Thursday, 18 July 2013

Fabregas asema hataki kurejea England

Mcheza kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas amesema hana nia yoyote ya kuihama klabu hiyo na kurejea tena nchini England.

Cesc Fabregas
Hayo ni kwa mujibu wa kocha wake Tito Vilanova.
Klabu ya Manchester United siku ya Jumatatu iliwasilisha ombi la kutaka kumasajili nahodha huyo wa zamani wa Arsenal, kwa kitita cha pauni milioni ishirini na tano, lakini Vilanova amesema mchezaji huyo anataka kusalia nchini Uhispania kwa sasa.
''Ni ishara nzuri kwa klabu yoyote kupata maombi kutoka kwa vilabu vingine, vinavyotaka kuwasajili wachezaji wake, lakini Fabregas amesema anataka kusalia'' Alisema kocha huyo.
Vilanova ameongeza kusema kuwa'' Fabregas hataki kujiunga na timu zingine kwa sababu ya pesa au kutokana na muda wake wa kucheza uliosalia. Anafahamu huku kuna ushindani mkali, lakini ni uamuzi wake kusalia na Barcelona. Kwa sasa nimetulia''.
Kufikia sasa Barcelona halijasema lolote rasmi kuhusiana na ombi hilo la Manchester United, ambalo linaaminika kuwa chini ya dhamana kamili ya mchezaji huyo.
Fabregas alikuwa mchezaji mchanga zaidi wa Arsenal wakakti aliocheza dhidi ya Rotherham United wakati wa mechi ya kombe la ligi mwaka wa 2003 akiwa na miaka kumi na saba na siku mia moja na sabini na saba.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Arsenal walioishinda timu ya Manchester United kupitia mikwaju ya penalti kwa fainali ya kombe la FA mwaka wa 2005.
Vile vile Fabregas, anaichezea timu ya taifa ya Uhispania na aliisaidia kunyakua kombe la dunia na pia kuwa mabingwa wa bara Ulaya mara mbili.
Alijiunga na Arsenal mwaka wa 2003 akiwa na umri wa miaka kumi na sita.
Fabregas aliichezea Arsenal mechi 303 na kufunga magoli 57, kabla ya kusajiliwa na Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 25.4 kwa mkataba wa miaka mitano kwa wa 2011
Share:

Mzee Nelson Mandela afikisha miaka 95

Leo ni siku ya kimataifa ya shujaa wa kupinga Ubaguzi wa Rangi Afrika Kusini, Nelson Mandela.




Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela pia anaadhimisha siku ya kuzaliwa leo akitimiza miaka 95 akiwa bado amelazwa hospitalini.
Serikali ya Afrika Kusini imewaomba wananchi wake kusaidia watu wasiojiweza na kutenda mema kama heshima kwa Madiba.Mandela amelazwa hospitalini kutokana na matatizo ya kupumua.
Rais Barack Obama alimtakia kila la heri Mandela anayetambulika kama shujaa wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Madiba anasalia hospitalini mjini Pretoria, lakini madaktari wake wamethibitisha kuwa afya yake inaendelea kuimarika.
Naye rais Jacob Zuma amemtakia kila la heri Mandela katika sherehe za siku ya kuzaliwa kwake.
Watoto kwenye shule kote nchini humo walitarajiwa kuanzisha sherehe hizo kwa kumuimbia Mandela wimbo wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake katika siku ambayo pia iliadhimishwa miaka kumi na mitano ya ndoa yake kwa mke wake wa tatu Graca Machel.
Mwanawe Mandela wa kike, Zindzi, alisema Jumatano kuwa afya ya Mandela imeimarika pakubwa na kwamba alimpata akiwa anatazama televisheni huku akiwasiliana kwa macho yake na mikono alipomzuru wiki jana.
''Nina matumaini kuwa atarejea nyumbani wakati wowote sasa'' Zinzi aliambia shirika la habari la Uingereza Sky News.
Siku ya kimataifa ya Mandela iliwekwa na umoja wa mataifa kama njia ya kumkumbuka mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi zake za kupatanisha watu.
Mandela anasifika kote duniani kwa juhudi zake za kumaliza vita vya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Baadaye alichaguliwa kama rais wa kwanza mwafrika wa nchi hiyo mwaka 1994.
Chama cha kitaifa cha (ANC) kimesema kuwa katika siku hii ya kusherehekea siki ya kimataifa ya Mandela, ni heshima kwa miaka yake 95 kwa maisha yake aliyoishi vyema na ambayo ameitumia kupigania wananchi wa Afrika Kusini.
Share:

BABY MADAHA AOMBA PAMBANO WA NGUMI NA JACK WOLPER


Na Gladness Mallya
STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameomba pambano la ndondi dhidi ya Jacqueline Wolper ili waweze kumaliza ubishi wa bifu lao.


Akipiga stori na paparazi wetu mapema wiki hii, Baby alisema amechoshwa kusikia tambo za mpinzani wake huyo hivyo kama kweli ni mwanamke, wakutane ulingoni ili amuoneshe cha mtema kuni.

“Asiniambie mimi natafuta kiki, mimi ni msomi kuliko yeye, arudi shule au akauze vipodozi. Najua kuimba, kuigiza na ni msomi yeye anaweza hayo? Kimsingi naomba pambano nimtandike ulingoni,” alisema Baby Madaha. 

Source:Global Publisher
Share:

KAULI YA BAN K-MOON JUU YA MAUAJI YA ASKARI WA JWTZ DARFUR


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNO), Ban K-Moon(pichani chini), amesema amesikitishwa na kuhuzunishwa na mauaji ya askari saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililofanywa na waasi wa Sudan Julai 13, mwaka huu.

Askari hao wa JWTZ waliokuwa Darfur, Sudan ya Kusini kulinda amani kwa mujibu wa UNO, walishambuliwa na waasi hao karibu na kambi ya Manawashi eneo la Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala ambapo pia askari wengine 17 walijeruhiwa baadhi yao vibaya.

Katika salamu zake hizo kupitia kwa Msemaji wake, Katibu Mkuu huyo wa Uno, ameelezea masikitiko yake kuhusiana na vifo hivyo na kutoa pole kwa familia za marehemu waliokuwa wakilinda amani, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Vikosi vya Umoja wa Afrika kwa Umoja wa Mataifa vya Kulinda Amani (Unamid).

Ban K-Moon amelaani shambulio hilo dhidi ya Unamid na kuelezea matumaini yake kwamba Serikali ya Sudan itachukua hatua zinazofaa kuhakikisha kwamba wahusika wanafikishwa mbele ya sheria.


Wakati huo huo, Taarifa iliyotolewa na Unamid juzi jioni ilisema wajumbe wa Baraza la Usalama wanalaani kwa nguvu zote mashumbulizi hayo dhidi ya askari wa vikosi vya Unamid.
"Wajumbe wa Baraza la Usalama wameelezea masikitiko yao na kutuma salamu za pole kwa familia za marehemu hao pamoja na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Aidha, wameitaka Sudan kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo na kuwafikisha wahalifu hao mbele ya mkono wa sheria.

Taarifa hiyo ya Unimad iliongeza kuwa shambulio lolote dhidi ya vikosi vya Unimad halikubaliki na kuonya kuwa lisitokee tena shambulio lingine la aina hiyo huku ikisisitiza pande zinazovutana Darfur kushirikiana kwa lengo la kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive