Tuesday, 21 April 2015

Waziri wa TAMISEMI ameitaka mifuko ya jamii kusaidia watumishi kupata makazi.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu serikali za mitaa na tawala za mikoa TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii nchini isaidie watumishi kupata makazi hasa sekta ya afya ili waweze kutoa huduma bora na kwa wakati muafaka.
Mh Ghasia ametoa wito huo jijini dar es salaam wakati wa utiliaji saini makubaliano kati ya shirika la elimu kibaha na watumishi HOUSING kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma zinazotarajiwa kujengwa ndani ya eneo la shirika hilo ambapo amewataka kulenga maeneo yenye upungufu mkubwa wa nyumba za watumishi.
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa NHC Dk. Fred Msemwa amesema kupitia ubia huo katika kipindi cha miaka mitano watajenga nyumba 1,150 pamoja na miundombinu mingine inayoendana na huduma za jamii na hivyo kutawawezesha wafanyakazi mbalimbali waliopo ndani na nje ya kibaha kunufaika na kuongeza kuwa nyumba hizo watauziwa watumishi wa umma na baadae wananchi wa kawaida kwa masharti nafuu.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive