Sunday, 19 April 2015

dara ya maafa ofisi ya waziri mkuu inakusudia kutumia mabati laini kwa waathirika wa mafuriko Morogoro.

Idara ya maafa katika ofisi ya waziri mkuu inakusudia kutumia mabati mepesi kuwajengea waathirika wa mafuriko badala ya kutumia mahema ambayo yanachakaa kwa mda mfupi na kusababisha serikali kuingia garama ya kununua mahema mara kwa mara.
Mkurugenzi wa kitengo cha maafa katika ofisi  ya waziri mkuu Brigedia general Mbazi Msuya ameyasema hayo katika kikao cha kazi cha wadau na watendaji wanaohusika na maafa katika halmashauri ya wilaya ya Mvomero kilichojadili  juu ya mwongozo wa kuchukua  hatua za  dharura kulingana  na rasilimali zilizopo ambapo ameeleza mpango wa kutumia mabati hayo ambayo yanafahamika kama Pre Fabricated House  utaanza baada ya sampo itakayokubalika kupelekwa ngazi za juu  kwaajili ya kuidhinishwa.
 
Nae mkurugenzi msaidizi wa kitengo hicho naima mrisho amesema juu mpango huo ambao umeanza na wilaya 15 za Tanzania kwa mkoa wa Morogoro ikiwa wilaya ya Mvomero na Kilosa amesema lengo kubwa nikuhakikisha wanazuia majanga ambayo yamekuwa yakigharimu vifo na vilema vya maisha huku mkuu wa wilaya ya Mvomero Festo Kiswaga amepongeza mpango huo ambapo amesema wilaya hizo zimekuwa zikitokea maafa ya mara kwa mara
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive