li kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo
na wananchi kupata ulemavu,chama cha ACT wazalendo kimeitaka serekali
kutoa taarifa ya tume ya uchunguzi wa ajali za barabarani zilizo fanyiwa
utafiti ili kuweza kutafuta namna yakutatua matatizo ya ajali za mara
kwa mara.
akiwahutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Singida na viunga
vyake kwenye mkutano wa kunadi chama cha ACT kiongozi mkuu wa chama
hicho Bwana. Zitto Kabwe ,amesema aliyekuwa waziri wa uchukuzi Dk
Harsson Mwakyembe aliunda tume ya uchunguzi wa ajali na mpaka sasa
majibu hayaja tolewa,jambo ambalo limekuwa likisababisha ajali kuendelea
kutokea na kwa kipindi cha mwenzi Mach na April mwaka huu zaidi wa watu
mianane wamesha poteza maisha kwa ajili ya ajali.
Katika hatua nyingine Bwana. Zitto Kabwe ameitaka serekali
kuhakikisha inawabana wamiliki wa mabasi kote nchini ,watoe mikataba
ya kazi kwa madereva wao ili waweze kujulikana, kwa kufanya hivyo kuta
punguza ajali ambazo siyo za msingi.
Awali mwenye kiti wa chama cha ACT Bi.Anna Mghwira na kada wa chama
hicho Bwana Selemani Msindi maarufu kwa jina la Afande Sele wamesema
huduma nyingi hasa za afya wakati wa zamani zilikuwa zikipatikana
kulingana na uwezo wa serikali wakati ule, na kwasasa nchi imekuwa na
utajiri mwingi wa madini ,kilimo na biashara,lakini cha kushangaza fursa
hizo zimekuwa zikitumiwa na baadhi ya watu na kuwaacha wananchi wengi
wakiwa masikini.






