Tuesday, 21 April 2015
Waziri wa TAMISEMI ameitaka mifuko ya jamii kusaidia watumishi kupata makazi.
Mh Ghasia ametoa wito huo jijini dar es salaam wakati wa utiliaji
saini makubaliano kati ya shirika la elimu kibaha na watumishi HOUSING
kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma zinazotarajiwa
kujengwa ndani ya eneo la shirika hilo ambapo amewataka kulenga maeneo
yenye upungufu mkubwa wa nyumba za watumishi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa NHC Dk. Fred Msemwa amesema kupitia
ubia huo katika kipindi cha miaka mitano watajenga nyumba 1,150 pamoja
na miundombinu mingine inayoendana na huduma za jamii na hivyo
kutawawezesha wafanyakazi mbalimbali waliopo ndani na nje ya kibaha
kunufaika na kuongeza kuwa nyumba hizo watauziwa watumishi wa umma na
baadae wananchi wa kawaida kwa masharti nafuu.
Serikali ya Tanzania imesema hakuna watanzania waliouawa katika matukio ya mauji Afrika kusini.
Serikali imesema hakuna mtanzania
aliyeuawa katika matukio ya mauji ya chuki za kibaguzi (ZENOPHOBIA)
yanayofanywa na raia wa Afrika Kusini dhidi ya wageni na tayari imeanza
mpango wa kuwarudisha nyumbani watanzania 21 kati ya 23 waliohifadhiwa
katika kambi kwenye mjini DURBUN nchni humo kwa ajili ya usalama.
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe amesema vifo vya watanzania
watatu vilivyotokea nchni humo havina mahusiano na mauaji hayo
ZENOPHOBIA na kusisitiza serikali ya afrika kusini imeanza kuchukua
hatua na tayari watu wawatu waliohusika na kifo cha rais wa msumbiji
wamekamatwa.
Akizungumzia idadi ya watanzania waliohifadhiwa kwenye
Kambi katika mji wa DURBUN,Mhe Membe amesema takribani watanzania
23 wamehifadhiwa katika kambi ya isipingo iliyo na zaidi ya raia wa
kigeni elfu tatu ambao wako chini ya ulinzi wa serikali ya afrika kusini
na kusisitiza serikali imeanza utaratibu wa kuwarudisha nyumbani
watanzania 21 kati yao.
Akielezea msimamo wa tanzania kufuatia mauaji hayo ya ZENOPHOBIA
yanayoendelea nchni afrika kusini,Mhe. Membe amesema serikali inaunga na
jumuiya ya nchi za SADC kulaani vitendo vya mauaji yanayoendelea nchni
humo ambapo watu 8 wamekwisha uawa kikatili na kuita serikali ya afrika
kusini kuzuia mauaji hayo haraka iwezekanavyo.
Aidha amesema serikali ya Tanzania haitakuwa na tatizo la
watanzania kurudi nchni humo baada ya mauaji kudhibitiwa na kwa upande
wa wafanyabishara walisajiliwa kihalali na kupoteza mali zao, serikali
itawasiliana na wanasheria wake ili kuona namna ya kutafuta namna ya
nchi hiyo kuwafidia hasara waliyoipata.
Serikali yatakiwa kuvishirikisha vikundi vya uhamasishaji kukabiliana na mauaji ya imani za kishirikina.
Akizungumza katika ibada maalumu ya kuhamasisha jamii kujiepusha na
vitendo vya kishirikina iliyoanadaliwa na wadau mbali mbali kwa
ushirikiano na kanisa la Pentekost kamanda wa vijana wa mkoa wa
Arusha Bw. Philemon Molllel amesema baada ya kubainika kuwa ushirikina
ndio msingi mkuu wa mauaji ya walemavu wa ngozi,vikongwe,na maovu
mengine katika jamii kinachohitajika ni kushirikiana na kuhamasishana
kuutokomeza kazi ambayo vikundi hivyo vinaiweza.











