Wednesday, 19 June 2013

MDADA ACHEZEA KICHAPO KWA KUFANYA UKAHABA JIRANI NA MSIKITI...!!!

Richard Bukos na Issa Mnally

KHAAA! Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ iliyo chini ya Global Publishes, ipo mzigoni na hivi karibuni imenasa tukio la aina yake ambapo mke wa mtu amechezea kichapo ‘hevi’ akidaiwa kufanya ukahaba jirani na msikiti, Risasi Mchanganyiko lina kisa kamili.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu majira ya usiku jirani na msikiti huo uliopo nyuma ya Corner Bar, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanamke huyo na wenzake walikamatwa na baadhi ya vijana waumini wa Kiislamu waliokerwa na kitendo cha wao kutoa huduma haramu ya ngono maeneo hayo.


NGUO YA NDANI YAMVUKA
Wakati mwanamke huyo akicharazwa bakora, nguo ya ndani ilimvuka huku akipiga kelele kuwa hatarudia kufanya hivyo na kama akirudia basi akatwe kichwa.

NI KERO
Kutokana na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti huo, waliamua kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo hicho cha polisi.
“Tumeamua kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa, wanakojoa na kutupa kondomu hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.
Mmoja wa vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia mapaparazi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.

KUNA KISA NA MKASA
Alisema kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose kuhudhuria swala siku hiyo.

BOFYA HAPA KUSIKIA MAHOJIANO
Gazeti hili liliambatana na vijana hao hadi polisi ambapo lilipata nafasi ya kuzungumza na mwanamke huyo.
Risasi Mchanganyiko: Mama kwani wewe unaitwa nani na kwa nini unajiuza eneo lile?
Mwanamke: Naitwa Zulfa, unajua maisha ni magumu hata ninyi mnajua. Ni kweli mimi ni mke wa mtu lakini mume wangu hana kazi hivyo kuliko kulaza watoto njaa naogopa watakufa.
Risasi Mchanganyiko: Mume na watoto umewaacha wapi?
Zulfa: Mume naye anabangaiza mtaani, watoto wangu wawili nimewaacha nyumbani Manzese wamelala.
Risasi Mchanganyiko: Kwa nini usitafute njia nyingine ya kutafuta kipato kuliko kujiuza kwa sababu unahatarisha maisha na haya magonjwa ya siku hizi?
Zulfa: (kwa ukali), acheni maswali yenu kama mna hela nipeni nitaacha.

AINGIZWA LOKAPU
Hata hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.

NI SIKIO LA KUFA
Habari zilizolifikia gazeti ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa na kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini ya shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado wanaendelea na biashara hiyo maeneo hayo.

DAR INATISHA
Biashara haramu ya ngono imekuwa kwa kasi ya ajabu jijini Dar na utafiti wa mwaka juzi ulionesha kuwa kulikuwa na wanawake wanaojiuza zaidi 7,500 lakini kwa sasa ni maradufu, chanzo kikielezwa ni ukosefu wa ajira.
NA GLOBAL PUBLISHER

Share:

JOHN MNYIKA KUWASHA MOTO MWINGINE ARUSHA

WAKATI Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ikiendelea kumsaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema,Mbunge wa Ubungo John Mnyika kesho atawasha moto mwingine wa maombolezo uliotawanywa kwa mabomu jana.



Mnyika atakuwa msatari wa mbele kuongoza wafuasi wa Chadema kuaga miili ya watu watatu waliouawa katika shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Soweto.


Mbali na Mnyika zoezi hilo pia litasimamiwa na wabunge wanne wa Chadema walioachiwa huru kwa dhamana leo kwakua upelelezi wa kesi zao hazijakamilika.

wabunge hao waliachiwa huru kwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani hapo kabla ya kufikishwa Mahakamani na kutakiwa kurudi Polisi Julai 22 mwaka huu .


Wabunge hao Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu), walipewa dhama hiyo majira ya saa nane mchana.



Kabla ya Wabunge hao kuachiwa huru kwa dhamana, maelfu ya wafuasi wa Chama hicho walijazana katika Mahakama hiyo wakisubiri msafara wa wabunge hao, na mara baada ya kupewa taarifa kwamba wabunge hao wameachiwa huru wakiwa Polisi,maandamano makubwa yakaelekea katika Kituo cha Polisi.

Akizungumza baada ya dhamana hiyo Tundu Lissu alisema kwamba, Jeshi la Polisi limempa hasara kubwa baada ya kuvunja mawani yake na kwamba hivi sasa hawezi kufanya kazi yoyote mpaka atakapo pata mawani mapya.


Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliyefika jijini Arusha kwa ajili ya kuwawekea dhama wabunge hao alisema kwamba, Chama hicho bado kitaendelea na mipango yake ya kuomboleza na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu waliouawa kwa shambulio la bomu katika mkutano wa kisiasa wa Chama hicho Juni 15 mwaka huu katika Uwanja wa Soweto, marehemu hao ni pamoja na Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally, waliofariki kwenye mlipuko wa bomu.


Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutoka Polisi Mnyika alisema, "Kesho tutaendelea na zoezi la kuwaaga wenzetu waliofariki dunia katika mkutano wetu, na watazikwa kwa heshima zote za Chama,zoezi litaanzia kanisani kabla ya kwenda katika eneo maalum ilipoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho".

Hata hivyo Mnyika alikataa kujata jina la kanisa muda wala eneo iliyopangwa kwa madai kwamba ni mapema sana.


Share:

LUNDENGA AMTIMUA MREMBO JUKWAANI BAADA YA KUTINGA NA KIVAZI CHA NUSU UCHI...!!!

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss Morogoro 2013, Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini hapa wakati mrembo huyo alipokuwa akiwania kuvaa taji la mkoa huo.

Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili na kanuni za mashindano hayo kwa kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima ya Miss Tanzania.
Baada ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na kamati yake walikubaliana kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu wa shindano, Alex Niktasi na kumtaka amuondoe haraka.
Mbali na Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel (20) kutokana na kushiriki shindano hilo mara mbili mwaka huu, inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha.
Lundenga alipohojiwa na waandishi wa habari alisema kamati yake inataka kuendeleza nidhamu tangu ngazi ya chini, hivyo hawawezi kuruhusu utovu wa nidhamu.

Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive