Friday, 3 April 2015

arsenal kuchuana na liverpool

Arsenal
Arsenal itamkagua mshambuliaji Danny Welbeck ambaye ana jeraha la goti.
Mikel Arteta ,Alex Oxlaide Chamberlain,Mathieu Debuchy na Abou Diaby hawatachezeshwa licha ya kurudi katika mazoezi,lakini Jack Wilshere huenda akachezeshwa.
Liverpool
Wachezaji wa Liverpool, nahodha Steven Gerrard na Martin Skrtel wanaanza kuhudumia marufuku yao ya mechi tatu lakini Lucas amerudi baada ya jeraha la paja.
Daniel Sturridge huenda akachezeshwa baada ya kupona jeraha la kiuno naye Raheem Sterling amepona jeraha la kidole cha mguuni lakini Adam Lallana hajulikani iwapo atachezeshwa kutokana na Jeraha la kinena
Share:

fmilia kutambua miili huko garrisa

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa
Familia za wanafunzi waliouawa katika chuo kikuu kazkazini mashariki mwa Kenya zimeenda katika eneo la mkasa ili kuitambua miili ya waliouawa.
Zaidi ya watu 140 waliuawa katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Al shabaab mjini Garissa siku ya alhamisi ambapo wapiganaji hao waliwatenganisha wanafunzi hao kwa misingi ya kidini kabla ya kuwaua wanafunzi wa kikristo.
Wakati huohuo mamlaka nchini Kenya imetoa mabasi ili kuwasafirisha wanafunzi walionusurika hadi makwao,huku miili ya waliofariki ikisafirishwa hadi mjini Nairobi.
Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamoud,amesema kuwa Somalia na Kenya lazima ziimarishe ushirikiano wao dhidi ya Ugaidi baada ya shambulizi hilo.
Share:

rais wa somalia ataka ushirikiano na serikali ya kenya.......

Rais wa Somalia
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, amesema kuwa Somalia na Kenya zinafaa kuimarisha uhusiano wao dhidi ya ugaidi, baada ya wapiganaji wa kiislamu kushambulio chuo kimoja kikuu mjini Garrisa hapo jana Alhamisi.
Watu 147 waliuwawa wengi wao wakristo, baada ya wanamgambo hao wa Al- Shaabab kutumia kigezo cha kidini ili kuwatenganisha.
Bwana Mohamoud ametaja mauaji hayo kama tendo la kinyama ambalo halina msingi katika dini ya kiislamu.
Ametoa rambirambi zake kwa serikali ya Kenya.
Kenya imetoa zawadi ya shilingi millioni 5 kwa mtu yeyote atakayeweza kumkamata Mohammed Kano ,mwalimu wa zamani ambaye anashukiwa kupanga mauaji hayo.
Kwa sasa anaidaiwa kuwa nchini Somalia.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive