Sunday, 22 March 2015

manchester united yailaza liverpool anfield

Manchester United waishinda liverpool
Nahodha wa kilabu ya Liverpool Steven Gerrard alipewa kadi nyekundu baada ya sekunde 38 baada ya kuingia katika kipindi cha pili ili kuchukua mahala pake Adam Lalana aliyepata jeraha.
Kutolewa huko kuliisaidia Manchester United kuishinda Liverpool katika uwanja wa nyumbani wa Anfield.
Gerrard aliingizwa baada ya Juan mata kuifungia Manchester United bao la kwanza ili kuimarisha safu ya kati ilokuwa ikitawaliwa na manchester United. .
Nahodha huyo alimkanyaga Ander Herrera na hivyobasi kupata kadi nyekundi swala lililoathiri mchezo wa Liverpool.
Baadaye Juan Mata alipata bao la pili alilofunga vizuri na hivyobasi kuipatia ushindi manchester united
Share:

Nimeshawishika nitagombea urais 2015;asema Lowassa

Edward Lowassa
Katika Kurasa za magazeti ya Leo zimepambwa na tarifa mbambali za kurasa za mbele za magazeti zinaonyesha dhahiri Edward Lowassa kukubali kugombea Urais, Okello nimelifuatia suala hili kwa karibu mengi nimeyapata kutoka kwa Mashekh wa Bagamoyo. Ni ukweli dhahiri upande wa Jakaya katika dhamira yake ya dhati ni kumkabidhi Edward Lowassa ikulu ya magogoni.

Mengi katika vipaumbele vya ujumbe wa Jakaya katika ni kuhakikisha Edward Lowassa anaendeleza Yale ambayo ameyaacha ikiwemo elimu, Afya bora, miundombinu na kufuta umaskini kwa Watanzania wote.

Kumejitokeza makundi mbali mbali yakimtaka kugombea Urais, yeye binafsi amesema anafarijika kuona Watanzania wanasimama nae katika hili, mbali historia ya uongozi wake uliotukuka basi hii nafasi ya Watanzania kumuomba atangaze nia inampa nguvu hasa Dk. Jakaya kumtumia ujumbe mzito.

MAAMUZI NA MATUMAINI MAPYA NA EDWARD LOWASSA 2015.
Share:

wanajeshi watoto waachiliwa huru sudan kusini




Wanajeshi watoto

Waasi nchini Sudan Kusini wamewaachilia huru wanajeshi watoto wapatao 250 .
Ni oparesheni ya tatu katika msururu wa hatua zilizoanza kuchukuliwa na jeshi hilo mnamo mwezi Januari.
Mpango huo unatokana na makubaliano ya amani yaliotiwa sahihi mwaka uliiopita kati ya serikali na waasi katika jimbo la Jonglei wanaojulikana kama Kobra.
Shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF ambalo linasaidia katika operesheni hiyo limesema kuwa watoto wengine 400 zaidi pia wataachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo na kuifanya kuwa idadi kubwa ya watoto wanajeshi walioachiliwa kufikia sasa.
Hatahivyo UNICEF limesema kuwa kuna takriban wanajeshi watoto 12,000 wanaohusishwa na mzozo unaondelea kati ya serikali na waasi wanaoungozwa na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive