Akizungumza na ITV afisa uhamiaji mkoa wa Geita Charles washima amesema kati ya wahamiaji hao 23 mmoja ameshashitakiwa mahakamani na kuhukumiwa kwenda jela miezi tisa kutokana na kupatikana na hatia ya kuingia nchini kinyume cha sheria, aidha kati ya wahamiaji haramu waliokamatwa wengi wao ni watoto wadogo chini ya umri wa miaka kumi na nane ambapo idara hiyo inaandaa utaratibu wa kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Baadhi ya wahamiaji haramu hao kutoka burundi wamesema wamelazimika
kukimbia nchini mwao kutokana maisha magumu na hali ya vurugu
zinazoendelea kwa wananchi kupinga rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza
kuingia katika awamu ya tatu ya kuwania kugombea kiti cha urais.










