Tuesday, 25 June 2013

"LAZIMA NIFE KABLA YA KUFIKISHA MIAKA 40"...AUNT EZEKIEL

WAKATI vifo vikizidi kuwatafuna wasanii, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka na kudai kuwa hawezi kuishi miaka mingi na atakufa mapema kuliko watu wanavyodhani.

Aunt Ezekiel alifunguka hayo juzikati alipokuwa akipiga stori na mwandishi wetu jijini Dar ambapo alibainisha kuwa akijitazama mustakabali wa maisha yake basi anaona kabisa kuwa hawezi kufikisha hata miaka 40 kabla hajafa.

“Daah! Sijielewi kabisa yaani kwa jinsi ambavyo najiona, nikifikisha miaka 40 ni bahati aisee, dunia sasa imebadilika sana,” alisema Aunt.


Share:

MWANAMKE AOLEWA NA WANAUME WAWILI NA KUISHI NAO...!!!


MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji iitwayo Kayoga.

Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.

“Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sauti pale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anaweza kuongeza mwanamume mwingine,” anasema mmoja wa majirani hao.

Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa na amani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.

Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mume mkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliweka pingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’ wa mtoto huyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sita iliyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye baba mzazi wa mtoto.

“Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandalizi yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huo ilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia pale Padri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.

“Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado bali wake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena na majibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana,” alisema Katekista Abel.

Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wake ni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapo na baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidia mkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogo wake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.

Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.

"Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugia mpangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa hao yanawahusu nini watu hao?” alihoji.

“Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumba nitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?” alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwamba wataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akina mama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaume wawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufunga ndoa na mume mmoja.

Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili na kuwa na mamlaka juu yao.
Share:

POLISI WAMKEMEA JOYCE KIRIA KWA KUANDAMANA, HAYA HAPA NDIO MAJIBU


Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu (Imetolewa na Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania)
Joyce Kiria akizungumza na waandishi wa habari Jana jijini Dar es salaam ambapo alidai hajui mume wake yuko wapi



Share:

VIONGOZI WATANO WA CHADEMA WASHITAKIWA KWA UGAIDI .... MAJINA YA VIONGOZI HAO HAYA HAPA

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na vijana wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu mkazi Tabora mjini.

Mbali ya Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni Evodius Justinian wa Buboka, Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel Kihawa wa Dodoma, leo wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na kumwagia tindikali Musa Tesha katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika mwaka 2011.

Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.

Kesi hiyo ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, ya Tabora Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara Baada ya kusomewa shitaka hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili Prof Abdalah Safari, ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela ulitoa hoja kuiomba mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa sababu, kwanza mashtaka hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.

Sheria za uendeshaji wa makosa kama hayo hapa nchini zinadai kuwa mashataka kama hayo yanapofunguliwa ni lazima ridhaa ya Mkurugenzi wa mashtaka iwepo. Kwa kuwa ridhaa hiyo haikuwepo, mawakili waliiomba mawakili kuitupilia mbali kesi hiyo.


Sababu ya pili iliyotolewa na upande wa Utetezi ilikuwa kwamba maelezo ya kesi kuwa ni ya ugaidi, yalikuwa hayaonyeshi kuwa ni ya kigaidi tofauti na makosa mengine ya kawaida kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hivyo waliiomba Mahakama kutupilia mbali shitaka hilo au lifunguliwe kama kosa la kawaida.

Na sababu ya tatu ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, sheria inaelekeza kuwa mshitakiwa ashitakiwe katika mahakama yenye mamlaka na hadhi kama ile waliyopelekwa katika maeneo yale walikokamatwa. Hivyo mawakili waliiomba mahakama itupilie mbali shitaka, kwani washitakiwa kama walikuwa na hatia walipaswa kushitakiwa katika maeneo yao walipokamatwa. Baada ya hoja hizo, Mahakama iliahirisha kesi hiyo na itatajwa tena Julai 8 mwaka huu Tabora Mjini.

Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi au wafuasi wa chadema kufunguliwa kesi zinazohusiana na ugaidi, tarehe 18 Machi 2013, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare, la Ludovick Joseph walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya ugaidi.


Kosa jingine lililowakambili Lwakatare na Ludovick ni kula njama; kosa ambalo pia linawakabili washtakiwa wote ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume na kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Katika kosa la tatu, washtakiwa wote wawili wanadaiwa kufanya mkutano wa kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi.

Wakili wa serikali alidi kuwa washitakiwa wote Desemba 28 Mwaka jana walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyara Msaki kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi.

Pamoja na tuhuma hizo, 8 Mei, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimfutia mashitaka matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Katika uamuzi huo Jaji Lawrance Kaduri akitoa uamuzi huo alisema ulitokana kukubaliana na hoja ya mawakili wa Lwakatare; Tundu Lissu, Peter Kibatara na Mabere Marando na kusema kuwa.

“Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama inatoa amri ya kumfutia Lwakatare mashitaka matatu, yaani kosa la pili, tatu na la nne kwa sababu Jamhuri imeshindwa kuonesha maelezo yanayotesheleza kumshitaki Lwakatare kwa kesi ya ugaidi.


“Naamuru jalada la kesi ya msingi lilirudishwe Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya mshitakiwa kuendelea kushitakiwa kwa kosa moja la kula njama ambalo linaangukia katika sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002,” alisema Jaji Kaduri

Share:

USHAIDI WA PICHA MME WA JOYCE KIRIA NA VIJANA WENGINE WACHADEMA WAKIWA NA PINGU,KESI YA UGAIDI IGUNGA


 Bw.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza 
Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.
Kamanda Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na wtuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013.



Share:

MAREKANI YATOA ONYO KALI KWA MSAFARA WA RAIS OBAMA TANZANIA

Dar es Salaam. Licha ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.
Mbali na tahadhari hiyo, ziara hiyo ya Obama itakuwa na ulinzi mkubwa ambao pengine haujawahi kutokea katika historia ya viongozi wa nje wanaotembelea Tanzania kwani utahusisha idadi kubwa ya magari, ndege za kijeshi na meli kubwa ya kivita ambazo zitakuwa zikifanya doria karibu na pwani ya Tanzania.
Tahadhari za matumizi ya chakula, maji na nyinginezo zimetolewa katika nchi zote tatu za Afrika ambazo Obama atatembelea, kila moja kwa jinsi Wamarekani hao wanavyoitathmini.
Rais Obama atatembelea nchi za Tanzania, Senegal na Afrika Kusini.
Ulinzi
Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post la Marekani, ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa na gharama kwa walinzi, lakini safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.
Tahadhari
Kwa mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya Marekani, ambayo Mwananchi imepata nakala yake, watu watakaokuwa kwenye msafara wa Obama wametakiwa kutotumia kachumbari. Pia imewataka kutumia maji ya chupa zaidi.
“Kutokana na mfumo wa maji uliopo, tunashauri watu wetu kutumia maji ya chupa zaidi kwa kunywa na hata kwa kupiga mswaki,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa kuelewa fika tatizo la ugonjwa wa malaria nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa kutumia dawa ya mbu ya kupaka na kupuliza inayoitwa Deet.

Deet ni dawa maarufu huko Marekani na ikiwa katika aina tofauti ikiwamo ya kupaka na kupuliza na imekuwa ikitumiwa na jeshi la Marekani kwenye vita mbalimbali tangu miaka ya 1940 kabla ya kuanza kutumiwa na raia mwaka 1957.
ATM nazo noma
Pia watu watakaokuwa kwenye msafara wa Rais Obama wametakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za kutolea fedha (ATM) zilizoko karibu na hoteli watakazofikia.
“Kuna tatizo la uhalifu kwa hiyo siyo vizuri kutumia ATM ambazo ziko katika sehemu zisizo salama. Pia katika kipindi watakachokuwa Tanzania watu wanapaswa kutumia teksi ambazo zimeidhinishwa na hoteli.
“Pia siyo vizuri kuacha kompyuta ya fedha kwenye vyumba mtakavyolala. Pia kina mama wanapaswa kuchukua tahadhari ya mabegi yao watakapokuwa wanapita mitaani,” ilitahadharisha taarifa hiyo.

Share:

TUMUOMBEE MZEE MANDELA AFYA YAKE YAZIDI KUDORORA, IKULU KWA ZUMA HAKUKALILIKI...!!!

Nelson Mandela ‘Madiba’.

Habari hizo ambazo awali zilifanywa siri kabla ya kuvuja wikiendi iliyopita, zinasema kuwa Ikulu ya Afrika Kusini ilikosa umakini, hivyo ikaacha gari bovu limbembe Mzee Mandela na matokeo yake lilizimika kwenye barabara kuu (high way).

Kuzimika kwa gari hilo, kulisababisha hekaheka lakini ufumbuzi wa haraka ulikosekana mpaka dakika 40 baadaye ndipo ‘ambulance’ nyingine ilipofika eneo la tukio, ikambeba Mzee Mandela na kumuwahisha hospitali.

Ikulu ya Afrika Kusini imelazimika kutoa tamko, baada ya wachambuzi kuelezea tukio hilo kwamba zilikuwa dakika 40 za hatari za Mzee Mandela, kwa maana nusura zichukue uhai wa kiongozi huyo aliyeongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, miaka ya 1900 nchini humo.
Tukio lenyewe, lilijiri Juni 8, mwaka huu (zaidi ya wiki mbili zilizopita) lakini ikawa kimya katika vyombo vya habari, japo minong’ono iliendelea kushamiri, kabla ya mambo kuwekwa hadharani wikiendi iliyopita.

KIVIPI DAKIKA 40 ZA HATARI?
Kwa mujibu wa habari pamoja na makala za wachambuzi mbalimbali wa kisiasa nchini Afrika Kusini, muda mfupi baada ya Mzee Mandela kuondolewa barabarani pale gari lilipomzimikia na kuwahishwa katika Hospitali ya Mediclinic Heart, Pretoria, uvumi ulienea kuwa ameshafariki dunia.

Mchambuzi wa siasa za Afrika Kusini, Olwethu Sipuka ambaye makala zake hupatikana zaidi kwenye Tovuti ya Politicweb ya nchini humo, alieleza kuwa zile dakika 40 zilikuwa za hatari mno kwa Mzee Mandela ndiyo maana wananchi waliamini uvumi kuwa alifia pale.
“Afadhali taarifa za gari lililomzimikia zilisambaa baadaye, kama zingewahi, wananchi wangekusanyika eneo la tukio na pengine ingekuwa hatari sana kwa afya ya Madiba,” aliandika Sipuka na kuongeza:
“Kama wananchi wangewahi kufika pale barabarani, pengine wangetaka kumbemba Madiba wampeleke hospitali. Kama wangeamini amekufa, isingekuwa rahisi kwao kukubali ambulance nyingine imbembe. Hiyo ni hatari ambayo ingeweza kumsababishia kifo.”

Kwa upande mwingine, habari zinasema kuwa baada ya gari kuzimika, Mzee Mandela hakupata huduma yoyote kwa muda wote wa dakika 40 ambazo alikwama pale barabarani.
Dk. Mamphela Ramphele ambaye naye ni mchambuzi wa siasa za nchi hiyo, alihoji katika makala yake ni kwa nini baada ya kuzimika ambulance ambayo ni ya kijeshi, haikwenda nyingine ya serikali kumchukua Mzee Mandela, badala yake ikaenda ya kiraia?

Aliandika kuwa afya ya Mzee Mandela haipaswi kufanyiwa mchezo, kwani jeshi la Afrika Kusini halina ambulance moja, ile ya kiraia haiwezi kuwa na ubora unaotoa huduma kwa mgonjwa anayestahili matibabu ya ICU (kiwango cha uangalizi wa hali ya juu).

Zipo taarifa zinazosema kuwa zile dakika 40 alizokwama barabarani, zilisababisha hali ya Mzee Mandela iwe mbaya zaidi, kwani baada ya ambulance ya pili kuwasili, aliwekwa katika mashine ya oksijeni ambayo ilimsaidia kupumua mpaka alipofikishwa hospitali.
Mchambuzi mwingine, Blade Nzimande, aliandika kuwa kutoka Johannesburg, nyumbani kwa Mzee Mandela mpaka Pretoria kwenye Hospitali ya Mediclinic Heart, ni umbali wa zaidi ya maili 31 (kilometa 50) hivyo ilihitajika umakini wa hali ya juu.

“Alitolewa nyumbani akiwa na hali mbaya, inafahamika macho yote ya wananchi wa Afrika Kusini yanafuatilia mwenendo wa afya yake. Gari lililombemba halikutakiwa kuwa na hitilafu ya injini. Kuna uzembe mkubwa umefanyika.”

IKULU YATOA TAMKO
Kutokana na kuenea kwa uvumi huo, Ikulu ya Afrika Kusini, wikiendi iliyopita, ilitoa tamko kuhusiana na tukio hilo la ambulance iliyokuwa imembeba Mzee Mandela kuzimika barabarani.

Msemaji wa Ikulu ya Afrika Kusini, Mac Maharaj, alisema kuwa ni kweli kwamba gari lililokuwa limembeba Mzee Mandela lilizimika barabarani lakini halikumwathiri kwa chochote.

“Alikuwa na madaktari ambao walijiridhisha kwamba hakutakuwa na hatari yoyote katika kusubiri gari lingine la kumpeleka hospitali,” alisema Maharaj kwa niaba ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.

Aliongeza: “Ambulance iliyokuwa imembeba ilikuwa inasindikizwa na magari mengine, kwa hiyo kama hali ingekuwa mbaya zaidi, angehamishwa katika gari lingine na kukimbizwa hospitali. Haikuonekana hatari kubwa.

“Timu ya madaktari kutoka idara ya ulinzi ilijiridhisha kwamba afya ya Mzee Mandela itakuwa salama ndiyo maana waliruhusu subira hiyo ya dakika 40. Ile ambulance ni ya jeshi, tulipewa taarifa baada ya kuzimika, tukafanya juu chini kupata nyingine, ikaonekana itachelewa zaidi ndiyo maana ikatumika ya kiraia.

“Tunapenda wananchi wote wajue kuwa tupo makini na afya ya mzee wetu. Ile ambulance ya kijeshi ina vifaa vyote ya ICU na madaktari waliokuwa wamemzunguka ni madaktari bingwa, kwa hiyo wana uwezo mkubwa. Hakukuwa na uzembe hata kidogo.”

ZUMA IKULU HAPAKALIKI
Kwa mujibu wa taarifa za Ikulu ya Afrika Kusini, afya ya Mzee Mandela, inasababisha Rais Zuma asiwe na utulivu, kwani muda mwingine anafuatilia maendeleo ya kiongozi huyo aliyewahi kufungwa jela miaka 27, kipindi anaongoza harakati za kupinga sera za ubaguzi wa rangi nchini humo.

Imeelezwa kuwa tangu Aprili 29, mwaka huu, pale Zuma alipomtembelea Mzee Mandela na kuona ukweli jinsi afya yake inavyobadilika na kuwa mbaya zaidi, amekuwa hakai akatulia ikulu, badala yake hutumia muda mwingi kufuatilia maendeleo ya rais huyo wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini.

Habari zinafafanua kuwa siku hiyo, Zuma ambaye aliongozana na viongozi wengine wa Chama cha African National Congress (ANC), kwenda kumjulia hali hali, alishtushwa kuona Mzee Mandela akiwa hatikisi kichwa wala kupepesa macho.

Chanzo kimoja kutoka Ikulu ya Afrika Kusini ambacho hakikutajwa jina, kilieleza kwamba hata safari za nje, Zuma amezipunguza kwa hoja kwamba taifa halitamwelewa yeye kuwa mbali katika kipindi hiki ambacho Mzee Mandela anaumwa sana, japo afya yake inaelezwa kuimarika.

MBEKI AWATOA HOFU WANANCHI
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, amewatoa hofu wananchi wa nchi hiyo kuwa Mzee Mandela anaendelea vizuri, ingawa katika siku za hivi karibuni amekuwa akipelekwa hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kutibiwa.
Mbeki aliyemrithi Mandela mwaka 1999, alisema kuwa ni vizuri wananchi wakadumisha sala kwa kumwombea mzee huyo badala ya kukata tamaa na kuamini uvumi kwamba ameshafariki dunia.

ANC YATAKA MANDELA AHESHIMIWE
Chama cha ANC, Jumamosi iliyopita, kilitoa tamko kuwa Mzee Mandela inabidi aheshimiwe na kwamba siyo kila mtu anaweza kuwa msemaji wa maendeleo ya afya yake.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Ikulu ya Afrika Kusini inabidi ifanye kazi vizuri kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kweli na zenye uhakika kuhusu kiongozi huyo aliyeiongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 1994 mpaka 1999.

“Chama chetu cha The African National Congress kwa mara nyingine kinataka pande zinazohusika zifanye kazi yake. Vilevile tunataka vyombo vya habari na familia, kuheshimu taarifa za faragha kuhusu Mandela.”

TATIZO NI MAPAFU
Mzee Mandela ambaye mwezi ujao anatarajiwa kutimiza umri wa miaka 95, kwa muda mrefu sasa anasumbuliwa na tatizo la mapafu kujaa maji.
Habari zinasema kuwa tatizo la mapafu, ni matokeo ya athari alizozipata akiwa gerezani kipindi alipofungwa miaka 27 jela katika miaka ya 1900.
TUMUOMBEE MZEE MANDELA

Mandela amekuwa kielelezo chema siyo tu kwa Afrika Kusini, bali Afrika na duniani kote. Nasi Watanzania kila mtu kwa imani yake ni vema kumuombea salama ili Mungu ampe nafuu na kumponya maradhi yanayomsibu kwa sasa.
Share:

HAWA NDIO AINA YA WANAUME ASIOWAPENDA JACQUELINE WOLPER "GAMBE"

Jacq wolper

Jacqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai hawapendi wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu na si rahisi kuonyesha mapenzi yao ya dhati kwake, pia hawezi kutembea nao hadharani kwa kuhofia ndoa zao.

“Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake halafu mtu mzima hivi unakosa penzi la kweli. Mapenzi yenu yatakuwa ya chumbani tu,” alisema.

“Hamtaweza kutembea pamoja, lakini ukiwa na kijana ambaye ni rafiki hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake.

“Wengi wenye fedha zao kuna wakati wananiona nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke, ninahitaji kuwa na mtu anayenijali na kuwa karibu na mimi.

“Kuna watu wanaamini fedha zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau.”
Anasema wengine huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni malaya, lakini wanasahau kuwa nao ni binadamu.

“Kila binadamu anapenda na kupendwa,” alisema.

Share:

MAMA ALIA BAADA YA KUJIFUNGUA MAPACHA WALIOUNGANA KWENYE MAKALIO MBEYA...!!!


MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Kasumuru, Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Grace Joel Lwesha (19), amelia baada ya kujifungua watoto walioungana.Akizungumza na waandishi wetu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jengo la Watoto, Grace alilia kutokana na kile alichodai kujifungua watoto walioungana wakati yeye ni maskini.
Watoto hao mapacha wa kiume, Eliudi na Elikana wameungana sehemu ya makalio hivyo kulazimika kutumia sehemu moja ya haja kubwa.

Grace aliwaambia waandishi wetu kwamba, watoto hao walizaliwa katika Hospitali ya Kyela, Februari 20, mwaka huu wakiwa na miguu miwili na mikono miwili kila mmoja.
“Baada ya kujifungua Machi mosi nilihamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa uchunguzi zaidi ili waweze kujua ni jinsi gani watakavyotenganishwa,” alisema.

Hata hivyo, hospitali hiyo ya mkoa haikufanikiwa badala yake Machi 16, walimhamishia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kuanzia hapo mpaka sasa anafanyiwa maandalizi kwa ajili ya safari ya kupelekwa nchini India kwa upasuaji.
“Ninawapenda sana watoto wangu hawa pamoja na kwamba wapo katika hali hii, ndugu zangu walipokuja hospitalini kuniona akiwema mama yangu walinifariji na kunisihi nisiwachukie nizidi kuwapenda.

“Kuwatunza ni kazi ngumu sana kwani mara nyingi wamekuwa wakininyima usingizi kwa sababu wamekuwa wakilala kwa nyakati tofauti.
“Nakumbuka siku niliyojifungua mume wangu alikosa raha lakini sasa anawapenda kwani amejua kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.

“Maisha yetu ni magumu kwani tunatoka kwenye familia maskini, kazi yetu ni kilimo cha kutumia jembe la mkono hivyo bado kuna mahitaji mengi nashindwa kumudu. Nichukue nafasi hii kuwaomba msaada Watanzania wote walioguswa na tukio hili,” alisema Grace.
Grace alifunga ndoa na Erick William Mwakyusa Desemba 23, 2010 na katika ndoa yao wamejaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Lide (3) na hao mapacha ni uzao wake wa pili.

Mama huyo anaomba msaada kwa mtu yeyote aliyeguswa na habari hii atume mchango wake kupitia namba 0753308525 ambayo ni ya mumewe au aende kumuona Muhimbili.
Share:

KAJALA AKUNUSHA KUHUSU KUGOMBANA NA WEMA SEPETU

Kajala akiwa kajiachia katika pozi

Baada ya siku chache za magazeti ya udaku nchini kuripoti kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa karibu sana kati ya mwanadada Wema sepetu na Muigizaji mwenzake Kajala masanja, tuliamua kufanya uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa suala hili ili tusije kuipotosha jamii kwa habari za zisizo na ushahidi wowote.

Katika habari iliyoripotiwa na blogs na magazeti kadhaa ya udaku kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema kuwa chanzo ni vitendo vya mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala kwenye dili anzopata za kucheza filamu na hasahasa kumkosesha dili ya kwenda china kufanya filamu aliyoalikwa na watanzania waishio nchini humo.

Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta hewani wasanii hawa ili tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada Kajala alikuwa wa kwanza kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo na kuwashangaa wanaoziandika wanazipata wapi.

“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala

Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema
“Wolper nimekutana naye kwenye party ndo tukaamua kupiga picha, au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu mwingine zaidi ya wema? Wolper ni rafiki yangu” Alisisitiza Kajala

Tulipojaribu kumtafuta wema simu yake ilikuwa haipokelewi na baadaye ilipokelewa na alisema yuko location anatengeneza filamu na mwigizaji Rado hivyo tumtafute baadaye.

Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive