamana

          Shirika la habari la Uingereza la Sky, mnamo Ijumaa, lilionyesha picha za kuogofya zinazoshukiwa kuwa za bafu ambalo mpenzi wa Pistorius Reeva Steenkamp, aliuawa.
Taarifa zinazohusiana
ajali, Afrika Kusini

Polisi walisema kuwa wamechukizwa mno na kufichuliwa kwa picha hizo.

Bwana Pistorius mwenyewe anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake, kupitia mlango wa bafu alimokuwa , alisema alidhani kuwa alikuwa mwizi aliyevamia nyumba yake.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa hatua ya mahakama mwanzo kutathmini kesi siku yake Jumanne.

Pistorius ni mwanariadha mlevamu asiye na miguu yake miwili ingawa hukimbia kwa miguu bandia au vyuma. Alishiriki michezo ya Olimpiki mjini London mwaka jana.

''Familia ya Pistorius ilimuunga mkono alipokuwa anajiandaa kufikishwa mahakamani , alisema mjomba wake,'' Arnold Pistorius.

''Tunaamini maneno yake , tunampenda na tutamuunga mkono kwa kila hatua ya kesi hii,''alisema Mjombake Pistorius.

"tumeshtushwa na picha hizi za ajali iliyotokea nyumbani kwa Oscar."

Msemaji wa polisi ameelezea kuwa polisi wanachunguza nani aliyefichua picha hizo .

''Kitendo hiki hakikuhitajika na kimetuudhi kweli. Hatujui picha hizi zimetoka wapi,'' alisema polisi huyo.

Pistorius atafikishwa mahakamani Jumanne kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana, kufuatia kukamatwa kwake, kuhusu mauaji ya Steenkamp.

Kesi hiyo inatarajiwa kuakhirishwa kwani uchunguzi wa polisi ungali unaendelea.

Pistorius ameajiri baadhi ya mawaklili shupavu nchini Afrika Kusini kumtetea.

Anasema kuwa alimpiga risasi Bi Steenkamp kupitia mlango wa choo kimakosa baada ya kudhani kimakosa alikuwa mwizi.

Hata hivyo, viongozi wa mashtaka wanasema kuwa alimuua kwa maksudi baada ya wawili hao kugombana.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive