Monday, 17 June 2013

SINGIDA:MSICHANA WA MIAKA 19 ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUMTUPA MTOTO WA SIKU 10........

Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP.Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya kukamatwa kwa Aziza Jumanne (19) mkazi wa kijiji cha Sughana jimbo la Singida kaskazini kwa tuhuma ya jaribio la kuuwa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa siku kumi.(Picha na Nathaniel Limu).

Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mkulima Aziza Jumanne (19) mkazi wa kijiji cha Sughana tarafa ya Mgori jimbo la Singida Kaskazini, kwa tuhuma ya jaribio la kumtupa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa siku 10 kwa lengo la kumuua.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida Geofrey Kamwela, amesema kuwa tukio hilo la aibu na la kusikitisha, limetokea Juni 12 mwaka huu saa nane mchana kweupe katika kijiji cha Sughana.
Amemtaja mtoto huyo mchanga wa kiume aliyetupwa na mama yake kuwa ni Akramu Alfa.

Kamwela amesema siku ya tukio mama yake mkubwa na mtuhumiwa Mariamu Ramadhanai alipata wasi wasi baada ya kutomwona Aziza akiwa muda mrefu bila kuwa na mtoto wake mchanga.
Amesema “kutokana na wasi wasi huo, Mariamu aliweza kuita majirani kwa ajili ya kumhoji Aziza alikompeleka mtoto wake mchanga.

Baada ya kumhoji Aziza aliweza kufunguka na hivyo kwenda kuonyesha mtoto wake shambani alikomtupa na bahati nzuri, walikikuta kichanga hicho bado ki hai”.
Kamanda huyo amesema kuwa uchunguzi wa awali unaomyesha wazi kuwa Aziza ametenda kosa hilo baya baada ya kutekelezwa na mwanaume aliyempa mimba na kumzaa Akramu.

Hili ni tukio la pili ndani ya mwezi moja na nusu kwa watoto kutupwa na mama zao kwa lengo la kuwaua.
Mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, inadaiwa mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu tawi la mkoa wa Singida, alimtupa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi mitano kwenye pagala la nyumba.

Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela hadi sasa mzazi huyo hajulikani alikokimbilia na mama yake mzazi kutoka Babati alifika ili amchukue mtoto huyo aliyetekelezwa, lakini hakuweza kukabidhiwa kwa madai hakuna ushahidi wa kuonyesha amezaliwa na mtoto wake aliyekuwa akisoma uhasibu.

Share:

MKASA MZIMA KUHUSU KUPIGWA KWA MBUNGE NASSARI KATIKA KITUO CHA KURA MAKUYUNI

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshambuliwa na vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Arusha aliyejulikana kwa jina la Kalanga na kulazimika kulazwa katika hopitali ya Selian Mkoani Arusha katika fujo zilizotokea katika kituo cha kupigia kura cha Zaburi, kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.

Akizungumza kutoka eneo la tukio, Mratibu wa wanawake wa Chadema Mkoa wa Arusha Sesilia Ndossi alisema “muda wa saa 5 asubuhi tulienda katika kituo cha kupiga kura cha Zaburi, kumsindikiza Mbunge wa Arumeru ambaye katika Uchaguzi huo yeye alikuwa Wakala.

"Lakini tulipofika hapo tulimkuta raia mmoja mwenye asili ya kisomali akiwaita watu na kuwaambia pigia CCM, ndipo Nassari akamuuliza kwanini unapiga kampeni kituoni...

"Huyo Baba alihamaki, akamrukia Nassari wakamchangia na Diwani mmoja aliyeitwa Kalanga, wakamsukuma akaanguka damu ikaanza kumtoka puani...

"Baada ya hapo,tukalazimika kuingilia kati na kuondoka na Nassari akaenda mahali tulipokuwa tunalala akabadili mavazi akaenda kutibiwa Minjingu,

"Hata tulipofika huko waliendelea kutufuata wakaja na gari imejaa vijana wa kimasai wakimtafuta Nassari. Tulivyoona hivyo, tulilazimika kukodi gari ambayo hawaifahamu ndipo tukamwondoa kumpeleka Arusha hospitali ya Selian kwa matibabu zaidi."

Taarifa zaidi kutoka Makuyuni zinasema walipomkosa Nassari walimpiga dereva wake Gadi Palangyo na Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Monduli, Thomas Kilongola, hadi walipokuja kuokolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Makuyuni.

Hadi tunaandika habari hii Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia suala hili baada ya simu yake kuita bila mafanikio.

Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive