Wednesday, 20 May 2015

Wanafunzi wa vyuo watoa tamko NEC kuhusu mkanganyiko wakati wa kupiga kura kwa watakaokuwa nje ya maeneo waliyojiandikishia

Katika kuelekea uchaguzi mkuu, umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa Chadema kupitia  baraza la vijana wa chama hicho mkoa wa Tabora wametoa tamko la kuitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuweka bayana namna ambavyo wanafunzi wataruhusiwa kupiga kura mahali popote walipo kwakuwa siku ya kupiga kura vyuo vitakuwa vimefungwa na wengi wao kurejea makwao hatua ambayo wamedai kuwa itawanyima haki hiyo kwakuwa sisehemu waliyojiandikishia kupiga kura.
Wakizungumza na ITV katika ofisi za Chadema kanda ya magharibi   mjini Tabora, viongozi wa Bavicha na Chaso, wameonesha wasiwasi mkubwa wa kudai kuanza kwa mizengwe ya kunyimwa haki ya kupiga kura kutokana na mkanganyiko katika fomu ya maombi ya utambulisho wa mpiga kura inayotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi   wanazotakiwa kujaza  na wanavyuo, na utaratibu mzima wa zoezi la uchaguzi litavyoendeshwa wakilinganisha na lile la uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hasa kwa kufungwa vyuo na wanafunzi kurudi  makwao  maeneo ambayo kimsingi hawakujiandikishia katika daftari la kudumu la mpiga kura.
 
Katibu wa Chadema mkoa wa Tabora Bw.Alinanuswe Edson ameiomba serikali kulishughulukia mapema suala hilo ambalo amedai huenda likaleta mzozo ambao pengine ukasababisha athari kubwa hususani kwa vijana.
 
Aidha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 baadhi ya wanafunzi wa vyuo  imedaiwa kuwa hawakupata fursa ya kupiga kura ipasavyo  kutokana na kuwepo kwa mkanganyiko uliosababishwa na kuondoka  maeneo ambayo walijiandikishia kupiga kura na hivyo kuleta usumbufu mkubwa katika kuteleza haki hiyo ya kimsingi.
Share:

Follow Us

Random Posts

BTemplates.com

Powered by Blogger.
The Magazine

Facebook

Total Pageviews

Random Posts

Recent Comments

Recent Posts

Popular Posts

Blog Archive