Saturday, 27 July 2013

STAA WA BONGO MOVIES DUDE ANASWA NA DEMU MWINGINE

STAA wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenaswa na demu mwingine aitwaye Mboni Mhando tofauti na mkewe anayeshi naye, Eva
Dude na demu huyo aliyebainika kuwa ni msanii, walinaswa juzikati katika Hoteli ya Traventine Magomeni, jijini Dar wakijivinjari katika mikao ya kimalovee ambapo paparazi wetu alitumia kifaa maalum cha kupigia picha na kuwanasa bila wao kujijua.
Baada ya kuzinasa picha hizo, paparazi wetu alimvaa Dude na kumuuliza kulikoni agandane na demu huyo wakati ana mkewe nyumbani, alichomoa kuwa siyo demu wake bali ni msanii mwenzake eti wanapanga mipango ya kazi.

Hapa tulikuwa tunapanga mipango ya kufanya filamu, huyu ni msanii tena wa siku nyingi sababu aliwahi kucheza kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu miaka ile,” alisema Dude huku akimsihi paparazi afute picha kama amekwisha piga.
.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive