Saturday, 18 April 2015

Wanafunzi waliopigwa na radi kufuatia mvua iliyonyesha mkoa wa kigoma wazikwa.

Mkuu wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya  amewaongoza mamia ya wakazi wa manispaa ya kigoma ujiji  kuaga miili ya watu wanane wakiwemo wanafunzi  sita wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya kibirizi mjini kigoma walio fariki dunia jana baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua iliyonyesha kwa takriban masaa matatu.
Majonzi yalitawala shughuli hiyo  hasa baada ya miili hiyo kupokelewa katika viwanja  vya  shule ya msingi kibirizi kabla ya ndugu kukabidhiwa tayari kwa maziko huku mwili wa Mwalim Elieza Mbwambo ukisafirishwa kwenda moshi kwa maziko .
 
 Akitoa salam za rambirambi mkuu wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewataka wafiwa na wananchi kuchukulia  tatizo hilo kama ni tukio la ajali ya kawaida na kwamba msiba huo ni mzito.
 
Kwa upande wao viongozi wa dini Shekh Moshi Guoguo kutoka Bakwata na mchungaji Emmanuel Mtoi wa kanisa la KKKT wakitoa mawaidha katika msiba huo, wamewataka waumini wa dini mbalimbali kujiandaa kwa kuwa kila mwanadamu ataonja mauti  kwa wakati wake na kwamba imani za kishirikina zisihusishwe katika msiba huo.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive