Ni siku 9 sasa tangu mkasa wa Shambulizi la magaidi kutokea katika Jumba
la kibiashara la Westgate mjini Nairobi, Kenya. Serikali imeandaa
maombi ya kitaifa yanayojumuisha dini zote kuombea usalama wa nchi
Viongozi wa dini mbali mbali wamekusanyika katika uwanja wa jumba la KICC kwa maombi ya kitaifa kuombea nchi, manusura na jamaa za waliopoteza wapendwa wao kwenye shambulizi la magaidi Shambulizi hilo lililofanyika tarehe 22 mwezi huu. Maombi hayo yamehudhuriwa na wakuu wa serikali wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Rutto, mawaziri na wabunge.
Bado kuna maswali mengi yaanyostahili majibu kuhusu namna serikali ilivyolishughulikia shambulizi hilo
Pia viongozi wa upinzani wa muungano wa CORD wakiongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga akiandamana na viongozi wa vyama tanzu wa muungano huo, aliyekuwa makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na wengineo walijumuika pamoja katika uwanja wa jumba la mikutano ya Kimataifa KICC.
Maombi hayo yanahudhuriwa na viongozi wa didi mbali mbali wakiwemo wakristo, Waislam,
Wahindu na dindi nyinginezo. Viongozi wa dini ya
kiislam wameendelea kukikashifu kitendo
hicho cha magaidi na kusihi vyombo vya usalama kutohusisha ugaidi na
Uislam.. Huku maombi hayo yakiendelea kundi la wataalam wa uchunguzi
kutoka mataifa mbali mbali wanaendelea na uchunguzi wao katika jumba la
Westgate Mall kutafuta ushahidi kuhusiana na shambulizi hilo.
Maafisa kutoka Uingereza, Ujerumani Marekani, Israel na Canada
wakishirikiana na wenzao kutoka Kenya wanaendesha shughuli iliyoanza
Jumatano iliyopita. Maswali mengi hadi sasa hayajapata majibu kuhusiana
na shambulizi hilo lililodaiwa kuteklelezwa namagaidi wa kundi la
Al-Shabaab walio na uhusiano na kundi la magaidi la Al-Qaeda. Washukiwa
tisa bado wanahojiwa na polisi kuhusian na shambulizi hilo. Serikali
imesema magaidi 5 waliuawa kwenye shambulizi hilo ingawaje hadi sasa
hakuna hata maiti moja ya magaidi hao iliyotambuliwa.





