Monday, 8 July 2013

Graca: Zawadi za Mandela zipelekwe makumbusho

Waumini wakimwombea Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela katika Kanisa la Change Bible katika Mji wa Katlehong uliopo kilometa 40 kutoka Johannesburg jana. Picha na AFP.

Johannesburg, A Kusini Wakati Mandela akiendelea kupatiwa matibabu, mkewe Graca Machel, hajabanduka pembeni mwa kitanda alicholazwa.

Mandela amelazwa katika Hospitali ya magonjwa ya moyo ya Medi-Clinic huko Pretoria tangu Juni 8, mwaka huu na Graca amekuwa akilala hospitali katika chumba kilicho karibu na kile cha Mandela.

Msaidizi wa Mandela, Zelda la Grange alisema, Madiba siku zote amekuwa akitaka Graca awe karibu yake na hata akiumwa hupenda kufahamu yuko sehemu gani.

Hata hivyo, Le Grande, alisema Graca hatumii muda mwingi katika chumba cha hospitali, bali hulala katika kiti kilicho pembeni mwa kitanda cha Mandela.

Wapenzi hao wanatarajiwa kutimiza miaka 15 ya ndoa yao siku tatu kabla ya Mandela kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake ‘Mandela Day’ ambayo kwa Afrika Kusini, siku hiyo ni sikukuu ya kitaifa.

Imeelezwa kwamba Graca ameagiza baadhi ya zawadi, salamu za heshima na pole zinazoletwa hospitali hapo zipelekwe katika Kituo cha Kumbukumbu cha Mandela.

“Machel ameagiza tupeleke zawadi, kadi na barua zinazotumwa kwa ajili ya Mandela katika kituo cha kumbukumbu, pia amesema kama kuna barua au salamu zenye anuani, tujibu. Alishauri hivyo kwa sababu aliona vitu hivyo vikiendelea kukaa nje ya hospitali vitaharibiwa na hali ya hewa” alisema msimamizi wa kituo hicho, Vene Harris.

Tangu Mandela alazwe, Graca amekuwa mkimya, akijitokeza mara chache hadharani kiasi cha kushindwa kukutana na Rais wa Marekani, Barack Obama aliyeitembelea nchi hiyo Julai Mosi.

Wakati watoto na wajukuu wa Mandela wakipigania mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela wakirushiana maneno makali wakati baba yao yuko mahututi, Graca hajawahi kuzungumza lolote.

Watoto, Serikali wadaiwa kuuza haki ya mazishi

Gazeti la uchunguzi la The Sunday Independent la Afrika Kusini limesema mtoto mkubwa wa Mandela, Makaziwe Mandela na binamu yake, Ndileka wapo kwenye mipango ya kupata fedha kutoka kwa Televisheni ya CNN wakati wa mazishi ya baba yao.

Mmoja wa maofisa wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) ambaye pia alishiriki mkutano huo alikaririwa akisema kwamba Makaziwe na Ndileka walikaa katika mkutano wa siri mwishoni mwa Juni mwaka huu pamoja na maofisa wa shirika hilo na Ofisi ya Rais ili kupanga jinsi ya kuyarusha matangazo ya mazishi ya kiongozi huyo kwa vyombo vya kimataifa

Share:

Matonya bado ahaha rumande Songea

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Seif Shaban maarufu kama Matonya 

Dar. Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Seif Shaban maarufu kama Matonya bado anaendelea kusota rumande mjini Songea baada ya kukataliwa dhamana kutokana na kufanya utapeli baada ya kulewa kupita kiasi na kushindwa kufanya shoo iliyoandaliwa na promota mmoja mjini humo.

Matonya alitakiwa kufanya shoo kwenye Ukumbi wa Jambolee uliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Matonya alifika ukumbini akiwa amelewa hali iliyompelekea kushindwa kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo, Ndipo waandaaji wa show hiyo walipoamua ifanyike kesho yake na kiingilio kiwe ni kununua bia .

Wakati huo msanii huyo alitakiwa akafanye show nyingine Wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivyo na matokeo yake akaamua kukata tiketi kurudi Dar es Salaam. Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfata hadi alipokuwa amefikia na kukuta amehamia sehemu nyingine.

Share:

JK ataja sifa za viongozi waliofilisika kifikra

Rais Jakaya Kikwete akiweka saini juu ya mpira uliotumika katika pambano la kirafiki Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa katika Tamasha la Matumaini. Anayeangalia ni mwamuzi wa pambano hilo, Othman Kazi. Yanga ilishinda kwa penalti 4-3. Picha Michael Matemanga


Rais Jakaya Kikwete jana alipuliza kipenga kuzindua Tamasha la Matumaini Dar es Salaam na kuwanyooshea kidole viongozi wa dini wanaohubiri siasa katika maeneo ya ibada akisema kufanya hivyo ni kufilisika kifikra.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupiga filimbi kuashiria ufunguzi wa tamasha hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema ni jambo la hatari kwa Watanzania kukubali kugawanywa kwa misingi ya udini, rangi au maeneo wanakotoka.

Alitaka dini zitumike kuwaunganisha wananchi na siyo kuwagawanya akisema Watanzania wanakwenda makanisani na misikitini kusali na siyo kufanya siasa. Alisema kiongozi yeyote wa dini anayesisitiza waumini wake kuunga mkono chama chochote cha siasa amefilisika kifikra.

“Ni hatari tukigawanyika, ni lazima tuwaambie watu wanaotaka kutugawanya kwa misingi ya dini, rangi au maeneo tunakotoka kwamba hatutaki na wala hatukubali. Nchi hii wakoloni waliishindwa hivyo lazima tuendeleze utamaduni wa kukataa kugawanywa kwa msingi wowote ule,” alisema Rais Kikwete.
“Ni hatari tukigawanyika, ni lazima tuwaambie watu wanaotaka kutugawanya kwa misingi ya dini, rangi au maeneo tunakotoka kwamba hatutaki na wala hatukubali. Nchi hii wakoloni waliishindwa hivyo lazima tuendeleze utamaduni wa kukataa kugawanywa kwa msingi wowote ule,” alisema Rais Kikwete.

Aliwataka wanasiasa kuepuka kauli zenye kuchochea vurugu miongoni mwa wananchi wanapokuwa kwenye harakati zao za kisiasa akisema madaraka ya kisiasa yatafutwe kwa njia ya amani na siyo kuingiza kauli za uchochezi zenye kuwagawa wananchi.

“Nawaasa wanasiasa wasipandikize chuki za kidini au maeneo wanakotoka wananchi, kama ni madaraka yatafutwe kwa njia ya amani kwenye sanduku la kura,” alisema Rais. Alisema Tamasha la Matumaini liwe mfano wa kuigwa wa kutumia michezo kuwaunganisha watu badala ya kuwagawanya.

Alisema timu zilizotumbuiza jana zilimebeba majina ya Simba na Yanga, zimejumuisha wabunge kutoka vyama vyote ikionyesha kuwa wote ni wamoja licha ya tofauti za kisiasa.

Alipongeza mkakati wa waandaaji wa tamasha hilo ambao wametangaza kwamba mapato yatakayopatikana yatatumika kusaidia shule za sekondari katika mikoa minane nchini.

Share:

Wafuasi wa Morsi wauawa nchini Misri

Takriban watu 15 wameuawa mjini Cairo kufuatia ghasia nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi wanaamini kiongozi huyo anazuiliwa
wafuasi wa morsy


Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.

Waandamanaji hao wanasema vikosi maalum viliwafyatua risasi baada ya swala ya fajir huku wengine wakishambuliwa walipokusanyika nje ya makao ambako bwana Morsi anadhaniwa kuzuiliwa wakitaka watawala kumwachilia huru.

Msemaji wa chama cha Muslim brotherhood amesema kuwa idadi ya waliofariki katika ghasia hizo imefikia 30 huku zaidi ya watu 500 wakijeruhiwa.

Lakini katika taarifa yake, jeshi la nchi hiyo limesema kuwa kundi moja la kigaidi lilikuwa likijaribu kuingia katika kambi hiyo na kumuua mwanajeshi mmoja.

Limeongezea zaidi ya watu 200 walitiwa mbaroni wakimiliki silaha kama vile visu.

Duru kutoka wizara ya afya zilisema kuwa afisaa mmoja wa jeshi aliuawa.

Bwana Morsi, aliyekuwa rais wa kwanza wa kiisilamu kuchaguliwa kidemopkrasia Misri, aling'olewa mamlakani na jeshi, siku ya Jumatano baada ya kufanyika maandamano makubwa.

Mmoja wa waandamanaji Mahmud al-Shilli, aliambia shirika la habari la AFP kuwa wanajeshi waliwarushia gesi ya kutoa machozi lakini kikundi cha wanaume waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliwafyatulia risasi.

Katika taarifa iliyosomwa kwenye vyombo vya yhabari vya serikali, jeshi lililaumu kikundi cha watu wlaiokuwa wamejihami ambao limesma ni mgaidi waliokuwa na njama ya kuvamia kambi ya jeshi.

Share:

WANAWAKE WAWILI WAMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA AFRIKA KUSINI WAKITOKEA TANZANI

Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.

Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.

“When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa.
Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller.
Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini.


Share:

MKE WA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA, MAMA ANNA MKAPA AMETENGWA...!!!

MAMA ANNA MKAPA.

MKUTANO wa wake za marais uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wazito, akiwemo Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush na Mkewe, Laura, umeacha kitendawili kizito kuhusu mke wa Rais wa zamani, Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa. Imebainika kuwa katika mkutano huo, ambao mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma alikuwa ni mwenyeji wao, Mama Anna Mkapa hakuhudhuria, lakini pia imeonyesha wazi kwamba hakupewa fursa kulingana na hadhi yake.

Mkutano huo wa Kimataifa ulifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, Juni 2-3 mwaka huu, uliozungumzia nafasi ya wanawake kuinuka kimaendeleo, ukizihusisha taasisi zinazoendeshwa na wake wa marais, wakiwemo wale wastaafu.



Gazeti moja hapa nchini lilibaini kuwa, katika mkutano huo kiligawiwa kitabu kilichobeba jina la ‘African First Ladies Summit’, kilichokuwa na orodha ya viongozi mbalimbali, wakiw
emo wake za marais na wake za marais wastaafu takribani 31, kikielezea wasifu na taasisi wanazoziongoza, lakini Jina la Mama Mkapa halikuwemo.



Katika kitabu hicho, Mama Mkapa, ambaye anaendesha Taasisi ya Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), jina lake kutokuwepo, baadhi wanaona kwamba Mkutano huo haukumpa fursa mama huyo, hasa kutokana na kazi kubwa ambayo imekuwa ikifanywa na taasisi yake hiyo ya kuwainua wanawake kama mazungumzo ya mkutano huo yalivyokuwa yameegemea.

Taasisi ya EOTF ni taasisi ya kwanza kuendeshwa na mke wa Rais hapa nchini, na ilianzishwa wakati Rais Benjamin Mkapa akiwa madarakani. Tangu ilipoanzishwa imekuwa ikijishughulisha na kuwainua wanawake kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali, ikiwemo ujasiriamali.

Tofauti na mama Anna Mkapa ambaye haijulikani kama alitengwa au alijitenga katika mkutano huo, lakini kitabu hicho kilielezea wasifu na shughuli zinazofanywa na wake za marais kama Mama Salma kupitia taasisi yake ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais Obama, Michelle ambaye juhudi zake amezielekeza katika kujenga jamii na familia kupitia mradi wake wa Let’s Move!.

Wengine ni pamoja na mke wa Waziri Mkuu wa zamani Tony Blair, Cherie Blair, Laura Bush na wengine.

MTANZANIA Jumapili lilimtafuta kwa njia ya simu msaidizi wa Mama Mkapa aliyetambulika kwa jina moja la Prisca, ambaye alikiri kuwa alipata mwaliko wa mkutano huo.

Kuhusu kutohudhuria, alisema hilo lilitokana na programu zake nyingi, ikiwa ni pamoja na banda ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya 37 ya biashara, Sabasaba ambako alikuwa na wageni wake.

Alipoulizwa mbona mkutano huo ni mkubwa sana huku Mama Salma pia akiwa na banda lake huko, lakini aliliacha na kwenda katika Mkutano, iweje kwa mama Mkapa, Prisca alisema hilo limetokana na kuwa na ‘programu’ zake nyingine.

Prisca alipoulizwa kama Mama Mkapa alialikwa katika mkutano huo, alisema kualikwa si tatizo, kwani anaweza kualikwa, lakini akawa na mambo mengine.

Alipoulizwa kama kuna tatizo kati ya EOTF na WAMA, alieleza kuwa hakukuwa na tatizo lolote, kwani hata katika kumpokea Mama Obama wakati alipotembelea ofisi za WAMA, Mama Anna Mkapa alikuwepo.

Prisca alisema kuwa hakuna tatizo kwa kuwa Mama Salma ni mke wa rais na Mama Mkapa alikuwa mke wa rais, hivyo hawana cha kugombea.

“Mama Salma akimwita Mama (Anna) kwenye ‘programu’ zake huwa anakwenda, vivyo hivyo kwa mama anapomwita mama Salma.

“Ninyi waandishi mambo madogomadogo kama hayo muwe mnayaacha na ndiyo yanawaweka katika matatizo na familia zenu, Mama Salma na Mama Mkapa wote wako ‘busy’ na hivi vitu naomba viishie hapo… kwanza umepata wapi namba yangu?” Alihoji Prisca.

Mkutano huo wa wake za marais, mbali na kuhudhuriwa na mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Cherie Blair, ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (Unaids), Michel Sidibé.

Baadhi ya wake za marais waliohudhuria pia ni pamoja na Mke wa Rais wa Uganda, Janet Museveni, mke wa Rais wa Msumbiji, Maria da Luz Dai Guebuza, mke wa Rais wa Sierra Leone, Sia Nyama Koroma, Balozi Nancy G. Brinker ambaye ni kiongozi wa kimataifa wa kupambana na ugonjwa wa kansa pamoja na wengine wengi.

Share:

RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AWAASA WAISLAMU NCHINI

dr ally mohammed shein

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amewataka Waislamu wote nchini kuishi na Watanzania wenzao katika misingi ya kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana, kama Uislamu ulivyofundisha.
Dk Shein aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa msikiti wa Masjid Taqwa, uliopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam, katika hotuba ilyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji MakameKatika hotuba hiyo ya ufunguzi wa msikiti huo, Dk Shein alisema kuwa ni wajibu kwa Waislamu kufanya kila jitihada katika kuilinda amani na utulivu alioubariki Mwenyezi Mungu hapa Tanzania.

Alisema kuwa kuna kila sababu kwa Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba wanaweza kufanya ibada zao katika mkusanyiko mkubwa kama huo wa ufunguzi wa msikiti bila ya hofu, woga wala bughudha ya namna yoyote.Dk Shein alipongeza jitihada zinazochukuliwa na wasimamizi wa msikiti huo katika kuimarisha na kuitunza historia yake tangu ulipoanzishwa mnamo mwaka 1927, ambapo historia hiyo inadhihirisha kuwa msikiti huo ni miongoni mwa misikiti mikongwe katika Jiji la Dar es Salaam.


Alitoa wito katika kushirikiana kuulinda na kuuendeleza msikiti huo wenye historia kubwa na kutoa shukurani kwa Yusuph Khamis Yusuph kwa busara aliyochukua ya kutumia sehemu ya kipato alichojaaliwa kwa kuisimamisha nyumba hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Dk Shein alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Waislamu kuzitayarisha nafsi zao kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao umebakiza siku chache kuingia ambapo Mwenyezi Mungu husogeza pepo kuwa karibu zaidi na waja wake.
Katika risala ya Waislamu wa msikiti huo, walisema zaidi ya Sh1.3 bilioni zimetumika kwa ujenzi huo. Viongozi mbalimbali wa dini na Serikali kutoka Zanzibar na bara walihudhuria wakiwamo Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji, Sheikh wa Dar es Salaa, Alhadi Mussa na Mbunge wa Ilala, Mussa Azan ‘Zungu’.

Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive