Idara
ya maafa katika ofisi ya waziri mkuu inakusudia kutumia mabati mepesi
kuwajengea waathirika wa mafuriko badala ya kutumia mahema ambayo
yanachakaa kwa mda mfupi na kusababisha serikali kuingia garama ya
kununua mahema mara kwa mara.
Mkurugenzi wa kitengo cha maafa katika ofisi ya waziri mkuu
Brigedia general Mbazi Msuya ameyasema hayo katika kikao cha kazi cha
wadau na watendaji wanaohusika na maafa katika halmashauri ya wilaya ya
Mvomero kilichojadili juu ya mwongozo wa kuchukua hatua za dharura
kulingana na rasilimali zilizopo ambapo ameeleza mpango wa kutumia
mabati hayo ambayo yanafahamika kama Pre Fabricated House utaanza baada
ya sampo itakayokubalika kupelekwa ngazi za juu kwaajili ya
kuidhinishwa.
Nae mkurugenzi msaidizi wa kitengo hicho naima mrisho amesema juu
mpango huo ambao umeanza na wilaya 15 za Tanzania kwa mkoa wa Morogoro
ikiwa wilaya ya Mvomero na Kilosa amesema lengo kubwa nikuhakikisha
wanazuia majanga ambayo yamekuwa yakigharimu vifo na vilema vya maisha
huku mkuu wa wilaya ya Mvomero Festo Kiswaga amepongeza mpango huo
ambapo amesema wilaya hizo zimekuwa zikitokea maafa ya mara kwa mara