Hayo yameelezwa na mwanasheria wa kituo cha sheria na haki za
binadamu (LHRC) Bi.Geline Fuko wakati akizungumza katika mikutano
mbalimbali ya kutoa elimu kuhusiana na katiba inayopendekezwa mjini
songea.
Bi.Geline Fuko amesema katika maeneo mbalimbali waliyozunguka
wamebaini kuwa machapisho ya katiba pendekezwa yako machache hivyo
wameitaka serikali kuchapisha machapisho hayo ya kutosha.
Katika mkutano uliofanyika chuo cha ualimu Songea TTC na
kuwashirikisha wanachuo na walimu katika chuo hicho wanachuo wamekosoa
katiba pendekezwa kutokidhi matakwa ya wananchi.





