Tuesday, 21 April 2015

Serikali yatakiwa kuvishirikisha vikundi vya uhamasishaji kukabiliana na mauaji ya imani za kishirikina.

Vikundi vya vijana vinavyotumika kuhamasisha jamii kwenye majukwaa ya kisiasa vikijengewa uwezo vina uwezo mkubwa wa  kusaidia kuelimisha jamii kuondokana na imani za  kishirikina ambazo licha ya kuwa kikwazo cha maendeleo zimekuwa chanzo kikubwa cha umwagaji wa damu .
Akizungumza katika ibada maalumu ya kuhamasisha jamii kujiepusha na vitendo vya kishirikina iliyoanadaliwa na wadau mbali mbali kwa ushirikiano na kanisa la Pentekost   kamanda wa vijana wa mkoa  wa Arusha Bw. Philemon Molllel amesema baada ya kubainika kuwa ushirikina ndio msingi mkuu wa mauaji ya walemavu wa ngozi,vikongwe,na maovu mengine  katika jamii kinachohitajika ni kushirikiana na kuhamasishana kuutokomeza kazi  ambayo  vikundi hivyo vinaiweza.
 
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakiwemo wanaounda vikundi vya uhamasishaji wamesema  wakiwezeshwa na kushirikishwa kupunguza vitendo hivyo ni jambo linalowezekana kwani yote hayo ni matokeo ya mmomonyoko wa maadili tatizo ambalo ufumbuzi wake ni kuelimisha jami
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive