Thursday, 13 June 2013

RAIS PAUL KAGAME AMGOMEA JK

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amemshambulia kwa maneno makali Rais Jakaya Kikwete, akijibu ushauri alioutoa kwa serikali yake wa kukaa katika meza ya mazungumzo na waasi wa kikundi cha Democratic Force for the Liberation of Rwanda (FDLR), ili kumaliza mapigano. Shirika la Habari la Rwanda, linalojulikana kwa jina la News of Rwanda, jana lilimkariri Rais Kagame akitoa maneno ya kejeli na yenye mwelekeo wa kupuuza ushauri wa Rais Kikwete.

Kauli hiyo ya Rais Kagame, ambayo pia imesambazwa katika mitandao mbalimbali ya habari, inaonyesha kukerwa na ushauri wa Rais Kikwete ambao ameuita upumbavu uliojazwa ujinga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Kagame kutoa kauli hiyo tangu Rais Kikwete alipotoa ushauri huo, wakati akizungumza katika kikao cha Mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika mapema mwaka huu, mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Waasi wa FDLR ambao jamii yao ni Watutsi, walikimbilia nchini Kongo baada ya mapigano ya kimbari ya mwaka 1994, yaliyosababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wamekuwa wakiendesha chokochoko dhidi ya Serikali ya Rais Kagame.

Akizungumza katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi maofisa 45 wa jeshi lake, Rais Kagame alisema ushauri wa kufanya mazungumzo na waasi wa FDLR ni ujinga na haupo katika historia ya Wanyarwanda.

“Nilinyamza kimya kwa sababu sikupenda kusikiliza ushauri kuhusu FDLR, kwa sababu nafikiri ni upuuzi ulioambatana na ujinga, hatuwezi kuacha maisha yetu kama Wanyarwanda tunavyoishi sasa.

“Ushauri wa Kikwete ni sawa na kucheza na makaburi ya watu wengi ambao ni ndugu zetu,” alisema Kagame.

Katika hatua nyingine, Rais Kagame alilihimiza jeshi lake kujiimarisha na kuendelea na moyo wa ulinzi wakati wote.

Akiwa mjini Addis Ababa, katika mkutano uliojadili suala la amani ya Kongo pamoja na ukanda wa maziwa makuu, Rais Kikwete alitoa ushauri ambao uliwagusa pia Rais Yoweri Museveni na Joseph Kabila, ambao aliwataka kufanya mazungumzo na waasi wanaopingana na serikali zao.

Rais Kikwete alisema Rwanda inapaswa kufanya mazungumzo na waasi wa FDRL ambayo ni njia muafaka ya kutafuta amani katika eneo la Mashariki ya Kongo.

Inadaiwa kuwa ushauri huo wa Rais Kikwete ulipokelewa kwa hisia tofauti na viongozi wa ngazi za juu, hususan wale wa usalama wa serikali ya Rwanda na wapo walioamini kuwa hana huruma na maisha ya Wanyarwanda, kwa kile walichodai kuwa ameonyesha kuyapendekeza makundi ya waasi ya FDLR, ambayo yanahusishwa na wapiganaji wa Interahamwe, yaliyoendesha mapigano mwaka 1994.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo, amekwishakaririwa akieleza kuwa ushauri wa Rais Kikwete ni jambo lisilokuwa la kawaida lenye udhaifu.

Naye mmoja wa wasomi nchini humo aliyezungumzia ushauri wa Rais Kikwete, ambaye ametambulishwa kwa jina moja la Profesa Rwanyindo, aliuelezea ushauri wa Rais Kikwete kuwa upo katika mtazamo wa kupuuza historia iliyolikuta taifa hilo hapo nyuma.

Wahanga wa mauaji ya kimbari wamemuandikia barua Rais Barack Obama wakimuelezea Kikwete anavyoonea huruma kundi la watu ambao Marekani yenyewe imeshawajumuisha katika makundi ya kigaidi.

Dadisi za wachambuzi nchini Rwanda zinaelezea kuwa kauli ya Rais Kikwete ni sawa na mapendekezo yasiyokuwa katika mpangilio kwa kupendelea waasi wa FDLR, hali inayozua wasiwasi kuwa anaweza asiwe na msaada wa kusimami amani, ustawi na ushirikiano katika nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Wakati huo huo, Rais Kagame ameyashutumu mashirika mbalimbali vya Umoja wa Mataifa kwa kuwa na uhusiano wenye mashaka na mamlaka za Afrika.

“Wapo kwa sababu moja …wametoka kwa wakoloni waliotutawala, natolea mfano kwa haya waliyotusema kuwa sisi tunahusika na machafuko yanayotokea Kongo,” alisema Rais Kagame.
Share:

MUME WA MTU ANASWA GUEST HOUSE NA SHOGA WAKIFANYA UCHAFU WAO

 Tukio hilo lililoshuhudiwa na watu kibao, lilijiri Juni 10, mwaka huu katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Kunaswa kwa wanaume hao ambao ilidaiwa walikuwa kwenye harakati za kufanya Usodoma na Ugomora, kulifuatia mke wa mmoja wao kunasa meseji za kimapenzi walizokuwa wakitumiana wawili hao.
Mama huyo alipobaini meseji hizo chafu, wawili hao wakisisitiziana kukutana kwenye gesti hiyo usiku wa siku hiyo, alimpigia simu mmoja wa waandishi na kumpa mkasa mzima ambapo walikubaliana saa moja zoezi la kuwanasa litaanza..
Ilipofika saa 1:30 usiku, timu yetu, mama huyo, wapambe wake na polisi walikuwa wanafanya doria nje ya gesti hiyo.

Saa 5:30 usiku, mume wa mwanamke huyo akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa shoga walifika gesti hiyo bila kujua kama waliwekewa mtego wa kunaswa na kwenda kuchukua chumba namba 2.
Wakiwa ndani, mke alimpigia simu mumewe na kuhoji alipokuwa akajibiwa alikuwa mitaa ya nyumbani kwao Manseze, Dar akipiga stori na rafiki zake.

Wawili hao wakiwa wanajiandaa na mchezo wao usiofaa, polisi aligonga mlango akijifanya mhudumu aliyetaka kumpatia taulo, jamaa bila kujua alifungua ndipo walipofumaniwa na kuibua varangati zito.

Kufuatia timbwili hilo, waliwekwa chini ya ulinzi na kutolewa pale gesti tayari kupelekwa kituoni ndipo mwanaume anayedaiwa kuwa shoga akatimua mbio mithili ya mwanariadha wa kimataifa, Usain Bolt wa Jamaika na wanandoa hao waliendelea kuzozana huku mke akimlalamikia mumewe na kumwambia wakifika nyumbani ampe talaka yake.

Hata hivyo, mwanamke huyo aliomba sakata hilo lisipelekwe polisi kwa madai alichotaka ni kumfumania mumewe na kwamba alikuwa na ushahidi wote.

GPL
Share:

JACK WOLPER ............''BABY MADAHA ASITAKE KUPATA UMAARUFU KUPITIA JINA LANGU TENA ANIKOME"

MWANADADA anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Jaqueline Massawe ‘Wolper Gambe’ amesema anamshangaa sana msanii wa muziki ambaye pia ni mwigizaji Baby Madaha kutumia vyombo vya habari kutengeneza ugomvi wakati hana mawasiliano naye yoyote na wala si rafiki yake au mtu aliyekaribu naye na hana mazoea naye.


“Nimelizika na umaarufu nilio nao sihitaji kujipeleka katika magazeti na kuongelea vitu ambavyo havina faida katika jamii, mimi sina urafiki na Baby Madaha, namshanga anavyotapatapa kuniandika vibaya kwa jambo lisilo nihusu, mambo hayo niliyafanya nikiwa Chipukizi”
“Nakumbuka mimi nilipigiwa simu na rafiki yake akiniomba namba mwenye nyumba lakini ghafla nikapiwa simu na mwandishi wa habari mara Polisi nikashangaa huyo mtu hata namba ya mwenye nyumba sijamtumia nasumbuliwa na watu utafikiri mimi ndio mtuhumiwa, lakini jambo ninalomshangaa mimi ni dalali?,” alihoji Wolper.
Hivi karibuni yalizuka maneno yakiwahusisha wasanii hawa wawili ikisemekana walikuwa wakigombea nyumba ya kupanga, huku Baby Madaha kuigizwa mjini na mwenye nyumba kwa kupangishwa nyumba hewa, Wolper amedai kuwa kwa sasa yeye amekuwa makini halipii nyumba kienyeji bali ulipia kwa mwanasheria wake tena kwa kufuata taratibu kwa kukwepa utapeli.
Share:

ZITO KESHO KUWA MGENI RASMI SHOW YA MWANA FA, HUKU SUGU AKIWA KWA JIDE


Ile the Big Square 1, show za magwiji wa muziki Tanzania mwana FA ‘The Finest’ na Lady Jay Dee ‘Miaka 13 ya Lady Jay Dee’ zitapigwa kesho June 14, huku presha ikiwa inaongezeka hasa kwa fans wanaotamani kuhudhuria show walioichagua na kuona ukubwa wa show kama walivyotarajia.

Show hizi kubwa zina nguvu sana kutokana na ukubwa wa majina ya wasanii husika. Kwa mujibu wa lady Jay Dee timu anaconda kesho itaungwa mkono na mheshimiwa Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.

Jide ambae hivi karibuni ameachia wimbo mpya unaopatikana kwenye album yake ‘Nothing but the truth’ inayoitwa Yahaya, amepost kupitia kupitia ukurasa wake wa facebook na pia katika akaunti yake ya Twitter kuonesha list ya wasanii watakaopanda jukwaani, na pia uwepo wa Sugu.

” Miaka 13 ya Lady JayDee, Ijumaa ya kesho shughuli inaanza rasmi saa 3:00 usiku...Ukiskia paaaa ujue show imeisha

1. Prof Jay 2. Juma Nature 3. Grace Matata 4. Hamza Kalala 5. Wakazi na ugeni wa Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU

Nyimbo zote unazozipenda zitalia tar 14 June, pale Nyumbani Lounge sababu yaaaaa sababu yaaaaaa ?????????”
Kwa upande wa Mwana FA ambae atapiga show yake na Live band akiwa na kundi kubwa na maarufu kwa upigaji wa Live Band ‘Wananjenje’, yeye amepewa full sapoti na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.
Zitto ameweka wazi kupitia akaunti yake ya twitter kuwa anamsapoti sana msanii huyo.

“You have my full support “@MwanaFA”

Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive