Sunday, 22 March 2015

wanajeshi watoto waachiliwa huru sudan kusini




Wanajeshi watoto

Waasi nchini Sudan Kusini wamewaachilia huru wanajeshi watoto wapatao 250 .
Ni oparesheni ya tatu katika msururu wa hatua zilizoanza kuchukuliwa na jeshi hilo mnamo mwezi Januari.
Mpango huo unatokana na makubaliano ya amani yaliotiwa sahihi mwaka uliiopita kati ya serikali na waasi katika jimbo la Jonglei wanaojulikana kama Kobra.
Shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF ambalo linasaidia katika operesheni hiyo limesema kuwa watoto wengine 400 zaidi pia wataachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo na kuifanya kuwa idadi kubwa ya watoto wanajeshi walioachiliwa kufikia sasa.
Hatahivyo UNICEF limesema kuwa kuna takriban wanajeshi watoto 12,000 wanaohusishwa na mzozo unaondelea kati ya serikali na waasi wanaoungozwa na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive